Head of East African peacekeeping force in DRC resigns, citing harrassment

Head of East African peacekeeping force in DRC resigns, citing harrassment

Kagame anakuzwa sana, mtu tumemfundisha wenyewe...
Kama umemfundisha nenda kamkamate!! Congo Waasi wana Silaha za Kisasa na Zana za Kivita lukuki , 1. Zinawafikiaje? 2.Wana magari Mafuta yanawafikiaje?3. Rwanda wana kiwanda cha kuprocess dhahabu japo awana machimbo yake- sustainability ya hichi kiwanda ina hakikishiwa na gold toka wapi? Ni hayo tu kwa sasa
 
Kwani Tanzania tumelipwa shingapi na Uganda, Msumbiji au Seychelles? Maana Marekani ikipigana huko Chad ila ikachota mafuta kupitia Exxon Mobil tunasema ni uporaji ila Kwa ngozi nyeusi tunasema wanafidia gharama zao!!
Kwani Zimbabwe ni Tanzania? Kila kinachofanywa na Zimbabwe ni lazima kifanywe na Tanzania. Zimbabwe ilikuwa na wanajeshi hadi 12,000 ndani ya Congo kwa wakati mmoja na hiyo ilikuwa 30% ya jeshi la Zimbabwe tena wamekaa miaka mingi, wapi Tanzania iliwahi kuwa na wanajeshi hata 5,000 kwa wakati mmoja wakipigana sio kulinda amani, wapi Tanzania iliwahi peleka msaada wa Airforce, wapi Tanzania ilijitolea kupigana na wanajeshi wake zaidi ya 200 wakafa.

Tanzania ilikuwa na mission nyepesi pale Seychelles kwanza visiwa vidogo wakati DRC kubwa zaidi ya mara mbili ya Zimbabwe. Kuzuia mapinduzi si ni confrontation ya kutumia hata chini ya wiki. Hakuna mapinduzi yanafanyika kwa miezi, siku moja hadi tatu zaidi ya hapo ikifika mwezi hao ni kundi la waasi sio jeshi au mamluki wanaopindua serikali. Kinachobaki ni kulinda amani na kusubiri watulie kisha mnarudi.

Uganda ulitaka tulipwe nini kwani ilikuwa hisani ile? Si ni kiherehere cha Mwalimu Nyerere kuhifadhi waasi dhidi ya Iddi Amin. Wewe uliona wapi Rais anapinduliwa kisha anapata hifadhi nchi jirani na makamanda wake wanamfuata kupiga kambi na mafunzo wanapatiwa. Tulifanya kazi ya kulinda mipaka yetu sasa Uganda itulipe nini.
Na kwani hujui Uganda walitulipa war reparations walimaliza kulipa miaka ya 2000s around 2006 au 2008 kama nakumbuka vizuri.

Kwahiyo mkuu unatetea hao wazungu kina Exxon Mobil kisa Zimbabwe? Hiyo ni whataboutism
"kwanini umeiba?" === "mbona na fulani kaiba"
 
Ina maana anahofia hujuma kutoka ndani (ambazo ndio mbaya zaidi) kuliko kutoka kwa waasi hata wasiomfahamu vyema.
Taarifa vyanzo vingine vya habari inasema serikali ya DRC yenyewe ndio ilitaka aondolewe. Ni mpuuzi au tuseme jeshi la Kenya limeenda kupiga picha hamna kitu linafanya. Tangu wameenda kule M23 inachukua maeneo kuliko hata wasingeenda, Wakenya kazi kupiga picha na kuita press.

Serikali ya Congo haikuomba walinda amani, hao wapo ni UN. Yenyewe iliomba peace enforcement na waasi wakigoma basi nguvu itumike. Sasa hawa Wakenya ni kama wanasiasa pale ndio maana Uganda iliwacheka tangu hawajafika ilijua hawa hamna kitu. Wamenikera wakati wanaenda nilijua wana jipya kumbe hamna lolote. Wanafaa sare zinang'aa na helmets na modern small arms kumbe wako location na makamera.

Mwezi Februari kwenye mkutano Rais Felix alisikika akisema pembeni na huyo Maj. Gen. Nyaghah alimwambia hivi ...
"Don't favour the M23. It would be a shame if the population took it out on you. You have come to help us and not to have problems, be attentive to this, communicate with the population"

Sijui kulikuwa na mazingira gani mpaka akasema don't favour the M23.
 
Ajira za upendelro na kujuana Vyeo vya kupeana kwa kujuana

Matokeo ndio hayo unakuta mtu.licheo kubwa kijeshi ukimpelreka vitani lioga kama kuku wa mdondo

Matokeo ndio hayo Mtuj jeshini apate kazi kihalali apite mafunzo kihalali na apande vyeo kihalali
Tatizo hilo ndilo limelight hata jeshi la Urusi hadi linakodi jeshi binafsi la Wagner liwasaidie
Na pia nimeona anapata watetezi wengi. Kamanda anayekimbia vita ni mlenda wa nazi kabisa.

Unapoingia jeshini lazima uadmit kuwa kifo ni sehemu ya job description. Sasa commander anashindwa kuongoza vikosi vya kulinda amani kwa sababu anahofia kufa.

Woi
 
Jana hiyohiyo Major General Alphaxard Muthuri Kiugu kateuliwa kuwa mkuu wa EACRF-DRC kujaza nafasi ya Major General Nyaghah
Ngoja tuone huyu atakuwa na jipya gani...

Ila bado Kenya ina jeshi bora sana ukanda huu hasa kivifaa na kimafunzo.
 
Congo pasikie tu, hivi vita na utitiri wa waasi ni mipango ya watu wengi wenye nguvu ndani na nje ya Africa.

Hasara ya kuwa na nchi kubwa isiyo na jeshi imara ndiyo hii. FARDC ina mamluki kibao na makamanda wengi ni wala raha tu.

Ukienda PKO omba Mungu umalize muda wako urudi bongo tu.
Miaka kadhaa Lt. General James Mwakibolwa aliwatwanga m23 vilivyo lakini ukatolewa waraka toka UN kuyataka majeshi yanayounda FIB( jwtz, sandf na malawi) yaondoe baadhi ya silaha uwanja wa vita ikiwemo mizinga na mifumo yoyote ya maroketi ( isipokuwa RPGs).

Its neither today nor tomorrow, this will stir to generations.

Sorry for women and children of Nord kivu ( North Kivu) 😭😭
Na kuna baadhi ya vitu vilizuiliwa kuwekwa wazi kabisa peace keeping kweli ya kuisikia kuna mahali ilipigwa mizinga kwa mtindo wa triangle ilikuwa ni kwenda ku sweep tu ila wale jamaa walionyeshwa battle ipoje na Mzee.
 
wapi Tanzania iliwahi kuwa na wanajeshi hata 5,000 kwa wakati mmoja wakipigana sio kulinda amani,
Uganda, na walikufa zaidi ya hiyo elfu 5!!
Kwahiyo mkuu unatetea hao wazungu kina Exxon Mobil kisa Zimbabwe? Hiyo ni whataboutism
"kwanini umeiba?" === "mbona na fulani kaiba"
Hapana nashangaa double standards, yaani wazungu wakisaidia kupambana na waasi kama UNITA kule Angola au ISIS kule west Africa wakipewa mikataba ya kuchimba madini na mafuta tunasema wanaibia waafrika. Ila kwa Hawa Zimbabwe na Angola ambao walijichukulia tani za dhahabu tunasema ni halali sababu wanarudisha gharama za vita?? Why the double standards wakati ni Yale Yale tu.
Tanzania ilikuwa na mission nyepesi pale Seychelles kwanza visiwa vidogo wakati DRC kubwa zaidi ya mara mbili ya Zimbabwe.
Zimbabwe Ukiachana na operation kitona je walikua na mission Gani ngumu. Nachojua waliweka tu ulinzi Ili Rwanda asivamie Western Congo na maeneo ya dhahabu kama Katanga. Na vita ilipiganwa zaidi hapo Pweto na walipotoshana nguvu basi Kagame hakusogea.

Zaidi ya hapo Rwanda alibaki tu Kivu, Maniema, Ituri, Equater basi hawakufanya counter offensive yoyote Kuelekea Kinshasa au Bas Congo. So walikua more of peace keepers hao Zimbabwe, je Ina justify kubeba migodi.

Nakumbuka Rwanda walipomsaidia Kabila walijimilikisha migodi Ili kufidia gharama za vita. Sasa Zimbabwe wanakuja kupinga Hilo suala kwa kufanya Yale Yale alafu unasemaje ni liberators?
 
Kagame hajawahi fundishwa na Tanzania, labda tuseme Uganda kipindi ana RPF na Zimbabwe kipindi anaanza kuwa na jeshi la kisasa alipochukua nchi.
Amewahi soma briefly pale Monduli. Hii ilikua documented kwenye kitabu Cha Philip Rentyjens kuhusu ushawishi wa Nyerere kwenye vita ya DRC. Hivi unajua hata Wamba Dia Wamba alikua akiongoza vita ya Pili ya Congo kutokea Dar??
 
Uganda, na walikufa zaidi ya hiyo elfu 5!!

Hapana nashangaa double standards, yaani wazungu wakisaidia kupambana na waasi kama UNITA kule Angola au ISIS kule west Africa wakipewa mikataba ya kuchimba madini na mafuta tunasema wanaibia waafrika. Ila kwa Hawa Zimbabwe na Angola ambao walijichukulia tani za dhahabu tunasema ni halali sababu wanarudisha gharama za vita?? Why the double standards wakati ni Yale Yale tu.

Zimbabwe Ukiachana na operation kitona je walikua na mission Gani ngumu. Nachojua waliweka tu ulinzi Ili Rwanda asivamie Western Congo na maeneo ya dhahabu kama Katanga. Na vita ilipiganwa zaidi hapo Pweto na walipotoshana nguvu basi Kagame hakusogea.

Zaidi ya hapo Rwanda alibaki tu Kivu, Maniema, Ituri, Equater basi hawakufanya counter offensive yoyote Kuelekea Kinshasa au Bas Congo. So walikua more of peace keepers hao Zimbabwe, je Ina justify kubeba migodi.

Nakumbuka Rwanda walipomsaidia Kabila walijimilikisha migodi Ili kufidia gharama za vita. Sasa Zimbabwe wanakuja kupinga Hilo suala kwa kufanya Yale Yale alafu unasemaje ni liberators?
Uganda ilikuwa ni vita, hapo Tanzania ilikuwa imevamiwa. Sitaki kuamini kama unatumia akili yako kulinganisha situation ya vita ya Uganda ambayo JWTZ ilikuwa inawajibika direct 100% dhidi ya situation ya operation ya Zimbabwe ndani ya DRC ambapo jeshi la Zimbabwe halilazimiki kufia hapo.

Tanzania hata wangekufa wanajeshi milioni moja pale Uganda, ni vita yetu. Zimbabwe wametoka kwao kuvuka Zambia kuingia Congo kupigania nchi nyingine.

Zimbabwe hiyo operation Kitona unaona ni ndogo sio, na unajua mission objectives zao wakati wanaenda Congo na funding ya hiyo operation. Hawakuwa peacekeepers acha kudanganya, peacekeepers wanakuja na ground attack aircrafts? Peacekeepers wanakomboa mji mkuu na chanzo kikuu cha umeme?

Hakuna justification ya Zimbabwe kubeba madini ila yalikuwa ni makubaliano baina ya DRC na Zimbabwe. Kwa bajeti gani Zimbabwe ingeweza endesha ile expensive operation miaka kadhaa vile vikwazo vya kiuchumi?

Unatafuta kuhararisha wizi na unyonyaji hapo Congo kwa kujificha nyuma ya "mbona Zimbabwe waliiba"
 
Zimbabwe na Angola walinufaika mno na vile vita, na ndio ilikuwa njia ya serikali ya Kabila kugharamia Vita.....hata wavamizi pia (Rwanda na Uganda) waliiba mali za Drc.

Kwa Zimbabwe ilikuwa Vita ya kujitakia tu (japo waliingia kwa mwavuli wa Sadc) na ilikuwa njia ya wao kutumia mali za Drc kukwepa makali ya vikwazo hivyo askari wa Zimbabwe na maafisa wao walitajarika huko.....kwa Angola waliona Kabila akiondoka huenda watawala wapya wakatoa hifadhi kwa UNITA (japo nao pia waliingia kwa mwavuli wa Sadc na walinufaika mno na mali za huko.

Ule ulikuwa ni msaada kwa Drc, ila gharama Drc walilipia wenyewe....au tuseme waliununua.

zitto junior mtu chake
 
nakubaliana na wewe
 
Back
Top Bottom