Ni wazi kwamba ndani serikali ya JPM hakuna mashirikiano, wakati vipimo vinaendelea kulikuwa gape kama serikali wamehisi kuna sintofahamu walipaswa kutuma team ya wataalam kwenda kwenye hii maabara kujua kile wanachokiita aidha mashine feki ama uongozi wa maabara unavyokosea ugunduzi wa kuleta majibu, na hili lingefanyika pasina watanzania kujua kama yawezekana kuna weakness kwenye hii maabara ambapo saiv kuna mkanganyiko mkubwa na taharuki.
Jengine ni kwanini Rais amepeleka sample za nanasi, fenesi sjui papai kwenye mashine ya kupimia Covid-19? Kwann asingetumis sampili za binadamu tofauti tofauti? na kuzirejea hizo kwa hizo kwa majina tofauti? Huwezi kupeleka mafenes halafu ukaja kujenga hoja kama alizojenga sababu kubwa ni ile mashine je kwa mtazamo wa kawaida imetengebezwa kwa kugundua vitu ambavyo havitokani na mwadamu? Nadhan hapa chochote kinaweza kutokea kwenye majibu ni uncertain
Mimi namlaumu sana, wakati anasema aliyoyasema kwanini hakutoa way forward kwasabab amekuja kueleza yale kuna watu washatoka kwenye vipimo na zoezi linaendelea Labda lipo katikati sasa je hawa waliokwishakupewa majibu wafanywe nini? waachiwe warudi majumbani mwao kwa wale walio positive kwa vile mashine ilikuwa feki lakini je wale tulioambiwa wamepoa tuwarudishe kwa vipimo labda sample zao zipelekw nchi nyengine kwa vile Tz mashine ni za mabeberu hazina viwango ama vipi? Laki baya zaidi sasa kuna wiki 2 hakuna update yeyote kuhusu covid 19 Tz, je watu wafahamu ugonjwa wa corona hamna tena Tz, ama kama ipo ni kwa kiwango gani ili wananchi wajitathmini kwa tahadhari?
Tarehe 13 ile kamati ndio itatoa majibu, je wakileta majibu mashine ni feki ambayo si feki itafika lini kutoka wapi na itahakikishwa kwa muda gani? Kipindi hicho chote wagonjwa wa covid nchini watatambulika vipi?
Amesema wananchi wachuke tahadhari kwani ugonjwa je upo nchini? Walijuaje maana mashine ni feki ama wapimaji maabara hawana ufanisi walitoa majibu ya possitive mengi ilhali yawezekana wote ni negstive, kwanini vyuo na wanafunzi wasirudi mashuleni, kwa vili ligi itarudi soon.
Ukweli ni kwamba kunaibuka maswali mengi sana kwenye ile hutuba