Hebu leo wakumbuke wahadhiri wa vyuo vikuu waliokufurahisha kwa jinsi ya umahiri wao wakufundisha na walivyokuwa 'fair'

Hebu leo wakumbuke wahadhiri wa vyuo vikuu waliokufurahisha kwa jinsi ya umahiri wao wakufundisha na walivyokuwa 'fair'

Dr. Adolf Mihanjo,
Dr. Benson Bana,
Prof. G. Mutahaba,
Prof. R. Mukandara
Sr. Maria Kente
Prof. Suleiman Ngwale
Dr. Ngw'aza Kamata
Hawa watu walikuwa safi sana pale UDSM
 
Prof. Haidari Amani
Huyu amenifundisha Consumer Behavior mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Dar es Salaam ktk Introductory Microeconomic Analysis EC 116. Alikuwa fundi sana na alinifanya niupende sana uchumi. Hii course walikuwa wanafundisha na aliyekuwa naibu gavana benki kuu Dr. Natu Mwamba pamoja aliyekuwa msajili wa hazina Dr. Oswald Mashindano, hawa walikuwa wabovu wote. 😃​

Prof. Delphin Gayata Rwegasira
Mtaalamu huyu na mhitimu wa chuo kikuu cha Harvard (A.M, PhD Economics, 1971-1976) amenifundisha Monetary Economics EC 371 na Policy Analysis EC 664, Alikuwa anafundisha kwa hisia sana na ana ujuzi mkubwa sana wa sera za fedha, pia alikuwa msimamizi wa andiko langu kipindi namaliza chuo.​

Hawa kwa sasa wote wamestaafu ila ni waalimu niliowapenda sana walikuwa very smart kichwani, mmoja ni jirani yangu huwa tunakutana mara moja moja kupiga story.
 
Ha ha nimeshangaa kuwataja hao jamaa hao jamaa hawafai hata kidogo na Ossoro jr naye hakuna kitu anachofundisha hakieleweki kutishana tu kwa kifupi EC 116 na 126 hazina lecturer walio fair ila EC 117 na 127 wako poa sana
Dr. Karamagi mwalimu bora sana wa Ec 126(intermidiate Micro Economics) anajua hadi anakera

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DR SIASA ISSA MZENZI WA UDSM MZEE BABA AKIKUFUNDISHA AC 100 NA AC 101 FIRST YEAR KULE B.COM YANI HAPA MZEE BABA NDIO UTAJUA NINI MAANA YA MAKABATI YA ACCOUNTS YANI MIE NIMESOMA HGL MPAKA NAMALIZA BCOM 2012 SIKUWAHI KU BALANCE BALANCE SHEET STATEMENT HATA MOJA MPAKA NAMALIZA HADI MASTERS.ILA NIKAJA NIKAGUNDUA KUWA MARKS ZA KWENYE MITIHANI YA ACCOUNTS HUWA ZINAPATIKANA KWENYE ZILE CORRECT ENTRIES.
Naam Dr Siasa Issa Mzenzi sheikh yupo fair sana.

Mwalimu bora sana wa Accounts

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo umewataja walimu bora sana wa uchumi

Huyu Prof Rwegasira akikufundisha monetary economics aisee hata pen ikianguka huokoti ili usipoteze cocentration.

Miongoni mwa Prof wangu Bora wa wakati wote.
Prof. Haidari Amani
Huyu amenifundisha Consumer Behavior mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Dar es Salaam ktk Introductory Microeconomic Analysis EC 116. Alikuwa fundi sana na alinifanya niupende sana uchumi. Hii course walikuwa wanafundisha na aliyekuwa naibu gavana benki kuu Dr. Natu Mwamba pamoja aliyekuwa msajili wa hazina Dr. Oswald Mashindano, hawa walikuwa wabovu wote. [emoji2]​

Prof. Delphin Gayata Rwegasira
Mtaalamu huyu na mhitimu wa chuo kikuu cha Harvard (A.M, PhD Economics, 1971-1976) amenifundisha Monetary Economics EC 371 na Policy Analysis EC 664, Alikuwa anafundisha kwa hisia sana na ana ujuzi mkubwa sana wa sera za fedha, pia alikuwa msimamizi wa andiko langu kipindi namaliza chuo.​

Hawa kwa sasa wote wamestaafu ila ni waalimu niliowapenda sana walikuwa very smart kichwani, mmoja ni jirani yangu huwa tunakutana mara moja moja kupiga story.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof. A. Pereka, Prof. Remmy Assey, Prof. Gabriel Mbassa mabingwa wa animal physiology, gross anatomy na myology pale school of veterinary medicine
 
Back
Top Bottom