Hebu tuyaangazie mafanikio ya Diamond Platnumz mwaka huu wa 2018. Tunaweza pata cha kujifunza

Dong Jin

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2018
Posts
968
Reaction score
2,034
Msanii diamond platnumz ni moja ya wasanii wenye mafanikio sana katika medani ya muziki Tanzania na Afrika kiujumla... safari yake kimziki ilianza miaka tisa iliyopita (2009) baada ya kutoa wimbo wa "nenda kamwambie" ambao ulimtangaza vilivyo na hapo hapo kuchomoza. Mapito yake mpaka alipofikia leo ni makubwa na ya kukatisha tamaa kwa mtu mwenye roho nyepesi... tuachane na hayo twende kwenye maada husika.... Tuangazie katiaka nyanja mbalimbali....

Tukianza na MUZIKI
Kwa mwaka huu diamond kafanya poa sana kimuziki. Kaachia albamu ya A BOY FROM TANDALE ambayo ukisikiliza nyimbo zake mule sio za kitoto... unajua kweli kuna gwiji wa muziki kakaa hapa. Albamu ina ngoma kibao zinazohit mtaan... zikiongozwa na "AFRICAN BEAUTY" Alomshirikisha mwimbaji wa kimarekani Omarion....
Kwenye upande wa kolabo usipime... nadhani kila unayesoma huu uzi unaijua vizuri shida ya KWANGWARU huko mitaani... kuna TIME TO PARTY aliyoshirikishwa na Mr flavour, na hii hitsong ya sasa ambayo wabongo tunaiita homa ya jiji #JIBEBE Idea ya kijana wake Mshedede almaarufu kama Mbosso... Moja ya ngoma ambazo mond kafanya na kashirikishwa zkifanya poah sana huko kenya kwnye mtandao wa itunes

Master of collabos... πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ

Tukija upande wa MATANGAZO ya makampuni...
Diamond kasaini mikataba mingi minono minono na makampuni makubwa duniani. Kasaini mkataba na kampuni ya vinywaji ya kifaransa Bellaire... Bellaire yenye nembo ya diamond platnumz

Kasaini mkataba na gucci kampuni kubwa duniani la nguo ambao wanavalisha lebo na familia nzima... Gucci
GSM MALLS nazo bado zina mkataba naye... Bado pia dili na Safaricom ya kenya ambayo ni sawa na Vodacom kwa Tanzania.... Anamkataba na kampuni ya Cocacola iliyomfanya hadi kutengeneza wimbo spesho wa kombe la dunia wa #COLOURS na Jason derulo...

Kwa upande wa SHOWS...
Mwanzoni tu mwa mwaka huu diamond alipiga show km tatu hivi mfululizo huko Kenya... Baadhi ya poster za show huko Kenya

Akaja akapiga show kubwa kabisa Kenya hukohuko siku ya uzinduzi wa albam yake ya " A BOY FROM TANDALE".... alifunika pia kwa kujaza uwanja wa taifa kwenye siku ya kumtambulisha mbosso "MBOSSO DAY"... Mbosso day

Mwezi wa tano alienda kwenye show ya ONE MUSIC FEST inayowakutanisha mastaa kibao kutoka Afrika huko London.....
....

Pia alikuwa na show huko sweden ndani ya mwezi huo huo...
Kama hiyo haitoshi akafanya tour ya albamu yake katika miji kumi huko marekani... poster ya show zake zote

Hakukaa akaelekea Mayotte ambako nako akafunika vya kutosha...

Hakupoa tena huyooo Madagaskar ambako akaenda kujaza uwanja wa mpira... show ya mond alojaza uwanja huko madagascar

Hapo bado haitoshi ana show tatu kubwa huko Kanada mwezi wa kumi na moja...

Kuna One music fest dubai inakuja....
Kuna nyingine hv karibuni mwezi huu huko Namibia.......

Pia kuna wasafi festival tumeambiwa inakuja

Kwenye upande wa BIASHARA
Diamond platnumz ni mmoja ya wasanii wanaoiogopa sana kesho yao.. ndio maana kawekeza sana kwenye mziki wake na nje ya muziki... Ni msanii pekee kwa Afrika mashariki kuwa na Vituo vyake ya habari ambavyo ni Wasafi tv na Wasafi fm...kwa upande wa Afrika wapo wawili tu na yule mnaija Olomide...
Pia ana karanga zake Diamond karanga ambazo zinafanya poah sana sokoni na kupitia hizo karanga kuna vijana wamebadirisha mpaka maisha yao kwa ofa mbalimbali zinazopatikana humo ambapo zawadi kubwa ya gari iliyotolewa kwa bwana Said wengine walidai imeizid hata ile ya miss Tanzania πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚... kijana akiwa kwenye gari alilojishindia
Ana perfume zake zinazofanya poa sana huko uarabuni... ana lebo ambayo ni miongoni mwa lebo kubwa sana hapa Afrika yenye wasanii A-LIST ARTISTES ambao wana vibao vinavyosumbua sana mitaani... kama Chombo na Pochi nene kutoka kwa Rayvanny, Kwangwaru kwa Harmonize, Nadekezwa yake Mbosso, na Gundu ya Lavalava... Jibebe pia haijasahaulika hapo... ana studio yake binafsi ambayo imefanya poah sana kwa mwaka huu chini ya laizer (magic fingers).... Baadhi ya nyimbo za wasanii wa WCB Wasafi zinazofanya vizuri kwenye mtanfao wa boomplay music

Kwenye upande wa JAMII inayomzunguka
Vijana wengi wameinuliwa na diamond katika nyanja mbalimbali.. kuanzia watangazaji wa tv na redio, madansa, wasanii, wapiga picha, walinzi, wafanya usafi, madesigner, watu wa matangazo, nakadharika.... Kuna vijana waliojiajiri kupitia miradi ya diamond karanga na perfume.... Amekuwa piah akiwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu, wagonjwa na yatima nje na ndani ya Tanzania Diamond akiwa huko Rwanda na watoto wenye matatizo ya macho

Bado skendo za ajabuajabu ambazo zimewainua wengi akiwemo Hamisa na wengine wote waliowahi kuhusishwa naye kimahusiano.... Bila kuwasahau wale wenye page za udaku na utube channel zinazotegemea mond afanye kitu ili wapate cha kupost wabust followers na subscribers wao....

Hizo ni baadhi tu ya yale mengi ambayo diamond kafanikisha kujiweka mahali salama.... hapo hatujazungumzia upande wa tuzo zake... kama ile ya mtv ya MVP...
Nominations kwnye afrimma USA vipengele sita na afrimma NAIJA... marry you kufikisha mauzo ya platinum mara sita (6Γ— platinam sales),

Kuimba mbele ya rais siku ua kuingia kwa ndege yetu pendwa Bombadier.... na ile inshu ya kuwa moja ya wasanii wanne kutoka Afrika ambao Billiboard walisema ni tishio la dunia baadae... wengine ni Wizkid, Davido, na Tiwa sawage

Kiufupi mondi sio wa kispotispoti sidhan km ataweza poromoka leo au kesho....
 
Kwahiyo Tujifenze nini hapo. Know that siyo kila opportunity inayo mtoa mtu. Inaweza kukutoa na wewe. Tuliza mind Fanya kazi uipendayo
 
Kwahiyo Tujifenze nini hapo. Know that siyo kila opportunity inayo mtoa mtu. Inaweza kukutoa na wewe. Tuliza mind Fanya kazi uipendayo
Mi hii ndo kazi niipendayo... je ww unafanya kazi uipendayo? Mi mind uangu ina hang hang... je ww yako imetulia? Mi siijui ni opportunity gan itantoa, je ww unaijua opportunity itayokutoa au iliyokutoa? Ukiweza kuyajibu haya maswali ntakuona ni mtu makini sana... kumbuka sio maswali rahisi km unavoyafikiria. Km huez n bora upite hivi....
 
Mbona kuna Alikiba mmoja humu kaanzisha Thread eti "Diamond ameisha mvuto"? Mi nikamwambia kashangilie yanga huko.
 
matango pori Madagascar ilikuwa festival kama fiesta hapa kwetu...alafu ile show ya New York aliimbia viti mbona hukuitaja
 
Ngoja team kibakuli wasikie domo kafanya yake 2018 [emoji38][emoji38]
 
Mkuu umetisha simba asiefungika ni hatari
 
Hili bandiko limetokea Madale kabisa, hakuna shaka
 
Kuna kitu cha kujifunza hapa ingawa haters ni wengi mno! Big up mond na uzidi kuchanja mbuga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…