Hebu tuanzie hapa: Ben Saanane alitoka kwao saa mbili asubuhi ila hakurudi mpaka leo. Yupo hai? Kuna huu ujumbe aliotuambia

Hebu tuanzie hapa: Ben Saanane alitoka kwao saa mbili asubuhi ila hakurudi mpaka leo. Yupo hai? Kuna huu ujumbe aliotuambia

Ukitaka jamii ikuone jasiri kemea jambo lenye masirahi kwa jamii hata kwa kulia utaeleweka na siyo kubwabwaja maneno ya kumlenga mtu, YOU WILL DESTROYED
 
Mikono ya mfalme imejaaa damu na laana za watu hawa ndio zinamtesa kila alifanyalo anavurunda.
Siku akiamua kuoga hadharani ndio wataukumbuka ule ushauri wa Zitto kutumia kipengele kile cha katiba kwa ajili ya chek up ya uhakika wa dish kukaa vizuri
 
Haya mauaji ya kina Ben, Azory na wengine. Hayata kwenda na upepo bure bure tu.

Iwe miaka 5, 10, 15, 20 iyajo wahalifu/wahusika watafikishwa kizimbani na kufungwa maisha. Haijalishi vyeo walivyokua navyo au kiburi walichokua nacho.
Mbona damu ya chacha wangwe na mtikila yenyewe ilienda na haulalamiki,na hii itaeenda bure tu kama za hao wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hatari,, africa viongoz hawataki wakosolewe,, utapotea familia yako ibakie na upweke bila ht kuona kaburi lako,, Ben alikosea kumshambuliaa Ngosha kiasi kile,japo Kweli hata sisi wengine anatukera lakini hatuvuki mipaka
Hakika mkuu.... angeweka critics zake kwenye mfumo wa swali then angetembea zake kuwaacha watu wajadili. Alionekana kumkamia binafsi mfalme, hakusoma alama za nyakati za mfalme wa sasa.

Bro nikikutukana wewe kuwa ni mlemavu wakati sio mlemavu, utakasirika. Lakini nikikutukana wewe ni mlemavu ilihali ni mlemavu kweli utakasirika zaidi. Utahisi nakudharau na kukudhihaki, Utatafuta namna ya kunikabili. Ndicho kilichotokea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ben Saanane alitumwa na Mbowe Afrika Kusini, kumbe ilikuwa janja ya kumuuwa ili kuficha wizi wa ruzuku ya chama.

Ni kama Chacha Wangwe tu alichofanyiwa

Mkuu hauna ushuru Mdomo, chunGa Ulimi usilete mgogoro
 
Mwenzenu Kubenea alisema Ben hajapotea yupo anakula bata na washkaj zake. Mkikosa kiki mnaanza porojo porojo....
 
Hakika mkuu.... angeweka critics zake kwenye mfumo wa swali then angetembea zake kuwaacha watu wajadili. Alionekana kumkamia binafsi mfalme, hakusoma alama za nyakati za mfalme wa sasa.

Bro nikikutukana wewe kuwa ni mlemavu wakati sio mlemavu, utakasirika. Lakini nikikutukana wewe ni mlemavu ilihali ni mlemavu kweli utakasirika zaidi. Utahisi nakudharau na kukudhihaki, Utatafuta namna ya kunikabili. Ndicho kilichotokea

Sent using Jamii Forums mobile app
Exctly
 
Juzi niliona picha ya Rais Magufuli akimuombea mama yake mzazi ambaye amepatwa na maswahibu kama yaliyokatisha uhai wa binti yake ambaye alizikwa hivi karibuni.Nilipomuona nilijikuta nikiwaza sana!

Turudi kwenye mada. Ben Saanane mara ya mwisho kabla hajapotea alitoka kwao asubuhi kama kawaida kwenda kwenye mihangaiko ila hakurudi tena hadi leo. Siku chache baada ya kupotea namba yake ikaondolewa kwenye makundi yote ya WhatsApp naamini alikuwa akishurutishwa fanya hili...fanya hili...Siku baada ya siku hadi alipomaliza yote. Mbaya zaidi kuna ujumbe aliotuachia "Tuutafakari" ambapo alikuwa akilalamika kuwa yupo mtu mmoja alikuwa akimtumia ujumbe kila alipokuwa akiishambulia elimu ya mfalme kule kisiwani kwenye mitandao ya kijamii kuwa "mara umebakiza post tatu mara mbili" na mwisho kabisa akamwambia "Naamini sasa hutapost tena" Ujumbe zaidi aliambiwa "Baba yako atajilaumu sana kwa kukusomesha na sasa hatayafaidi matunda ya elimu yako,Ben wewe bado ni kijana mdogo sana kufa"

Ninachoamini ni kuwa dola inajua kabisa yaliyomkuta Ben. Kama sivyo basi wangeshachukua hatua stahiki. Emb fikiria watu wote waliokuwa wamekithiri kwa ukosoaji kipindi kile walifanywa nini? Tundu Lissu mbunge na mwanasiasa maarufu sana alishambuliwa kwa risasi nyingi mchana kweupe tena mbele ya makazi yenye ulinzi mkali na hakuna chochote mpaka leo. Njoo kwa kuke kwa ofisi za Fatuma Karume hadi bomu likarushwa kwenye ofisi zao. Kina Roma walivyopigwa kwenye majumba yasiyojulikana! Itakuwaje kwa Ben aliyekuwa naye amekithiri kwa ukosoaji?

Mimi naweza kufikiria haya na huenda moja wapo likawa sahihi
1. Huenda Ben kapigwa ban labda kwa kipindi fulani....Ila hapana, siku wakimtoa huko je? Si wataaibika?
2. Huenda walidhamiria kumpiga kisha wamuachie ila wakazidisha kipigo na ikawa bahati mbaya jumla!
3. Au moja kwa moja walimmaliza.
4. Au labda walimpa ofa ya kwenda nchi za watu kukaa tu huko ili asiwe tena anashambulia....Thubutuuu yani mfalme umkosoe, uwe mfuasi wa "mabeberu" halafu akupeleke kula bata?

Wazo namba 2 linanishawishi nikubaliane nalo zaidi kwakuwa naamini hata kina Roma Mkatoliki na wenzake walipokuwa wanapigwa kama ingetokea bahati mbaya iwe jumla basi nao wasingeonekana mpaka leo.Linanishawishi nikubaliane nalo kwakuwa wote waliokosoa walielekezwa kwenye mfumo huu wa kupotezwa ila baadhi yao Mola akawanusuru!

Kuna kile kipindi maiti zilikuwa zinaokotwa kiholela sana kule baharini mara mto Ruvu huku zikiwa zimefungwa kwenye viroba. Hiki ndicho kipindi kile cha kukamatwa watu kule MKIRU na kwenda kuona joto la motoni kule Stakishari! hiki ndicho kipindi kilichokuwa muda mfupi tu tangia Ben atoweke. Ndicho kipindi alichopotea Azory.........Mbona siku hizi zile maiti za "wahamiaji haramu" hazipo tena? Kwanini kipindi kile ziliibuka sana zikiwa zimefungwa kwenye mifuko huku sisi wengine tukielewa kuwa kule Stakishari kulikuwa na kwata la kufa mtu likiendelea? Hadi watu wakawa wanatambaa kama nyoka? Kwanini kwanini kwanini?

Ukweli wa haya naamini kuwa hautajulikana kama tutaujenga "mfumo mfalme wa kisiwa" kama tulivyotahadharishwa humu Jf......"Mfumo mfalme huyu" ni hatari kwa afya yetu hivyo tuchukue tahadhari mapema sana.
Unaonaje kama ukaisadia Polisi na uje na ushahidi uliokamilika Central Police Dar
 
.
rejea maiti 11 za wahamiaji haramu zilizookotwa barabarani majuzi kati- sifa za waongo na wach0chezi huwa ni kukosa kumbukumbu
Na zenyewe zilikutwa kwenye viroba? wewe kaa kimya kwa vile halijamkuta ndugu yako. Lakini habari za kutoka ndani ni kuwa miaka hii mitatu matukio haya ni makubwa kuliko awamu ya tatu na nne
 
Kuandika siyo tatizo ila huenda mkono wako uliokusaidia kuandika haya ukawa na kilema kama syo mkono basi kutakuwa na tatizo kwenye kokonatia!!

Kwakuwa tunapenda vitu vya uongo uongo ,,umbea, uhayawani, na masuala ya kumkandamiza mwanadam mwenzako kwa mambo ambayo nafaham nafsi inakusuta ila kwa sabab tu ya Visa vya wanadam unaweza kuongea yote Haya!!

Sina Hakika kisheria kama hata ww unaweza ama mie ninaweza kuhoji ama kutaka uhalali Wa elimu yangu!! Taasisi husika nadhani ndo zina authority hiyo nikiamni kwamba they are legalised and recognized institutions!!

You /I sina hakika kbsa kwamba you /I can question my or ur education and expecting to get a genuine answer may be according to the context of inquiry!!

Mengine haya ni kukosa tu kufikiri na kuendeleza hla tu!!!

Haya hayajaanza leo hata mataifa makubwa na yenye uwezo mkubwa kijeshi na kiusalama haya yanatokea na tusivyo na akili tunaenda ati kushtaki utafiki ni Baba zetu!!! Au kuongoza taifa la watu zaidi ya mil 50 tunalinganisha na familia zetu ambazo zinawatoto watatu lakn hata kuzi control zatushinda sembuse mamilion haya ya watu!!!!!

Mtalalamika lkn wenzenu wanatenda!!! Mtashtuka kumekucha mnaendelea kulia lia ila muda huo wenzenu watakuwa wame win!!

Heri ya mwaka mpya!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna neno hata moja na lenye kuleta mantiki kwa aliyoyazungunza mleta mada.

Bora ungekaa kimya tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupigwa risasi sio hoja,Hoja ni kupigwa Risasi 38.Hivi ulishawah fanya imagination ya tukio lenyewe na uangalie linawezekana au lah?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nafikiri hata kukusudia tu kumpiga mtu risasi iwe moja au elfu 1 ni kinyume cha ubinadamu, na utawala wa haki! Lakini hoja ama swali langu la awali kwa eltwege, lilikua; alichookiandika ni fact au amesukumwa na chuki yake dhidi ya CHADEMA, hizi risasi 38 wala sijaziongelea!
 
Back
Top Bottom