Nina mawazo tofauti sana na mtoa mada.
Kwangu kipindi kigamu na cha taabu basi ni hiko cha huyo mnaemsifia.
Ugumu wa maisha Tanzania ulianzia kwakwe.
Hakukua na ajira za kutosha serikalini, mbaya zaidi hta Yale makampuni na taasisi za watu binafsi zilizotoa ajira nyingi zilifungiwa. Hapo wengi walionja joto la jiwe kwa ugumu wa maisha.
fursa za kujiajiri zilikuwa finyu kutokana na mzunguko mdogo wa pesa. Kipindi hicho mtu kuingiza pesa ilikuwa ni ngumu Sana. Ukuaji wa miji na watu kujenga Kama zamani kulipungua kutokana na ugumu wa maisha, ila watu wamesahau tu.
Huyu bwana alipenda kujisifu kwa kile alichokifanya. Yaani kamradi kadogo tu basi ndio inakuwa wimbo wa kumsifu. Miradi mingi Kama UDOM, mwendo Kasi, daraja la kigamboni, barabara za mikoani, shule za kata, na miradi mingi sana haikujengwa kipindi chake lakini ilikuwa kimyaa yaani kama hakukua na kinachoendelea.
Uongozi ule ulikuwa una mambo ya kushangaza Sana. Yaani ajira za walimu 400 zikitangazwa basi inakuwa nayo ni sehemu ya kumsifu yeye. Nilikuja kuuchukia mara baana ya ajira flani kutoka lakini majina karibia nusu kuwa ni majina hewa. Yaani unaona namba ya shule ndio ile ile shule yako tena mwaka ndio ule ule uliomaliza lakini jina la aliepata kazi hata hulijui, tena ile namba yake haikuwepo kwenye list ya waliofanya mtihani pale. Yaani unakuta namba ya mwisho ilikuwa 75 lakini huyo mtu namba yake 508. AU MMESAHAU?.
Ona Sasa hivi mama anavyomwaga ajira, vyuoni, taasisi za umma, serikalini za mitaa na kwengineko tena bila kujisifu, just imagine ajira hizi ndio ingekwa kipindi kile ingekuwaje. Lakini kimya watu wanakula mema ya nchi. Na miradi ya nchi inaendelea.
Haikuwa rahisi kuona hata tangazo la kazi kwenye mfumo wa ajira, lakini ona Sasa? Tunafeli wenyewe tu.
Yule bwana amesababisha vijana wengi wakae mtaani bila kazi tena kwa muda mrefu sana.
Kuna mengi mema ameyafanya lakini si ndio awe rahisi Bora Tanzania.
NB: kwangu kiungozi Mh Samia Ni far more best than him