Hebu taja hapa zile furaha ndogo ndogo ambazo hazitoshi kumwambia mtu ila huwa unajisikia raha

Haha wewe unadai "muacheni nimfunze adabu huyo kima" kumbe kimoyomoyo unasema mtoeni asije kuniua bure.
 
Uko safarini ukajichanganya ukala hovyo tumbo likaanza kuuma unafeel kushusha mzigo mara unasikia konda akisema ni time ya kuchimba dawa....wewe mwenyewe wajua furaha inayopamba moyo wako huku ukiwahi kushuka.
 

4. Umebetia Ada ya shule mchezo wa kikapu odds 2 kama ikipatikana over 58.5 Quater ya 4. Mchezo unachangamka sana unasubiria ile laki 7 iwe 1.4M kwa hamu.

Unatulia hadi dakika 47:31 vikapu viko 56 tu..halafu kimya kimetawala unaanza kuhisi tumbo la kuhara, kichwa kugonga, njaa, huzuni, majuto mpaka inafikia dakika ya 47:56!

Ghafla unashanga timu moja imepata free throws ikatumbukiza vikapu vitatu!!!

Ubao unasoma 48:00 gone, vikapu 49, mara kile kineno kifupi cha rangi ya kijani "WON" kinajitokeza chini ya mkeka pale kikisindikizwa na tarakimu za salio la 1.4M! Aisee asikwambie mtu hio furaha yake haielezeki!
 
Share nasi ndugu.. maana Kuna watu wakitokaga kwenye situation kama hizo huwa wanalia!,sio kwamba analia kwa kipigo no analia machozi ya furaha kwa kuokolewa..πŸ˜‚πŸ˜œ

Hebu leta hako kaushuhuda..
Bro haka kaushuhuda sikaleti ng’o🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…