Hebu jionee waalim vyuo vikuu wanavyolalamika

G. Activist

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
482
Reaction score
125
Wana bodiHii imekutwa kwenye baadhi ya email ambazo huwa zinakuwa circulated kwa waalimu wote wa UDSM wakijadili maada fulani.

Hivi ni wapi kunaunafuu, sisi wanafunzi hapa UDSM ndio kabisa tunaogopa kupaza sauti zetu, je na hawa walimu wetu wanaogopa pia kupaza sauti zao!!

Kiutaratibu wanasiasa hawakupaswa kulipwa mshahara kama wabunge au mawaziribadala yake zingelipiwa taaluma zao. Hivi mtu kama professor maji marefu au Jahpeople analipwaje milioni kumi na marupurupu juu wakati professor aliyesota kusomana kupublish for years analipwa milioni tatu na bado mazingira ya kazi yanambana?Hivi kazi ya mbunge au waziri ni ipi hadi astahili malipo makubwa kiasi hicho? Hataofisini hawaonekani, wakienda field wana allowance, hizi milioni kumi mshahara nikwa ajili ya nini? Huku ukimuacha TA, AL, Lecture na professor wa chuo kikuuanahangaika kupiga lecture hadi saa mbili za usiku na akitumia vi-cube kama ofisi? Inashangaza sana kwamba mtu anafanya kazi Univeristy lakini hata kiti cha kukaliaofisini hakuna.

Ukifika asubuhi ukakuta ofisini kwako kumejaa unaanza kupitakuchungulia ofisi nyingine kuona ni nani hayupo ili upate pa kukaa. Ofisi ya watuwatatu inatumiwa na watu 20? Hata computer moja hakuna. Lakini kila kukichaunapangiwa deadlines za kumaliza kazi. Hizo kazi tunafanyia wapi? Hata mkopo wakununua laptop tu hatukuwahi kupewa. Na hapo hapo kila mwaka unalazimishwa upublish.Na huna incentives wala benefits zozote unazozipata kutokana na kazi zako zaidi yamshahara. Na bado serikali inabana fursa za watu kujiongezea kipato halali, kwakuchelewa promotion na nyongeza za mishahara. Arrears za tangu mwakajana hatujapatahadi leo. Wengine tangu wapandishwe madaraja hawakuwahi kubadilishiwa mishahara.Nafikiri UDASA waangalie ni namna gani hatua zichukuliwe dhidi ya uonevu huu.
 
Wee nawe mambo ya mijadala ya ndani ya watu unailetaje huku? Halafu wewe unakuwaje mwanafunzi halafu unaweza kuaccess email za wanaUDASA? hebu futa post yako hapa mambo ya walimu wa chuo yanawahusu nini JF? Hapa unataka tujadili kitu gani?
 
Hehehe, hii sekta ya ualimu ni kama ina laana kwa hapa Tanzania. Ni dhahiri kua zinahitajika fikra na mitazamo mipya juu ya huu mjadala
 
ni kweli ulicho sema kuwa mishahara ya wabunge na wanasiasa kwa ujumla ni mikubwa mno ukilinganisha na watumishi wengine.lakini hawa wanataaluma nao nina mashaka na uadilifu,elimu na utu wao kwa jinsi wanavyojenga hoja zao juu ya hili.mimi nawaona kama nao ni wasaka tonge tu kwa hiyo nao wanataka wanufaike kwa kiwango cha juu iwezekanavyo.wangekuwa waadilifu wangesema kwa nini mwanasiasa alipwe milioni kumi wakati mwalimu wa shule ya msingi analipwa chini ya laki mbili.
 
Kwenye hoja yao ya msingi sioni kama wanaomba kuongezwa mishahara badala yake wanasema mishahara ilipwe kutokana na taaluma ya mtu na si cheo. Kwa msingi huo ina maana hata huyo mwalimu wa secondary mwenye degree ya sayansi atalipwa mshahara sawasawa na mkurugenzi wa bandari au mbunge mwenye degree ya sayansi. Huoni kama pana hoja ya msingi hapo?
 
Mkuu, hata walimu wa s/msingi wanajipigania kivyao! rejea hoja walizotoa miezi michache iliyopita wakati wakijiandaa na mgomo ambao hata hivyo haukuwa na mafanikia zaidi ya serikali dhalimu (narudia tena dhalimu) ya Tz kuwanyamazisha kupitia mahakama!

Mwl chuo kikuu hakatazwi kutetea hoja ya kutaka maslahi zaidi mf. mshahara mzuri, vitendea kazi, malipo kwa kazi za ziada n.k eti kisa mwl wa s/msingi analipwa laki 2!! Pia kumbuka hata kiwango cha elimu cha mwl wa s/msingi ni kidogo SANA kulinganisha na Lecturer (au Proffesor)!!

Swali; Je unaweza kuniambia Mbunge anayejikusanyia karibia Tsh. 10 m kila mwezi ana vigezo gani ambavo Mwl wa chuo kikuu hana au hawezi kuwa navyo?!
 
kwani huyo professor amesoma kwa pesa zake toka mfukoni? pesa za serikali ndo zimemsomesha..after enjoying benefits u must incur costs...waache tu walipwe m3 hzo..after all mwalim ni mwalim tu na ualim ni wito..abt politicians nchi almost zote duniani politicians wanachukua pesa ndefu..
 
hizi kauli za kijinga huwa nazichukia sana. Kwani kina magembe wamejisomesha.? Wengi wao si walikuwa walimu wakakimbilia kwenye siasa.? Kwani kusomeshwa ndo ulipwe kidogo? Nani kakuroga?
 
kwani huyo professor amesoma kwa pesa zake toka mfukoni? pesa za serikali ndo zimemsomesha..after enjoying benefits u must incur costs...waache tu walipwe m3 hzo..after all mwalim ni mwalim tu na ualim ni wito..abt politicians nchi almost zote duniani politicians wanachukua pesa ndefu..

umejitahidi kufikiri eeh?
 
Nchi hii ukishaitwa "mwalimu" ujue umekwisha. Uwe wa chekechea, praimari, sekondari, chuo kikuu.. wote ni tabu tupu!
 
Dawa ni kuwa wajasiria mali na kuachana na Ualimu afu hao wabunge wakafundishe.Ukitegemea mshahara hautaisha kulalamikia mishahara. jumlishia na kaufisadi kidogo walahi utajikuta huendi benki kukwangua salio.Poleni sana Waalilimu (ualimu)
 
kwani huyo professor amesoma kwa pesa zake toka mfukoni? pesa za serikali ndo zimemsomesha..after enjoying benefits u must incur costs...waache tu walipwe m3 hzo..after all mwalim ni mwalim tu na ualim ni wito..abt politicians nchi almost zote duniani politicians wanachukua pesa ndefu..
Hivi serikali ya Tanzania inatoa scholarship, za masters na PhD? Madokta na Maprofessor wengi ninaowafahamu wamelipia masters zao kwa hela yao ya mfukoni na hizo PhD zao zimelipiwa na mashirika au serikali za nje?

Kama ni bachelor, kila mtu kasomeshwa na serikali, hao mawaziri bachelor zao walisomeshwa na nani? Na kwanini wao walipwe mshahara mkubwa na marupurupu kibao kuliko wengine?

Inaelekea wewe upo katika kundi la wanasiasa wanaoneemeka na hii unequal distribution of resources iliyopo hapa nchini.
 
sasa kama hawa wanalalamika hali ngum,na sisi wa huku st kayumba inakuaje?? mh....yan 3mil mtu unalalamika??? na sisi wa laki2 itakuaje??
 
Kwenye hoja yao ya msingi sioni kama wanaomba kuongezwa mishahara badala yake wanasema mishahara ilipwe kutokana na taaluma ya mtu na si cheo. Kwa msingi huo ina maana hata huyo mwalimu wa secondary mwenye degree ya sayansi atalipwa mshahara sawasawa na mkurugenzi wa bandari au mbunge mwenye degree ya sayansi. Huoni kama pana hoja ya msingi hapo?
kwa tz yetu haiwezekan narudia tena haito wezekana.....ni ngumu!!!
 
kwani huyo professor amesoma kwa pesa zake toka mfukoni? pesa za serikali ndo zimemsomesha..after enjoying benefits u must incur costs...waache tu walipwe m3 hzo..after all mwalim ni mwalim tu na ualim ni wito..abt politicians nchi almost zote duniani politicians wanachukua pesa ndefu..
unajua maana ya mkopo ni nin?? unasema amesomeshwa,kwani halipi??
 
kwani huyo professor amesoma kwa pesa zake toka mfukoni? pesa za serikali ndo zimemsomesha..after enjoying benefits u must incur costs...waache tu walipwe m3 hzo..after all mwalim ni mwalim tu na ualim ni wito..abt politicians nchi almost zote duniani politicians wanachukua pesa ndefu..

Si kweli!!!!!!
 
Wana bodiHii imekutwa kwenye baadhi ya email ambazo huwa zinakuwa circulated kwa waalimu wote wa UDSM wakijadili maada fulani.

Hivi ni wapi kunaunafuu, sisi wanafunzi hapa UDSM ndio kabisa tunaogopa kupaza sauti zetu, je na hawa walimu wetu wanaogopa pia kupaza sauti zao!!

Kiutaratibu wanasiasa hawakupaswa kulipwa mshahara kama wabunge au mawaziribadala yake zingelipiwa taaluma zao. Hivi mtu kama professor maji marefu au Jahpeople analipwaje milioni kumi na marupurupu juu wakati professor aliyesota kusomana kupublish for years analipwa milioni tatu na bado mazingira ya kazi yanambana?Hivi kazi ya mbunge au waziri ni ipi hadi astahili malipo makubwa kiasi hicho? Hataofisini hawaonekani, wakienda field wana allowance, hizi milioni kumi mshahara nikwa ajili ya nini? Huku ukimuacha TA, AL, Lecture na professor wa chuo kikuuanahangaika kupiga lecture hadi saa mbili za usiku na akitumia vi-cube kama ofisi? Inashangaza sana kwamba mtu anafanya kazi Univeristy lakini hata kiti cha kukaliaofisini hakuna.

Ukifika asubuhi ukakuta ofisini kwako kumejaa unaanza kupitakuchungulia ofisi nyingine kuona ni nani hayupo ili upate pa kukaa. Ofisi ya watuwatatu inatumiwa na watu 20? Hata computer moja hakuna. Lakini kila kukichaunapangiwa deadlines za kumaliza kazi. Hizo kazi tunafanyia wapi? Hata mkopo wakununua laptop tu hatukuwahi kupewa. Na hapo hapo kila mwaka unalazimishwa upublish.Na huna incentives wala benefits zozote unazozipata kutokana na kazi zako zaidi yamshahara. Na bado serikali inabana fursa za watu kujiongezea kipato halali, kwakuchelewa promotion na nyongeza za mishahara. Arrears za tangu mwakajana hatujapatahadi leo. Wengine tangu wapandishwe madaraja hawakuwahi kubadilishiwa mishahara.Nafikiri UDASA waangalie ni namna gani hatua zichukuliwe dhidi ya uonevu huu.

Si muache kazi na mtafute ajira ndani na nje ya nchi wanakolipa poa. Mnang'ang'ania nini hapo?
 
kwa tz yetu haiwezekan narudia tena haito wezekana.....ni ngumu!!!
Yah, you might be right, kwa sababu wapanga mishahara ni hao hao wanasiasa. Sasa jah people atakubali alipwe mshahara wa darasa la pili kweli?
 
Du!Home of intellectuals vipi hapo kwenye ukosefu wa vitendea kazi, ofisi na mishahara na marupurupo kidogo,hivi dhambi ya kuwa chuo cha kata haiwezi kuhusika kweli?
 
Back
Top Bottom