The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Kuandika siyo tatizo ila huenda mkono wako uliokusaidia kuandika haya ukawa na kilema kama syo mkono basi kutakuwa na tatizo kwenye kokonatia!!
Kwakuwa tunapenda vitu vya uongo uongo ,,umbea, uhayawani, na masuala ya kumkandamiza mwanadam mwenzako kwa mambo ambayo nafaham nafsi inakusuta ila kwa sabab tu ya Visa vya wanadam unaweza kuongea yote Haya!!
Sina Hakika kisheria kama hata ww unaweza ama mie ninaweza kuhoji ama kutaka uhalali Wa elimu yangu!! Taasisi husika nadhani ndo zina authority hiyo nikiamni kwamba they are legalised and recognized institutions!!
You /I sina hakika kbsa kwamba you /I can question my or ur education and expecting to get a genuine answer may be according to the context of inquiry!!
Mengine haya ni kukosa tu kufikiri na kuendeleza hla tu!!!
Haya hayajaanza leo hata mataifa makubwa na yenye uwezo mkubwa kijeshi na kiusalama haya yanatokea na tusivyo na akili tunaenda ati kushtaki utafiki ni Baba zetu!!! Au kuongoza taifa la watu zaidi ya mil 50 tunalinganisha na familia zetu ambazo zinawatoto watatu lakn hata kuzi control zatushinda sembuse mamilion haya ya watu!!!!!
Mtalalamika lkn wenzenu wanatenda!!! Mtashtuka kumekucha mnaendelea kulia lia ila muda huo wenzenu watakuwa wame win!!
Heri ya mwaka mpya!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kama ni hivyo kuwa hakuna mtu mwenye "authority" ya (umesema - kuhoji) elimu ama vyeti vya elimu ya mtu isipokuwa taasisi zinazohusika, then hebu jibu maswali haya:
1. Watu wote waliondolewa (sema kutumbuliwa) katika nafasi mbalimbali walizokuwa wana hold ktk ofisi za umma/serikalini iwe ktk taaluma ya udaktari, ualimu, upolisi, utawala, fedha nk nk walilalamikiwa na nani kabla?
Je, ni taasisi zilizowatunuku taaluma zao hizo?
Je, siyo kwamba ilianza kwa watu wa kawaida tu kama mimi na wewe kulalamika kwanza kwa sababu ya poor deliverance waliyokuwa wanatoa watu hawa?
Je, si sawa tu na wanao - question uwezo wa kiakili na ufahamu wa mambo wa Bwana JPM huku reference base ikianzia kwenye elimu yake?
2. Well, let's all assume that ulichoki - raise hapa ni kweli na sahihi. Na kwa maelezo yako haya maana yake ni kuwa, yeyote ahojiye uhalali wa elimu ama kiwango cha elimu ya mtu, anakuwa anafanya kosa maana kwa mujibu wako, hana authority hiyo!!
Je, unadhani kwa kuwa ilitokea (na nakuhakikishia kuwa hata sasa itaendelea tu, na kesho na hata kesho kutwa na mpaka atakapoenda kaburini) kuwa Ben Saanane alikomaa sana kuhoji uhalali wa PhD ya Bwana John Pombe Magufuli, ndiyo majibu yake ni kumuua ama kumteka na kumtesa na kumfunga bila hukumu ya mahakama ktk gereza lisilofahamika?
3. Kama unadhani uko sahihi, na kwamba alivunja sheria fulani (unayoijua wewe tu), si ilikuwa rahisi tu kwa kumfungulia mashtaka kwa mujibu wa sheria aliyoivunja?
Tena unajua nini?
Ni, kwamba Ben Saanane alikuwa anasema haya kwa uwazi kabisa na kwa sauti kubwa inayosikika vyema kwa kila mtu iwe FB, Twitter, Instagram na hapa JF alikuwa Verified Member si kama mimi na wewe tunaotumia majina bandia.
Tatizo lilikuwa nini basi hata mkaamua kumuua badala ya kumshukulia hatua za kisheria (kama alikuwa anafanya kosa?)
4. Kwa ulichokiandika hapa (nikiamini kuwa pengine uko kwenye moja ya idara nyeti sana serikalini), huoni kuwa hapa umewasilisha utetezi wa serikali na kuthibitisha rasmi kuwa ninyi ndiyo mnahusika na kumpoteza ama kumuua kabisa ndugu yetu Ben Saanane?
Ndiyo. Hata ubishe hadi mwaka 2020 lakini kubali tu umejisahau na kujikuta unajichoma mkuki mwenyewe!!