Hebu tuanzie hapa: Ben Saanane alitoka kwao saa mbili asubuhi ila hakurudi mpaka leo. Yupo hai? Kuna huu ujumbe aliotuambia


Sasa kama ni hivyo kuwa hakuna mtu mwenye "authority" ya (umesema - kuhoji) elimu ama vyeti vya elimu ya mtu isipokuwa taasisi zinazohusika, then hebu jibu maswali haya:

1. Watu wote waliondolewa (sema kutumbuliwa) katika nafasi mbalimbali walizokuwa wana hold ktk ofisi za umma/serikalini iwe ktk taaluma ya udaktari, ualimu, upolisi, utawala, fedha nk nk walilalamikiwa na nani kabla?

Je, ni taasisi zilizowatunuku taaluma zao hizo?

Je, siyo kwamba ilianza kwa watu wa kawaida tu kama mimi na wewe kulalamika kwanza kwa sababu ya poor deliverance waliyokuwa wanatoa watu hawa?

Je, si sawa tu na wanao - question uwezo wa kiakili na ufahamu wa mambo wa Bwana JPM huku reference base ikianzia kwenye elimu yake?

2. Well, let's all assume that ulichoki - raise hapa ni kweli na sahihi. Na kwa maelezo yako haya maana yake ni kuwa, yeyote ahojiye uhalali wa elimu ama kiwango cha elimu ya mtu, anakuwa anafanya kosa maana kwa mujibu wako, hana authority hiyo!!

Je, unadhani kwa kuwa ilitokea (na nakuhakikishia kuwa hata sasa itaendelea tu, na kesho na hata kesho kutwa na mpaka atakapoenda kaburini) kuwa Ben Saanane alikomaa sana kuhoji uhalali wa PhD ya Bwana John Pombe Magufuli, ndiyo majibu yake ni kumuua ama kumteka na kumtesa na kumfunga bila hukumu ya mahakama ktk gereza lisilofahamika?

3. Kama unadhani uko sahihi, na kwamba alivunja sheria fulani (unayoijua wewe tu), si ilikuwa rahisi tu kwa kumfungulia mashtaka kwa mujibu wa sheria aliyoivunja?

Tena unajua nini?

Ni, kwamba Ben Saanane alikuwa anasema haya kwa uwazi kabisa na kwa sauti kubwa inayosikika vyema kwa kila mtu iwe FB, Twitter, Instagram na hapa JF alikuwa Verified Member si kama mimi na wewe tunaotumia majina bandia.

Tatizo lilikuwa nini basi hata mkaamua kumuua badala ya kumshukulia hatua za kisheria (kama alikuwa anafanya kosa?)

4. Kwa ulichokiandika hapa (nikiamini kuwa pengine uko kwenye moja ya idara nyeti sana serikalini), huoni kuwa hapa umewasilisha utetezi wa serikali na kuthibitisha rasmi kuwa ninyi ndiyo mnahusika na kumpoteza ama kumuua kabisa ndugu yetu Ben Saanane?

Ndiyo. Hata ubishe hadi mwaka 2020 lakini kubali tu umejisahau na kujikuta unajichoma mkuki mwenyewe!!
 
Uharo wa hali ya Juu kwa mwaka huu 2019 Taasis husika aihoji , ila inapaswa kukanusha ama kuthibitisha ukweli wa tuhuma hizi ...ni kama vile watuhumiwa wa uhalifu wanavyofikishwa mahakamani,wapo wanaoonekana hawana hatia na wapo wenye hatia.
Any way tumeshawazoea kumtetea na kumshangilia mfalme wa Beirut hata akikosea.....ila ipo siku Mtoto wangu atazaa na Mtoto wako utajuta kuzaliwa ...utataka kufuta makosa hautaweza.
Nyie wafundisheni watoto wenu muyatendayo sisi tunawafundisha tuliyoshindwa kuyatenda.
Natamani nitende ila umri umeenda ,but Iam telling you *bado kitambo kidogo*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ben Saanane alitumwa na Mbowe Afrika Kusini, kumbe ilikuwa janja ya kumuuwa ili kuficha wizi wa ruzuku ya chama.

Ni kama Chacha Wangwe tu alichofanyiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi wewe ni kiwavi au kirusi kinachojali tumbo lake tu? Eti ruzuku, kwani alikuwa mhasibu? Na huyo Mbowe, mamlaka inashindwaje kumfungulia mashtaka kama wewe mtu baki una ushahidi yenyewe inasubiri nini kukutumia ukathibitishe pasi na shaka? Sijui unaona sifa au unalazimisha sifa ilihali huna sifa za kusifiwa! Uone aibu na ujifunze kujenga hoja zisizo za kizushi! Hivi familia za wahanga hawa wakiona ulichoandika wanajisikiaje juu ya ushahidi huu wa kusingizia? Jiweke kwenye nafasi zao basi na pia nafasi ya Mbowe unayemtuhimu huku ukijua siyo kweli uyahisi machungu yao! Acha ujinga na siasa za kijinga hivi uwe unajitafakari kidogo!
 
Nina ushahidi wa kila aina.

Hata gazeti la Tanzania daima na mwanahalisi yaliandika kuhusu hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina ushahidi wa kila aina.

Hata gazeti la Tanzania daima na mwanahalisi yaliandika kuhusu hili

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ni mbali sana na mahakamani na najua hapo ulipo ni jirani sana na kituo cha polisi na mahakamani. Fanya hivi, chukua vielelezo vyako nenda aidha polisi au mahakamani umfungulie Mbowe mashtaka ya mauaji kwa kuwa una ushahidi. Hapo utakuwa umetenda haki kwa kuwasaidia ndugu, jamaa na wazazi wa wahanga hao! Kinyume chake huna lolote zaidi ya ulisikia na kusoma kwenye magazeti ushahidi ambao ni hafifu na dhaifu! Still wewe unabaki bush lawyer tu usiye na uelewa!
 
Hata wewe unaweza kwenda mahakamani kumshitaki Mbowe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyekua anatuma msg ni aliyekua Waziri wa Mambo ya Ndani.
 
Hata wewe unaweza kwenda mahakamani kumshitaki Mbowe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa lipi sasa? Wewe umedai una ushahidi wa kutosha ndio maana nikakuelekeza pa kwenda! Jifunze bila kufunzwa na hiyo ndiyo elimu kuu kushinda zote! Siku yakikugeukia hutoamini kwani kuna uliowaalika kuuhitaji huo ushahidi ulio nao ili wakaufanyie kazi na wakikuta hewa utajuta kuijua jf na hivi unaonekana ulipo watakudaka kama kuku wa nyama! Acha kujipa sifa na kufanya kazi isiyo yako kwani itakugharimu! Naamini wewe siyo dola na huwezi kuwa sehemu yake hivyo waachie majukumu yake wewe endelea kuimba pambio humu!
 
Sijuia hata hawa wanaotoa like wana akili timamu? Maana umeandika hovyo hovyo kabisa. Eti verified user!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Albadili imeanza nyakuanyakua.
Familia za watesi zimeanza kuonja joto la jiwe
 
Unaweza kutumia ushahidi wa gazeti la Tanzania daima na mwanahalisi kumshitaki Mbowe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kutumia ushahidi wa gazeti la Tanzania daima na mwanahalisi kumshitaki Mbowe

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwe unaelewa basi eeh! Ushahidi wa magazeti ambayo hukuyaandika wewe ni dhaifu mno na hakuna hakimu atakayekuwa tayari kurule kesi kupitia ushahidi wa kwenye gazeti! Bush lawyer vipi bwana? Nakuelimisha lakini huelewi na huenda una ubongo mzito sana! Ingekuwa hivyo wenye mamlaka wangeshautumia ushahidi huo mapema kabla yako! Ccm mna kazi sana kwani hakuna mwelewa wa taratibu za kisheria!
 
Hata hili la kupigwa Risasi lazima liongelewe kwa facts. Ni kweli kupiga au kutishia ni kosa lkn lazima tujikite kwenye facts. Ni kweli binadamu unaweza pigwa Risasi 38 na ukabaki salama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
''Kamanda'' kwa ndugu na Masela....
 
Haya mauaji ya kina Ben, Azory na wengine. Hayata kwenda na upepo bure bure tu.

Iwe miaka 5, 10, 15, 20 iyajo wahalifu/wahusika watafikishwa kizimbani na kufungwa maisha. Haijalishi vyeo walivyokua navyo au kiburi walichokua nacho.
Damu sio maji, ukiua, unakaribisha kifo kwenye nyumba yako, mafuriko makubwa ya kifo yameingia nyumbani mwako kwa kuwa mikono yako inanuka damu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…