Hayawi, Hayawi, Yamekuwa! Wakristo wa Uongo Tayari Wametokea

Hayawi, Hayawi, Yamekuwa! Wakristo wa Uongo Tayari Wametokea

Kwa sasa tunamtarajia Yesu kuja kuwanyakua watu wanaomwamini na ambao wanaishi maisha matakatifu. Atakapokuja ataishia mawinguni. Unyakuo huo utafanyika ghafla, kufumba na kufumbua, hivyo sio kila mtu atamwona Yesu wakati huo. Kitabu cha 1 Wakorintho 15:51-52 kinasema:
"Angalieni! Nawaambieni siri; hatutalala sote[hatutakufa wote], lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho; maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa..."

Katika kitabu cha 1 Wathesalonike 4:16-17 tunasoma tena hivi:
"Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko wa kutisha, pamoja na sauti ya malaika mkuu, pamoja na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele."

Katika tukio hilo la unyakuo, waliookoka tu ndio watakaonyakuliwa na kwenda na Yesu mbinguni. Watu wa dunia watashangaa kwa sababu ghafla wataona kuna watu wametoweka. Watakaoachwa watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Baadaye Yesu atakuja tena duniani pamoja na watakatifu wake kwa wazi na utukufu, na kila jicho litamwona. Katika Mathayo 24:30 tunasoma hivi:
"Ndipo itaonekana ishara ya Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya dunia watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na uweza na utukufu mwingi."

Kitabu cha Ufunuo 1:7 kinasema pia kwamba:
"Tazama! Anakuja na mawingu, na kila jicho litamwona, na hata wale waliomchoma; na kabila zote za dunia zitamlilia kwa uchungu. Naam, Amina."

Nimeeleza kwa muhtasari tu. Kuna matukio mengine zaidi ya hayo. Lakini tukio muhimu sana kwa sasa ni hilo la unyakuo. Ukikosa kunyakuliwa na Yesu utalia na kusaga meno.

Confess your sins, today, repent, believe in Jesus Christ, accept Him as your Lord and Savior, and live according to His Word. Siku ya unyakuo ikifika utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa na kuurithi uzima wa milele. Ubarikiwe🙏
naomba niulize wewe ni msabato ?
 
Angalie
Wakuu, heshima zenu. Mna habari kwamba unabii huu nao tayari umetimia?
Mathayo 24:24 – "Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, ikiwezekana, hata walio wateule.”
Marko 13:6 – "Wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye[Yesu Kristo],’ nao watawadanganya wengi."

Tumezoea kusikia Manabii wa uongo kuliko Makristo wa Uongo. Makristo wa Uongo kwa Kiingereza ni “false Christs.” Hao ni watu wanaodai kuwa wao ni Kristo lakini wanawadanganya watu kwa mafundisho ya uongo na miujiza feki

Hizi ni baadhi ya Sifa/Tabia za Makristo wa Uongo:
  • Wanadai wao ndio Yesu aliyerudi.
  • Wanapotosha mafundisho ya Biblia
  • Wanatenda ishara za uongo kwa kutumia ujanja, miujiza feki au hata kwa kutumia nguvu za giza(mapepo) ili kuwashawishi watu wawaamini
  • Wanajiinua juu ya Kristo badala ya kuwaelekeza watu kwa Yesu. Wanatafuta kuwa na mali, umaarufu, kuheshimiwa na kuwa na “power”
Hawa ni Baadhi ya Makristo wa Uongo Waliopo katika nchi mbalimbali:
Apollo Quiboloy wa Philippines

Anadai kuwa yeye ni "Mwana wa Mungu.” Mwaka 2021, Quiboloy alishtakiwa kwa kosa la kuwalazimisha wasichana na wavulana wajihusishe na ngono na kuwatishia kwamba wasipofanya hivyo wataangamia milele!

Alan John Miller wa Australia
Anadai kuwa yeye ni Yesu aliyerudi katika mwili mwingine. Mke wake Mary Suzanne naye anadai ndiye Mariamu Magdalene(Mary Magdalene).

Inri Cristo wa Brazil
Anadai yeye ni Yesu aliyerudi mara ya pili; na ana wafuasi.

Jung Myung-seok wa Korea Kusini
Anadai yeye ni Yesu aliyerejea mara ya pili, na kwamba yupo ili kukamilisha kazi iliyokuwa haijamalizika. Jung aliwahi kupatikana na hatia ya kubaka na kutumikia kifungo cha miaka 10.

Oscar Ramiro Ortega-Hernandez wa Marekani
Ortega-Hernandez alijitaja mwenyewe kuwa ni Yesu Kristo aliyetumwa kuja kumuangamiza aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani kwa madai kwamba ni Mpinga Kristo. Mwaka 2011 Ortega alikamatwa kwa kosa la kupiga risasi jengo la Ikulu ya Marekani.

Yesu wa Tongaren, Kenya
Hivi majuzi, huko Kenya alijitokeza mtu anayedai kuwa yeye ni Yesu. Wakati fulani wa Pasaka, vijana wa Kenya(Gen Z) walimtaka akubali kusulibiwa msalabani kama kweli yeye ni Yesu!

Ndugu zangu, Biblia ni kitabu cha kweli. Yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita, tunaona yakitimia waziwazi katikati yetu. Unabii huo wa kuja kwa Makristo wa Uongo nao umetimizwa. Hiyo ni dalili kuwa Yesu amekaribia kurudi. Yesu atakaporudi, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliofanya mambo haya:
  • Waliotambua kuwa ni wenye dhambi (Warumi 3:23).
  • Wanaokiri na Kuamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zao (Warumi 5:8).
  • Waliotubu dhambi zao na kuziacha (Matendo 3:19).
  • Waliompokea Yesu mioyoni mwao kwa imani atawale maisha yao (Warumi 10:10-13).
  • Wanaoishi maisha mapya ya utakatifu katika Kristo (2 Wakorintho 5:17).
Mimi ni miongoni mwao. Wewe je?
Act swiftly before time eludes you. Do not be beguiled by the fleeting pleasures of this world, for they are merely a passing illusion. In heaven awaits an eternal and incomparable bliss.
Angalieni mtu asije kuwadanganya, wengi watakuja kwa jina langu, wakisema ndiye Kristo, ndiye Kristo kwelii ,vilevile mimi ninasema vita mitetemo njaa vitatokea, watu watasalitiana vita huku na huko vyaja sikika
 
Angalie

Angalieni mtu asije kuwadanganya, wengi watakuja kwa jina langu, wakisema ndiye Kristo, ndiye Kristo kwelii ,vilevile mimi ninasema vita mitetemo njaa vitatokea, watu watasalitiana vita huku na huko vyaja sikika
wewe ni dheheb uh gani mkuu
 
Hapana. Yesu hakuoa. Mary Magdalene(Mariamu Magdalene) alikuwa mmojawapo wa kinamama waliomfuata Yesu na kumhudumia(Luka 8:1-3). Biblia inasema kwamba Yesu alimtoa pepo saba(Luka 8:2, Marko 16:9).
DAN Brown katika ,The Davince code,amesemaje pale?
 
Back
Top Bottom