Hebu tuangalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais Magufuli Maabara kuu ya Taifa

Hebu tuangalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais Magufuli Maabara kuu ya Taifa

Mkuu tusichoshane bure hapa.

Umesema kipimo kinapima specimen maalumu, ikiwa tofauti maana yake haiwezi kuzitambua itakuwa Unknown.

Sasa sample za hayo mapapai vimeleta positive na negative

Ukasema imekuwa positive kwasababu labda sample iliyo letwa iko contaminated sawa hilo linawezekana ikiwa kama kuna uzembe ulifanyika.

Sasa je haya yaliyokuja negative nayo imekuawaje, mbona hicho kipimo hakikusema kuwa hiyo sample haitambuliki??
Hii negative nayo imekuwa contaminated na nini hadi jibu lije negative??
Ebana wewe ni mzito sana kuelewa!Mimi napingana na aina ya sampuli zilizopelekwa!Ilitakiwa zipelekwe sampuli ambazo zinatambulika na kifaa husika!Sasa kama kifaa hakijawa designed kutoa majibu ya haitambuliki unataka kitoe hivyo?Ni sawa wewe uweke mkojo au damu ya mbuzi kwenye kipimo cha kupimia HIV,chenye outcome mbili tu ambazo ni + au -,kikipuka jibu kati ya hayo mawili utalaumu kifaa au wewe ambaye umeweka mkojo?
Njia sahibi ni kuweka damu ya binadamu ambayo tayari unajua majibu yake,fanya hivyo kwa mara nyingi iwezekanavyo ili kubaini ubora wa kifaa!Sikubaliani na aina za sampuli zilizopelekwa!
 
3 Wengine wanasema kuwa mh anawadharau wataalam, hana shukurani,anadanganya umma, anataka kuficha wagonjwa n.k.

Hii hoja haina mashiko.

Inakuwaje madaktari na wataalam wabobezi kabisa kwenye utafiti na vipimo unaletewa sample ya papai na fenesi unaambia ni ya binadamu halafu unakubali na kwenda kuipima??

Hii inatoa picha kuwa wataalam wetu wanalipua lipua tu na hawako makini na kazi yao, kama wako makini hili linawezekanaje??
Sample inapoletwa maabala huwezi kujua ni ya nini kwa vile ni swab. Swab inatumiwa kuchukua sample wenye kitu chochote. Unaposiki kuwa virus wanaweza kuishi kwenye surface fulani kwa muda kadhaa in maana wamekenda kuchukua sample kutoka kwenye hiyo suface kwa kutumia means fulani ambayo kwa kawaida wanatumia swab. Kitu wanachofanya ni kuswab eneo ambalo wanafikiri liko contaminated na kupima. Sasa kama papai liko contaminated na ukaswab sehemu ambayo virus vipo papai litakutwa positive pia.
 
Mkuu hebu ngoja kwanza, hivi vifaa vilikuwepo hapa nchini kabla ya corona na vilikuwa vikitumika kwa matumizi mengine!!?? Ama sijakuelewa vizuri.
Ndiyo mkuu. Ukiondoa hizi Kits ambazo zimeingia majuzi PCR based techniques ziko siku nyingi tu nchini. Hizo Kits za Kichina hata za Mmarekani hazitambuliwi na WHO. Zipo kwa ajili ya screening tu.
 
Ebana wewe ni mzito sana kuelewa!Mimi napingana na aina ya sampuli zilizopelekwa!Ilitakiwa zipelekwe sampuli ambazo zinatambulika na kifaa husika!Sasa kama kifaa hakijawa designed kutoa majibu ya haitambuliki unataka kitoe hivyo?Ni sawa wewe uweke mkojo au damu ya mbuzi kwenye kipimo cha kupimia HIV,chenye outcome mbili tu ambazo ni + au -,kikipuka jibu kati ya hayo mawili utalaumu kifaa au wewe ambaye umeweka mkojo?
Njia sahibi ni kuweka damu ya binadamu ambayo tayari unajua majibu yake,fanya hivyo kwa mara nyingi iwezekanavyo ili kubaini ubora wa kifaa!Sikubaliani na aina za sampuli zilizopelekwa!
Hicho unachokisema sio sahihi mkuu, hili linafahamika mkuu kama sample iliyo pimwa sio sahihi kwa matumizi ya kifaa husika kifaa kitashindwa kuitambua hiyo sample na si kutoa majibu ya positive na negative.

Kuna taarifa huko Kenya kuna mtu alipimwa Boda ya Uganda akakutwa positive, akarudishwa Mombasa karantini akapimwa tena na majibu yakaja Negative kuwa Hana.

Tena akapimwa mara mbili kwa uhakika zaidi jibu bado ni negative.

Huoni hapo tunazidi kuvumbua utata juu ya hizi machines.
 
Sample inapoletwa maabala huwezi kujua ni ya nini kwa vile ni swab. Swab inatumiwa kuchukua sample wenye kitu chochote. Unaposiki kuwa virus wanaweza kuishi kwenye surface fulani kwa muda kadhaa in maana wamekenda kuchukua sample kutoka kwenye hiyo suface kwa kutumia means fulani ambayo kwa kawaida wanatumia swab. Kitu wanachofanya ni kuswab eneo ambalo wanafikiri liko contaminated na kupima. Sasa kama papai liko contaminated na ukaswab sehemu ambayo virus vipo papai litakutwa positive pia.
Na iliyokutwa negative nayo ilikuwa contaminated na vitu gani hadi hicho kipimo kikatoa jibu negative??
 
Ni jambo la kushangaza na kutia shaka kuona wataalam na wanasayansi wa Tanzania wanavyopinga uchunguzi wa Rais kwa hoja dhaifu.

Hii inatia shaka juu ya uwezo wa wataalam tulio nao hapa nchini.

Hebu tungalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais kwa jinsi wataalam wetu walivyozitolea maelezo.

1 vipimo ni Specific kwaajili ya kupima virus ama bacteria, hivyo huwezi kupima sample tofauti DNA/RNA hivyo basi hakiwezi kupima papai, lazima kitaleta majibu tofauti.!!

Hoja hii haina mashoka kama ni hivo kwa nini vipimo hivi vimetoa majibu ya positive na negative wakati sample sio sahihi??

Je wataalam wetu walijaribu kuvifanyia uchunguzi wowote hivi vifaa pindi vilipokaja kabla hawajaanza kuvitumia??
Kama hawakufanya kwanini waliviamini moja kwa moja, taaluma yao iko wapi hapi??

2 wataalam wengine wakaja na hoja kuwa majibu yanaweza kuwa positive kwasababu sample zinaweza kuwa zinamaambukizi (Contaminated) ama wakati wa kuchukua sample ama wakati wa upimaji hivyo kipimo kitatoa majibu Positive.!!

Okay.
Sasa kama ni hivi hamuoni hapo kuna uwezekano kuna watu ambao ni negative hawana maambukizi Ila kwasababu ya uzembe/ makosa wakati wa kuchukua sample ama uzembe wakati wa upimaji wakaiambukiza hiyo sample na kumpa mtu majibu ya positive kumbe Hana maambukizi?? Mtu unapewa ugonjwa ilihali huumwi.

Alafu hivi kama hiyo sample sio sahihi na imetoa positive kwasababu ipo Contaminated mbona sample za nanasi na kondoo zimetoa majibu negative??
Kwanini iwe negative wakati sample sio sahihi na haipo contaminated??

Hili limekaaje sasa wataalam? Inamaana kama inangekuwa haipo contaminated si ingetoa majibu kuwa haitambuliki (sample sio sahihi) kwanini Sasa ikatoa negative??

Halafu Inamaana team ya watafiti wa Rais hawakuwa na uelewa kabisaa kiasi kwamba wakazichukua sample tu ovyo ovyo bila ya umakini wowote na kuzipeleka tu zikapimwe hadi zinapata maambukizi??
Siamini kama ni wajinga kiasi hiki.

3 Wengine wanasema kuwa mh anawadharau wataalam, hana shukurani,anadanganya umma, anataka kuficha wagonjwa n.k.

Hii hoja haina mashiko.

Inakuwaje madaktari na wataalam wabobezi kabisa kwenye utafiti na vipimo unaletewa sample ya papai na fenesi unaambia ni ya binadamu halafu unakubali na kwenda kuipima??

Hii inatoa picha kuwa wataalam wetu wanalipua lipua tu na hawako makini na kazi yao, kama wako makini hili linawezekanaje??

Hamuoni hapa kunatakiwa kufanyaka uchunguzi wa kina kama Rais alivyotilia shaka??

Kumbe sample zinakuwa contaminated hapo hapo maabara na kutupa majibu ya positive kwanini waachwe Sasa??.

Watanzania wenzangu Mimi kwa maoni yangu mh Rais anahoja ya msingi sana tusimpuuze, hawa wataalam wetu ndio wanatudanganya mh Rais yuko sahihi..

Kuna sehemu haiko sawa katika hili.

Kama una majibu ya maswali hayo uje hapa ulete ufafanuzi.

Cases kama hizo huwezi kurukia kwenye conclusion kwa kutumia maabara moja.

Mngepeleka sample hizohizo Nairobi, Kampala na Kigali. Halafu ndio mje na conclusion.

Wenye akili wanaelewa namaanisha nn.
 
Ndiyo mkuu. Ukiondoa hizi Kits ambazo zimeingia majuzi PCR based techniques ziko siku nyingi tu nchini. Hizo Kits za Kichina hata za Mmarekani hazitambuliwi na WHO. Zipo kwa ajili ya screening tu.
Kwahiyo kwasasa tunatumia hizo zilizokuwepo hapa nchini au tunatumia hizo tulizoletewa??
 
Cases kama hizo huwezi kurukia kwenye conclusion kwa kutumia maabara moja.

Mngepeleka sample hizohizo Nairobi, Kampala na Kigali. Halafu ndio mje na conclusion.

Wenye akili wanaelewa namaanisha nn.
Umeyasikia ya huko Kenya na Uganda?
 
Sample kuwa contamined haina maana kuwa contamination imetokea maabara. Kwa jinsi ilivyo contamination itakuwa imetokea kule sample zilipotokea au katikati. Kwa kuwa surfaces zinaweza kuwa contaminated kwa muda mrefu mpaka siku 8 inawezekana kama zilitoka sokoni basi hizo samples zinawezekan kuwa zimekuwa contaminated na surfaces za soko or anything which came into contact with those samples. Waliozichukua hizo samples kama hawako trained wanaeza pia kuasabisha contamination.

Kama contamination ingekuwa kwenye maabara basi control samples kama vile negatine na blank samples zingekuwa na majibu yenye walakini na Wataalamu wa maabara wangegundua hicho kitu.
Ndio nakuuliza kama hizo sample ziko contaminated kwenye process yote hiyo na mtu aliye chukuliwa hiyo sample akapewa majibu ya positive Inamaana tuna wagonjwa ambao ni positive kwa makosa na sio kwamba wanaumwa Corona kama walivyo ambiwa??

Unasema madaktari wangegundua, wangegundua lini wakati tunaona hapa hadi Rais ndio anakuja kuwafumbua macho mkuu?.
 
Mnaongelea vipimo wakati watu wanakufa. Ubovu wa vipimo lawama ziebde kwa nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu kufa haituzuii sisi kujaji vipimo,

Lawama zitaenda kwa hawa wataalam wetu kwa kuto kuvichunguza hivo vipimo wakati wao ndio wamepewa dhamana na wanalipwa kwa kazi hiyo.
 
We unataka kutuambiaje sasa? Kwamba vipimo ndio tatizo au wanasayansi ndio wenye tatizo?

Vipimo ambavyo vilitumika kupima idadi ile ya watu na kukuta ma maambukizi, halafu jitihada za kimatibabu zilipofanyiwa kwa watu hao mpaka ikapelekea wapone. Unaweza kutuambia vilitumika vifaa gani kuthibitisha kua wagonjwa hao walipona?

Au ni madaktari kutoka nchi gani na vipimo kutoka wapi vilivyo confirm kua wagonjwa hao wame-recover wakati hivyo vipimo hutoa majibu ya positive katika kila test itakayo fanyika?

Mimi ningelimuona Rais ana busara Kama sehemu ya zile samples za: Mbuzi,kondoo,Kware na Papai angepeleka Kenya au Afrika Kusini halafu RESULTS ziwe compared!
Huwezi ku-conclude kws Test kit 1 tu bila kupambanisha na Kit zingine ili kuondoa any shadow of doubt!

Kwenye Maabara yoyote huwezi kuwa 100% accuracy Kama hukuchukua all necessary measures wakti wa Testing. Inawezekana kabisa samples zile zilikuwa contaminated hata kabla haxijafika Maabara Kuu a kulikuwa na Uzembe in handling the samples before and after being received at the National LABARATORY...Who knows?
 
Ndio nakuuliza kama hizo sample ziko contaminated kwenye process yote hiyo na mtu aliye chukuliwa hiyo sample akapewa majibu ya positive Inamaana tuna wagonjwa ambao ni positive kwa makosa na sio kwamba wanaumwa Corona kama walivyo ambiwa??

Unasema madaktari wangegundua, wangegundua lini wakati tunaona hapa hadi Rais ndio anakuja kuwafumbua macho mkuu?.

Kama maelezo yako ni sahihi Ina maana Vipimo vyote vya Covid-19 Tanzania Ni Fake na Ubabaishaji mtupu!
But a serious concern is this: Wagonjwa wapo na watu wanakufa kwa !!
Sasa hapa tumwamini JPM au tuwaamini Wataalamu na Maabara? Who is trying to tell the truth or lie and for whose interest????😎😎
 
Kutokana na hayo hayo unayo jiuliza ndio mana hata Rais ameamua kuita tume ya wachunguzi huko maabara kuu ili tujue kipi ni kipi kutokana na ukakasi uliovumbuliwa.
 
Watu kufa haituzuii sisi kujaji vipimo,

Lawama zitaenda kwa hawa wataalam wetu kwa kuto kuvichunguza hivo vipimo wakati wao ndio wamepewa dhamana na wanalipwa kwa kazi hiyo.

Hawa Wataalamu hawana hatia mnataka kuwaonea tu! Wao wanakuwa GUIDED na vipimo kwa kupata swap sahihi toka kwa Binadamu under suspect ya Covid-19!

Sasa Kama mtu anakufanyia HILA anakuletea OIL, PAPAI, FENESI, KWALE etc, expect a very COMPLICATED RESULTS Kama tulivosikia: INDERTEMINATE, NEGATIVE na POSITIVE altogether!!
 
Back
Top Bottom