Hayati Rais Magufuli ningejua ungekufa ghafla vile ningekuwahi unipe Spirit yako ili niipandikize kwa Marais wajao wa Tanzania

Hayati Rais Magufuli ningejua ungekufa ghafla vile ningekuwahi unipe Spirit yako ili niipandikize kwa Marais wajao wa Tanzania

Kuna kitu watanzania Hawakipendi ulegelege na upigaji wa viongozi katika miradi ya maendeleo ya wananchi ndio maana wanamkumbuka.
 
fanyeni kazi,ni kazi ndio zinambeba jamaa mpaka leo.
Kumbuka mema yote aliyoyafanya Magu ni kwa faida ya watanzania wote na kama Kuna mabaya basi pia ni kwa wote, sina chuki tu na Magu but binafsi uongozi wake sikuuelewa hata kidogo, na huo ni msimamo wangu. Sio lazima wewe uukubali.

Kama wewe ulimpenda basi ni wewe sio lazima unilazimishe mimi nimpende pia au niukubali uongozi wake.

Kwangu mama ni bora mara buku kiuongozi.
Nikikumbuka ya kina sabaya, makonda, hali ya ajira, maisha magumu (vyuma kukaza), taasisi binafsi kufukuzwa, Kujuana katika ajira kwa kigezo cha kabila na chama hua sioni haja ya kuupenda uongozi ule.

Kaka yangu alimaliza chuo tangu 2015 ualimu na hakua na kazi, then Kuna UVCCM pale chuoni kwetu walimaliza 2019 na kupewa kazi wakati qualifications ni zilezile, na kumbuka hiyo kazi haikuwa ya usaili.

Yaani Kuna uhuni mwingi kipindi kile mpaka nasema mama ni bora sana
 
Kumbuka mema yote aliyoyafanya Magu ni kwa faida ya watanzania wote, sina chuki tu na Magu but binafsi uongozi wake sikuuelewa hata kidogo, na huo ni msimamo wangu. Sio lizima wewe uukubali.
unadhani naweza hata kufikiri au kushawishika!!!
Kama were ulimpenda basi ni wewe sio lazima unilazimishe mimi nimpende pia.
hata kudhani unalazimishwa huo nao ni ugonjwa.
Kwangu mama ni bora mara buku kiuongozi.
mama ni bora au utawala wake ni bora!!!
 
unadhani naweza hata kufikiri au kushawishika!!!

hata kudhani unalazimishwa huo nao ni ugonjwa.

mama ni bora au utawala wake ni bora!!!
Vyovyote, lakini wapo watu wanaochukia kuona Mh. Samia anafanya vizuri. Huu ni ugonjwa.

Mimi si mshabiki wa yeyote but naomba uongozi huu wa Mh. Samia uwe mzuri kupita uongozi wowote tangu Uhuru ili maisha bora kwa watanzania yapatikane.
 
Vyovyote, lakini wapo watu wanaochukia kuona Mh. Samia anafanya vizuri. Huu ni ugonjwa.

Mimi si mshabiki wa yeyote but naomba uongozi huu wa Mh. Samia uwe mzuri kupita uongozi wowote tangu Uhuru ili maisha bora kwa watanzania yapatikane.
Na uongozi utakaokuja baada yake uwe mzuri zaidi, ili tu maisha yawe bora
 
Wanasema JPM alikuwa muuaji, Wangapi wamekufa na watakufa kutokana ukosefu wa maji, umeme, biashara ngapi zitakufa, wangapi watafunga biashara wanaotegemea umeme , maji.

Miradi yote ya kimkakati ya JPM sasa hivi inasuasua elimu bure, mikopo kwa wanafunzi, ujenzi wa hospitali, bwawa la umeme, barabara, maji kila kitu alichotaka wananchi wapate bure au kwa bei nafuu sasa hivi vyote ni ghali sana au hauvipati kabisa.

Awamu ya sita inafanya kinyume cha JPM. Mkakati wao ni mmoja Tu. Kuiba as much as possible. Hawajali kitu kingine chochote, maisha ya wananchi wengi.

Bata, porojo, mipasho, uchawa, propaganda ndio Sera yao.
 
Uzuri ni kwamba sikuwahi kuwa mnafiki juu ya kumkubali JPM since akiwa madarakani na sasa hayupo. Binadamu tuwe na tabia ya kumkubali mtu na mazuri yake pindi angalipo hai ili kumtia moyo kwa kile anachokifanya, kinyume chake wengi waliomvunja moyo JPM leo hii ndio wanamkumbuka kwa kasi.

Ukifuatilia kwa makini utagundua kila alichokifanya JPM kilikuwa ni kwa maslahi ya nchi na wananchi kwa ujumla, haijalisha kuna watu waliumia, kufilisika, kushuka vyeo au kupoteza madaraka. Badala yake alizushiwa mengi mabaya ili kuonekana hafai.
You've nailed it Chief.
 
Back
Top Bottom