Headmaster Ifunda Tech. alinusurika kifo kutoka kwa wanafunzi

Headmaster Ifunda Tech. alinusurika kifo kutoka kwa wanafunzi

ndiwela

Member
Joined
Jul 19, 2012
Posts
25
Reaction score
4
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, jana walifanya vurugu kubwa shuleni hapo na kutaka kumuua Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shaaban Nsute.

Katika vurugu hizo ambazo zilianza juzi jioni hadi saa tano usiku, wanafunzi hao ambao walivalia kininja na kuficha sura zao wakiwa na visu mkononi, walivunja vioo vya madirisha shuleni hapo.

Wanafunzi hao wanadaiwa kumfuata Bw. Nsute nyumbani kwake lakini alikimbia na kwenda kujificha kwenye shamba la mahindi ambapo wanafunzi hao walimpiga mlinzi wa shule Bw. Yasini Luhala kwa mawe akiwa katika ofisi yake.

Akizungumza na Majira jana, Bw. Nsute alisema chanzo cha vurugu hizo ambazo zilidhibitiwa na Jeshi la Polisi ni baada ya mwanafunzi mmoja shuleni hapo kuvaa kofia zinazotumiwa na Waislamu (baraghashia).

Alisema mlinzi wa shule hiyo, Bw. Luhala alimnyang'anya kofia hiyo ili asiingie nayo darasani kwa sababu si sare ya shule lakini mwanafunzi huyo alichukua uamuzi wa kwenda kuwaita wenzake na kufanya vurugu.

Aliongeza kuwa, kutokana na vurugu hizo zaidi ya wanafunzi 30 wamefukuzwa shule na kuwataja baadhi yao kuwa ni Sadi Mwamed, Jamal Hashim na Athuman Ibrahim wanosoma kidato cha tano. Wengine ni Abdulazizi Hussein na Ally Abdallah wanaosoma kidato cha nne.

"Mwanafunzi aliyenyang'anywa kofia alidai Waislamu katika shule hii wanatengwa, kunyanyaswa na kuzuiwa wasifanye mambo yanayoendana na dini yao.

"Hawa wanafunzi walikuja nyumbani kwangu usiku na kugonga mlango, nilitoka mlango wa nyuma nikakimbia kwenye shamba
la mahindi, mke wangu alifungua mlango na kuwaambia sipo na alipowahoji wakamwambia walikuwa wakinihitaji ili niende nao Msikitini kuna kazi muhimu," alisema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt Letisia Warioba, alisema tukio hilo limemsikitisha sana.

Alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufika mapema eneo la tukio, kutuliza vurugu na kuimarisha ulinzi shuleni hapo hadi asubuhi na kuwataka wanafunzi waliobaki, waendelee na masko kwa kuzingatia taratibu za shule.

Source: Gazeti la Majira la J3 tar 4/3/2013
 
Poleni sana! Chonde chonde 'Wanafunzi taratibu jamani'. Mimi ni Ifunda alumnae (1982) naifahamu shule vizuri, bado namkumbuka Headmaster Philip alivopata shida.
 
Izi dini zinakoelekea zitafanya mambo mabaya ata zaidi ya haya binafsi naona Shule ziendelee ktk misingi ya shule na dini ibaki ktk misingi ya Dini. Dini yako isiwe ndio kitu cha kuhalalisha uvunjifu wa amani
 
ndio zitakosekana zero hapo? na hawa wenzetu mambo mengine ni us....e...,bado mntaka damu ya mtu mwingine...
 
Mkwawa sekondari tulikuwa tunakatazwa hata kuvaa kofia za kawaida enzi za Headmaster Mbao na secondmaster Tende na hatukubisha,ila hawa wa sikuhizi balaa tupu wakifeli kosa la mama Ndalichako.
 
Kuna shule za kikristo na kiislamu!!! Aonaye anahitaji sana ku-practice dini yake aende kwenye mojawapo ya shule hizo....aliyefuata shule na abaki na kufuata shule!!
 
Mambo haya ya wanfunzi wa kiislam kufanya fujo yanajitokeza sana siku za karibuni! mfano Kibiti sec, huko Bagamoyo na sasa Ifunda!
Come on... hii sasa ni mbaya, serikali iangalie haya mambo kwa umakini.
 
Nadhani umefika wakati serikali itamke bayana kuwa katiba ya nchi inasemaje kuhusu dini. Katiba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inasmea kuwa serikali hiyo haina dini. Ina maana kwamba shughuli zote zinazohusu serikali hazifuati misingi ya dini yoyote ile. Hivyo basi itikadi, imani na viashiria vingine vya kidini kama mavazi, alama n.k visihusishwe kwenye shughuli zake. Kwa mantiki hiyo basi, ina maana kwamba katika shule zote ambazo ni za serikali, katiba ya Jamhuri ifuatwe. Kama wanafunzai wanavaa sare, ziwe ni sare ambazo hazihusishi dini. Kama kutakuwepo na jamii fulani ambayo inakerwa na jambo hilo, wako huru kabisa kuanzisha shule zao ambazo itikadi za jamii hiyo zitazingatiwa, ili mradi hawavunji sheria.
 
Tatizo la ni malezi, hawa watoto wamepandikizwa roho za kuwa wanaonewa tangu wakiwa kwenye shule za watoto (madrasa) hivyo kubadili ama kuondoa hiki kizazi cha namna hii wabadilishe mfumo wa mafundisho yao kwa watoto wa madrasa. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, sio kosa lao ni kosa la mfumo wa malezi ya dini yao (Islamic).

Mlee mtoto katika njia ipasayo naye akikua hata mzee hataiicha daima.

Hapa kazi ipo
 
Ugaidi mbona wameuanza wakiwa watoto waadogo sana?
Eti hawa nao ni taifa la kesho. Kesho tutakuwa na taifa la ajabu sana
 
CCM kuikumbatia BAKWATA kutawatokea puani!NI BOMU HILO,bakwata kwa sasa haina control na kundi kubwa la waislam!kiundwe chombo kingine kitakachokua na sauti kwa waislam
 
Kitu ambacho wangetakiwa kukifaamu ni kua shuleni sio sehemu ya querrelling kuu issiues za dini.
 
Unajua!? siku hizi watumishi wa ibilisi shetani wanajifanya ni wanadini. Watumishi wa Yehova yaani walokole hawavunji sheria.
 
hapo wtaandamana tena kupinga wenzao kufukuzwa
 
Kwa kweli kabisa na kwa kumwogopa Mungu huyu anayefanya nipumue sasa hivi,kuna katabia kana nikera sana.
Utaona tatizo limefanywa kabisaaaaa na mtu wa imani moja na liko wazi kabisa lakini mtu anachangia eti Dini hizi! Zipi? wakati iliyofanya hivyo inajulikana? Tuache nidhamu ya woga na kubebana,kwa utaratibu huu wa kuogopana kuelezana ukweli ndio utatufikisha pabayaaaaa ndugu zangu. Wanafunzi wa kiislam wamefanya vurugu shuleni eti tu kwa nini wanakatazwa kuvaa kofia za namna ya imani yao. Halafu unasema dini hizi,si useme tu WAISLAM HAWA? Kwa nini wakristo na imani nyingine waingizwe hapo wakati hawahusiki? Ndugu zetu ukweli unauma lakini ni bora usemwe ili pengine tupone "Ndugu zetu waislam(SI WOTE) mtaiingiza nchi pabaya. Naamini hata yale ya Zanzibar kuuawa kwa Padre,laiti aliye uawa angekuwa Maalim au Shekhe basi nchi ingekuwa taabu kwelikweli. Acheni amani hii ilindwe wapendwa,mnapokutana onyaneni,na kusemezana ili tukae kwa amani wapendwa. Hebu jiulize umeua eti uislam uendelee, haya umeendelea,Halafu?
 
Wamechoka kusoma tu hao! Kama wanapenda kuvaa hizo kofia wakati wa masomo si waende seminary zao!?
Kama wanaijua dini yao vizuri, kofia kwa mwanaume sio kitu cha muhimu sana, nadhani wanaiita suna, yaani kuivaa au kutoivaa sio dhambi!
 
Wengi hawaijui imani yao vizuri na wamekuwa wakifuata mkumbo tu. Ukitaka kuprove muulize muislam wa karibu yako asili ya uislam i mean, UISLAM ULIANZAJE? Kama hatakukasirikia basi atakwambia sijui ngoja nkaulize. Hapo ndio asili ya tatizo wengi ni mamluki. Wanachojua wao ni KAFIRI tu bila kujua hata maana ya hilo neno. Maana yake ni "MPINGAJI" kwa kuwa neno kafiri ni neno la Kiarabu. Sasa ukija kwenye uhalisia mpingaji ni nani? Ukristo ulikuwepo na miaka 400-500 baadae ukaja uislam. 0+0 = 00
 
"Mwanafunzi aliyenyang'anywa kofia alidai Waislamu katika
shule hii wanatengwa, kunyanyaswa na kuzuiwa wasifanye
mambo yanayoendana na dini yao.
halafu utakuta mijiwanafunzi ya hivi ni vilaza wa kutupwa.
 
Tatizo la ni malezi, hawa watoto wamepandikizwa roho za kuwa wanaonewa tangu wakiwa kwenye shule za watoto (madrasa) hivyo kubadili ama kuondoa hiki kizazi cha namna hii wabadilishe mfumo wa mafundisho yao kwa watoto wa madrasa. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, sio kosa lao ni kosa la mfumo wa malezi ya dini yao (Islamic).

Mlee mtoto katika njia ipasayo naye akikua hata mzee hataiicha daima.

Hapa kazi ipo

Ukijadili ukweli ulivyo hapa JF utaitwa mdini. Ndio maana kila mtu anakwepa kusema asili ya vurugu mashuleni siku za hivi karibuni na kubaki kusema, hizi dini, hizi dini... utadhani wanafunzi wa imani ya Budha ama Zoroastrian nao wamehusika. Kwa mwendo huu suluhu iko mbali. CALL A SPADE SPADE, NOT A BIG SPOON!
 
Back
Top Bottom