Heaven on earth avamiwa na kujeruhiwa vibaya

Heaven on earth avamiwa na kujeruhiwa vibaya

Wajamaaee! Nchi hii amani imetoweka... Vibaka full swing kila kona?
Pole Mkuu Miss Heavan on Earth, Mwenyezi Mungu akuafu na awe na wewe 24/7 ..poleni jamiiforums
Mtihani huu upite bila madhara na Madhilaa kwetu sote....!
 
sio kila alie humu ni mwema...pengine mleta thread ana maana nzuri ya kiusalama
Wewe mleta uzi,
unatueleza kuhusu zahama iliyompata H.O.E harafu hutaki watu wajue
hospitali alipolazwa ili wakamjulie hali, wewe unataka wafanyaje? kama
unaona wanajf hawaaminiki si ni afadhari usingesema tu.
unakuta mtu mpo nae hospitali ila mnashindwa kujuliana hali, eti kwa
sababu tu ya kuendeleza utamaduni wa kutofahamiana miongoni mwetu!
Pole sana my da H.O.E
 
Dah habari za kusikitisha sana,Mungu amponye huko aliko.Jana tu tulikua naye kwenye thread flani kumbe kapatwa na majanga jioni.
 
Ndugu Jamaa na Marafiki.

Nasikitika kutoa taarifa juu ya madhira aliyokutana nayo dada na ndugu yetu HEAVEN ON EARTH jana usiku.
Akiwa anaelekea nyumbani kwake jana usiku alivamiwa na vibaka/majambazi na kumjeruhi vibaya sana.

Toka alipopatwa na madhira hayo mpaka mchana huu bado hawajeza kuongea, naomba tushirikiane kumuombea ili matibabu anayopata yaweze kumrejeshea nguvu na afya yake.

Nitakapopata taarifa za ziada nitawajuza.

UPDATE
Hatimaye amefanikiwa kuongea mchana huu, inatia matumaini kwamba afya yake inahimarika kwa upesi.

mpe pole sana .
 
Back
Top Bottom