Hebu tuanzie hapa: Ben Saanane alitoka kwao saa mbili asubuhi ila hakurudi mpaka leo. Yupo hai? Kuna huu ujumbe aliotuambia

Yaani mie natamani kama hawajakamalizia, wakamalizie kabisa, kafie mbele huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu umeongea maneno ya msingi sana.

Bahati mbaya vijana wengi hawapendi kusikia haya maneno wakiamini ni mashujaa,wanaweza waka tu offer chochot kipya ili kujijengea heshima na msingi imara katika safari yao ya kisiasa.

Leo hii tunapaza sauti namna bora hata ya kukosoa utawala kwa manufaa ya taifa kwa ujumla,watu hawaelewi,wanajisahau kwamba hata hii jamii forums tuliishaikosa kwa mwezi mzima kisa tu watu walichukia.wakaamua kufanya wanayojisikia,siku isiyo na jina inaweza ikafungiwa kabisa,tukakosa hata kibaraza cha kujadili,na hakuna panya wa kufanya chochote.

Mwisho niseme tu,mwenye pesa,au mamlaka si mwenzako dunia hii,labda subiri awamu nyingine mbinguni,kumkwaza kwa namna yoyote ni kujitafutia matatizo yasiyo na ulazima,ndio maana wenye busara hukaa kimya.
 
Haya yanatokea Tz tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Heri ya mwaka mpya kaka Misuli. Nimepishana na gari lako unaelekea Mtwara. Nimeona lina ulinzi mkali sana. Najua ilikuwa ni hela za kulipa wakulima wa korosho, maana mlisema siku 2 mtakuwa mshawalipa wakulima. Zikibaki kidogo niite hata tupige supu ya samaki wakati tunajadili hayo mafanikio.
 
Samahani mkuu..
Mo dewji hakurudi na majeraha kama akina ulimboka, kwahiyo hakutekwa.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ben saa nane alipitiliza kwenye unazi wa kijinga. Alitaka kujionyesha mkereketwa wa chadema na mfuasi mahiri wa falsafa ya umangi eti 'kujitambua' huku ukweli ni falsafa ya ubinafsi na ukabila. Baada ya cdm kushindwa walihamaki na kuanza campaign ya kumtukana kumzarau na kumbeza jpm kinara akiwa lissu. Ben saanane alipewa au kujipa shughuli ya kuonesha jpm kama mtu mjinga mwenye shahada ya phd feki. Alitumia uongo wa kustaajabisha na hadaa yenye maudhi kwelikweli.
Nachotaka kusema rais wa jamhuri ni mtu anayestahili heshima na kisheria wananchi wanawajibika kumpa heshima. Wapo wateule wa rais kikatiba wanawajibika kuonesha utii wa hali ya juu. Huenda ben alijitafutia balaa mwenyewe japo tofauti ndani ya cdm yenyewe inawezekana ndio chanzo cha yeye kutoweka.
 
Nimesikitika sana kuwa unaandika upuuzi uliochanganywa na kiingereza kibovu ili mradi tu uhalalishe masahibu yaliwapata akina Ben Saanane!!!? Haya onyesha ni sheria ipi au kanuni inayozuia mtu kuhoji elimu yako au ya mwingine yeyote. Mbona kwenye kuhakiki vyeti mlihoji uhalali wa elimu ya watu wengi tu, ila ilipofika kwa Bashite akaonekana ni malaika. 'Why the double standard'!!!!!!!?
 
Sababu No. 2 ndo naiona inachukua uzito wa kipotea kwa Sanane. Kama Sanane aliuawa itakuja kujulikana tu, regardless miaka mingapi itapita. Waliowaza kumuua na waliotekeleza mauwaji watakuja kujulikana hilo halina wasiwasi.
 
Umeandika article ndefu lkn ni upupuuuu.....

Once a person become a public figure, hata vaa yake, maamuzi yake, lifestyle, mahusiano yake na wengine etc.... huwa inaweza hojiwa, kama hata mavazi yanahojiwa why not elimu kitu ambacho ni moja kati ya criteria muhimu?




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kweli "Misuli"; unajaribu kuyeyusha hoja inayodai uhai wa mtu kwa maneno rahisi.
Haya tengeneza hiyo muvi yako tuione. Tuone jinsi gari jeupe lilivyomfuata Lisu, tuone jinsi sherehe adhimu ilivyofanyika kwenye Kasri ya Mfalme bila ya kuwepo mwana mpendwa, tujiulize mwana mfalme alikuwa umbali gani toka mahali risasi zilipomiminwa kwa Lisu, tutazame jinsi cctv camera zilivyonyofolewa na kutupiliwa mbali na nani alitoa agizo hilo lenye lengo la kupoteza ushahidi.
Hatutaki tuishie hapo, utuonyeshe jinsi Watanzania kwa maelfu yao walivyozuiwa kukusanyika kumwombea Lisu makanisani na misikitini; kitendo kilichofanywa na askari wa dola hadharani, pia usisahau jinsi mfalme alivyokataa kusaini fedha kwa ajili ya matibabu ya raia wa Tanzania aliyeangukia kwenye madhila makuu ya kupigwa risasi 38.
Ee Mwenyezi Mungu mweza wa yote, mpe huyu ndugu uwezo wa kutengeneza filamu murua ya Madhila ya Ndugu zetu hawa!!!!
 
Movie inatakiwa uanze kuitengeneza kuanzia Lisu anafuatwa fuatwa toka Dar na anaenda kuongea na waandishi wa Habari na sio polisi. Tunaenda anatoka bungeni watu walewale wa Dar wanazid kufuatilia hadi anaenda home kwake, hapa hakuna kusimama ye ni kuendelea na safari tu.Tufanye hayo ni trailer, movie kali sana ni pale jamaa wanashuka na mabunduki ya kivita ye na dereva wako ndani tu.Mara dereva analaza kiti na anamlaza lisu na yeye anashuka na kujificha chini ya gari.Movie inaendele mara paaaaaap risasi zinaanza kumiminwa kama njugu. Anapigwa risasi 38.Hapa tuchukue mfano risasi moja ni sekunde 1,so wanatumia zaid ya nusu dakika kumshambulia lisu na wakati huohuo hawajui hizo risasi zinamfikia au lah,wao ni kufyatua tu.Mwisho wanaondoka na dereva anaenda kumuokota lisu.Movie bado tu ni kwamba lisu bado alikua na faham licha ya mashambulizi ya siraha ya kivita na kupigwa Risasi 38.Utamu wa movie ni pale Lisu kuwa na faham licha ya risasi kupigwa karibu na spinal cord. Kwa wanaojua kazi za spinal cord basi hapa hii movie itawafurahisha sana.Movie bado ndefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya yako ni mawazo ya Kishetani. Hivi nyie watu wenye hoja na mawazo ya karne za ujima huwa mimba zenu zinatungwa kwenye kona zipi za hapa duniani!!!!!?
Hivi unajua kuwa raia wa Tanzania ndiye bosi wa kiongozi yeyote wa nchi hii? Raia anayo haki ya kikatiba ya khoji uhalali wa jambo lolote juu ya kiongozi yeyote. Soma Katiba ibara ya 8 (a) na (b). Kumlinganisha kiongozi wa karne ya 21 na Sulemani wa karne 9 BC ni kutaka kutuaminisha ujinga
Yeyote aliyemhukumu Ben kwenye Mahakama ya Kangaroo ana hatia ya damu yake.
 
Endeleza Mzaha, nakutakia kila la heri, "hujafa hujaumbika" mwanangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…