Hebu tupige story kidogo kuhusu ukatili katika ndoa, je ndoa za wake wengi nako kuna mauwaji?

Ni nadra sana mtu mwenye mke zaidi ya mmoja kunyimwa unyumba, maana Kila mwanamke anapambana kumfurahisha mume wao, binafsi naona kama mtu anajiweza kiuchumi ana afya njema nk, unaweza kuwa na mke zaidi ya mmoja

NB: ni vizuri zaidi kama watakuwa hawaishi nyumba moja Kila mwanamke awe na mji wake
 
Actually na biologically mwanaume unashauriwa uoe wanawake kuanzia 2 na kuendelea...

Kuoa mwanamke mmoja ni tatizo lako binafsi tu, sawa na yule asie oa kabisa kwa matatizo yake binafsi....hasa ya kimwili na kiakili.

Kuingiza sababu za kiuchumi kwa kushindwa kuoa wanawake kuanzia 2 na kuendelea hzo ni janja janja tu.

Wanawake kuna vitu wanaviitajia kutoka kwa wanaume mfano, heshima, usalama, na uhakika wa kula, kulala na kuvaa yeye na watoto wake....hayo mengine mengine sijui ya kumuongezea mke anakaza fuvu tu hataki ila ukimletea na kumuhakikishia mahitaji yake hayo anapata hawana shida kabisa.

Sema polygamy sio kwa mwanaume dhaifu.....inatakiwa uwe umekomaa kweli kweli, na uwe mtu wa misimamo.
 
Acha niwaibie Siri Leo! Ile Siri kati ya Hawa na Shetani ( nyoka) imeanza kuvuja. Kuna wanaume wasioweza kubeba vitu vizito vifuani. Hao baada ya kupata hiyo Siri wanaona Bora wamalizane na wake/ wapenzi wao. Ndugu zangu tusidadisi mambo ya ndani Toka kwa wenza wetu, Ili tuishi kwa amani na utulivu. Kumbuka Ile Siri ilikuwa kati ya 2 tu, wewe hutakiwi kuijua. Ukiinasa tu basi umauti unachungulia hapo. Tuwe majasiri na tusitake kuyajua yasiyotuhusu.
 
INASEMEKANA:
wanaume wenye wake wengi ndio wenye maisha marefu, ebu na wewe chunguza huko unako ishi
Hakuna matukio ya ukatili wa kijinsia
Mungu mwenyewe alikua upande wa Mitume na manabii wenye wake wengi kama:
1. Ibrahimu
2. Yakobo (Israeli)
3. Musa
4. Daudi
5. Sulemani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…