Hebu taja hapa zile furaha ndogo ndogo ambazo hazitoshi kumwambia mtu ila huwa unajisikia raha

Hebu taja hapa zile furaha ndogo ndogo ambazo hazitoshi kumwambia mtu ila huwa unajisikia raha

Usiombe ukawa unapigana halafu kipigo kikawa kimelalia kwako then watu badala waamue ndo unasikia Kobe fulani huko inasema "Waacheni wafundishane adabu"[emoji23]
Sasa unajiuliza tufundishane adabu wakati ukijiangalia wewe jicho limeshaumuliwa halafu adui yako ndo kwanza anatoka jasho tu na kakutia kabari inaitwa "bwana wa mabwana Alfa na Omega"[emoji23]

Bahati nzuri situation kama hizo ndo wanatokeaga na wasalamia wema hapo ndo unajua kumbe malaika bado wapo duniani.. kwa ubavu nawe unajidai kuparangana ili kuuwa soo..[emoji12]
Haha wewe unadai "muacheni nimfunze adabu huyo kima" kumbe kimoyomoyo unasema mtoeni asije kuniua bure.
 
Uko safarini ukajichanganya ukala hovyo tumbo likaanza kuuma unafeel kushusha mzigo mara unasikia konda akisema ni time ya kuchimba dawa....wewe mwenyewe wajua furaha inayopamba moyo wako huku ukiwahi kushuka.
 
Wajumbe, ni Kazi Tu au Kazi na Bata!

Haya maisha bhana fanya yote ila hakikisha unafurahia, viwango vya furaha vinatofautiana kutoka ndogo hadi zile kubwa ambazo hadi watu wengine watajionea.

Basi kwa kutambua tofauti hizo, sio vizuri kuipuuza furaha ndogo kwa kutarajia kubwa isiyo na uhakika. Unaweza kungoja milele, na hivyo utaishi bila furaha kwa sababu tu ya tamaa na mapuuza.

Nitaanza kwa mifano michache, kisha nawe utashea za kwako:

1. Umekwangua vocha ukafuta namba kadhaa, ila ukafanikiwa kubuni namba kitu ikasoma... ile feeling niaje! Enhee hiyo hiyo.

2. Ile muda umegombea daladala na ukabahatika kupata siti, unafeel aje! Tena unajikausha kama sio wewe, furahia.

3. Upo kwenye mdahalo halafu hujui kitu imeulizwa, unaona mwezeshaji ananyoosha mkono kukuelekea... ghafla jirani yako anainuka kujibu.

4. .......

5. ........

Tuendelee!

Miscellaneous happiness!!

4. Umebetia Ada ya shule mchezo wa kikapu odds 2 kama ikipatikana over 58.5 Quater ya 4. Mchezo unachangamka sana unasubiria ile laki 7 iwe 1.4M kwa hamu.

Unatulia hadi dakika 47:31 vikapu viko 56 tu..halafu kimya kimetawala unaanza kuhisi tumbo la kuhara, kichwa kugonga, njaa, huzuni, majuto mpaka inafikia dakika ya 47:56!

Ghafla unashanga timu moja imepata free throws ikatumbukiza vikapu vitatu!!!

Ubao unasoma 48:00 gone, vikapu 49, mara kile kineno kifupi cha rangi ya kijani "WON" kinajitokeza chini ya mkeka pale kikisindikizwa na tarakimu za salio la 1.4M! Aisee asikwambie mtu hio furaha yake haielezeki!
 
Back
Top Bottom