Hebu tiririka tabia mbaya za baadhi ya wafanyakazi kwenye maofisi

Hebu tiririka tabia mbaya za baadhi ya wafanyakazi kwenye maofisi

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (64)✍️
Kuna baadhi ya wafanyakazi kwenye maofisi wana tabia mbaya zinazowakera wenzao (watu wengine). Hebu tiririka tabia mbaya mojawapo - Natiririsha baadhi ya tabia mbaya.

🔘 TABIA MBAYA 1:
Kuna mfanyakazi ambaye kila kiongozi au bosi mpya atakayeripoti, ni lazima akajipendekeze kwa ajili ya maslahi yake binafsi. Huko haachi kueleza mabaya ya wenzake na kuficha mabaya yake.

🔘 TABIA MBAYA 2:
Kuna mfanyakazi ambaye akipewa kazi hamalizi, atafanya kazi kidogo kisha atahamia kwenye meza ya mwenzake ili kupiga stori. Kazi zake nyingi anasaidiwa na wenzake.

🔘 TABIA MBAYA 3:
Kuna mfanyakazi ambaye ana tabia ya kuwatega (kutongoza) wafanyakazi wenzake hasa wafanyakazi wapya (kupitia SMS/WhatSapp) kwa namba ngeni ambayo haikusajiliwa kwa majina yake. Deal lake likitiki anafanya kweli.

🔘 TABIA MBAYA 4:
Kuna mfanyakazi ambaye si kwamba ni mpole bali anajiona yeye ni bora kuliko wenzake, hivyo akiingia ofisini hataki kusalimia mpaka wenzake waanze kumsalimia yeye, na hupenda sana kujitenga.

🔘 TABIA MBAYA 5:
Kuna mfanyakazi ambaye tabia yake ni uchonganishi. Ni mchonganishi mzuri sana kati ya wafanyakazi kwa wafanyakazi, na wafanyakazi kwa kiongozi wao. Kama watu hawatamgundua au kuwa na msimamo, ofisi nzima watachukiana.

🔘 TABIA MBAYA 6:
Kuna mfanyakazi ambaye upinzani na ubishi ni jadi yake. Chochote kitakachopangwa au kujadiliwa ofisini au kupitia group la Whatsapp la kazini, ni lazima yeye atapinga bila sababu. Anatuma SMS ndefu za kupinga hoja au makubaliano ya wengi.

🔘 TABIA MBAYA 7:
Kuna mfanyakazi ambaye ana tabia ya umalaya wa wazi. Kila mfanyakazi mpya anayetambulishwa, yeye atamtaka kimapenzi kwa gharama yoyote.

🔘 TABIA MBAYA 8:
Kuna mfanyakazi ambaye hamalizi matatizo yake, kila siku ni mtu wa kuomba ruhusa ya kushughulikia matatizo yake. Leo akija na hili, baada ya siku kadhaa anakuja na lingine.

TIRIRIKA "TABIA MBAYA" NYINGINE
_____________
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
 
Hii namba 01 ipo sana hasa LOCAL GOVT...Mkurugenzi mpya akiripoti watu full kujipendekeza, ..UCHAWA!
 
Kuna ile tabia za wafanyakazi kuwa na masikhara yaliyopitiliza unaweza sema ni wandate kumbe wala kila mmoja ni mke na mume wa mtu ila kushikana shikana,wengine hadi kubebana na kubambiana kabisa inakuwa ni kawaida kabisa mh laiti kama wamiliki halali wangekuwa wanaona yanayoendelea maofisini cjui kama wangeeleweka
 
Hii ni mimi kabisa na Lizzy!
 
Ongezea hizi.
1.uchawi..ebana kuna watu wanajua waganga wote mashuhuri Tanzania hii.
2.Ombaomba..kuna mafala wao wanaomba hata mihogo ya kukaanga au chapati.
3.madeni..kuna watu wana madeni ambayo huwa hayaishi
 
Kuna work mate ni mmalila ila akiwa ndani ya ofisi anakuwa mnyakyusa ili tu boss wa kinyakyusa aendelee kumbeba, akiwa nje anarudi kwenye umalila wake, uchonganishi, kujipendekeza na uchawi ni dini za jamaa. Kuna mizimu ya kwenu ipo imara ukiajiriwa ofisini kwetu lazima utamuota anakufanyia kitu kibaya. Na kila aliyewahi fanya kazi nae ofisi nyengine hawataki kuwepo alipo jamaa.
 
Kuna ile tabia za wafanyakazi kuwa na masikhara yaliyopitiliza unaweza sema ni wandate kumbe wala kila mmoja ni mke na mume wa mtu ila kushikana shikana,wengine hadi kubebana na kubambiana kabisa inakuwa ni kawaida kabisa mh laiti kama wamiliki halali wangekuwa wanaona yanayoendelea maofisini cjui kama wangeeleweka
Hapa ndo hua nawahurumia walio olewa/kuoa watumishi wa
 
Hasa wadada Wanavaa nguo fupi na za ajabu huku weng wao wameoleka.
 
Back
Top Bottom