Namkumbuka mhadhiri mmoja aliyetumia baadhi ya wanafunzi kumpiga majungu mkuu wa kitivo ili yeye apate hiyo nafasi, alikuja kufanikiwa na hao aliowatumia wakawa watu wake watiifu na walioneemeka kwa kupata maksi za bure . Ingawa alikuja kuondolewa kwenye nafasi yake lakini aliharibu mno kitivo kwa kuwa anagawa maksi kwa watu waliokuwa watiifu kwake, yaani ukijipendekeza tu unakula GPA nzuri. Huyo jamaa ni kati ya watu wa hovyo ( Mungu nisamehe kwa hili) mno niliowahi kutana nao katika historia yangu ya elimu.