Heche adai mahakama inatumika kumkandamiza Lissu

Kipaumbele ni kiongozi wa Chama aachiliwe bila masharti yoyote. Usifanye kama kushikiliwa kwa Lissu kuwa ni jambo dogo. Hiyo ndiyo issue na agenda kuu!
Can't say it any better!

CHADEMA sasa ni lazima ajenda yao kuu iwe ni hatma ya Mwenyekiti wa chama. na hizi mbinu zote nyingine zinazotumia mahakama kuwabana.

Chama kina 'asset' ya wanachama wake na wapenzi wa chama hicho nchi nzima, na waTanzania wengine wote wanaoitakia mema nchi yetu.

Hawa wote wasiwe washirika bila ya kupenda katika kudidimiza taifa hili.

Ni wakati sahihi kuzitumia raslimali za chama hiki kupata mabadiliko chanya.

Wakiamua kutumia njia za maandamano, wasiyafanye nusunusu; ni lazima yawe ni maandamano ya kuzoa takataka zote ikibidi.
 
Kwanza kabisa nimpe Pole Heche.

Hicho anachokisema kila mtu anajua.Hicho kinachofanyika kila mtu anaona.Tanzania ina wananchi zaidi ya Milioni 60 na wote wanaona.Sasa habari ya kulalama tu bila kuelewa hasa anachotaka naona kama anasahau kwamba anachopitia Tundu Lisu ndio Gharama ya kutafuta haki ndio njia ambayo unapoamua kupambana na Dhuluma basi itabidi uwe tayari kukabiliana nayo.

So kama hajui nini cha kufanya atafute kazi ya Kufanya.Kule Jela Tundu Lisu yupo anafanya kazi yake.Ile ni sehemu ya kazi yake ili akitoka huko awe anafahamu kwamba Ukombozi una gharama gani.

Mahakama inatka kumwachi Tundu Lisu ila haiwezi mwachia kwa sababu ni Tundu Lisu.Tundu Lisu alishasema hayuko tayari kuachiwa kwa Masharti yoyote yale wala makubaliano yoyote yale na Chadema wakasisitiza hivyo hivyo kwamba wanataka unconditional release.

Ushauri wangu.There is only One Life.Chadema Watulie waingia makubaliano wapewe hayo masharti ya kuachiliwa kwa Lisu wayaweke in Public kisha warudishiwe mwenyekiti wao kisha waache COURT of PUBLIC OPINION Iamue.

Hii habari ya kurudia maneno yale yale ni Dalili kwamba kuna kukata tamaa.Msikate tamaa.Watanzania wanawategemea ila Tumieni Hekima.You cannot beat them in their Courts unless beating them means they win.

Mnakumbuka Mbowe alipkuwa na Kesi?Alisoteshwa vya kutosha na mwishowe akanyoosha mikono na kutafuta maridhiano akaachiwa mkamuita msaliti mkamtoa kwenye uongozi.Tundu Lisu yeye ameamua kukaza kama shujaa ninyi mliobaki huku mnatakiwa muwakeep Busy kwenye Politics na Ufuatiliaje vinginevyo itawachukua muda sana kuelewa kinachoendela na kufikia malengo.
 
Wanachama wetu na Watanzania hawataendelea kukalia kimya uonevu wa wazi kwa mtu asiye na hatia."
Wanawake wa CHADEMA juzi wameonyesha mfano hai; wakapigwa mabomu ya machozi.

Ni muhimu sasa chama kwa ujumla wake sasa kijipange kutimiza kazi hii kwa ufanisi.

HAKI inayokanyagwa waziwazi kabisa; kuidai liwe ni kosa?
 
Home boy ana Msaada gani Kwa Mwigulu na chama chake?

In fact homeboy akiwa free Mwigulu anapoteza u PM

Mwisho Kila mtu ana Mungu wake na shida zake.
 
Kuwa Jaji bongo ni aibu samtaimu, pamoja na malipo kiduchu. 😊
Bongo mahakama ni kinyago tuu. Mahakama huru ipo Kenya kwa ukanda huu wa mapoyoyo. Huyo jamaa anaweza kaa gerezani kwa miaka mingi sana bongo hii.
Mahakama huru ni pesa na madaraka.
 
Alichokiandika kina ukweli kwa 100%
Binafsi ninachukizwa sana na huu uonevu wa kipumbavu unaofanywa na watu wenye mamlaka. Kuna kundi la watu wachache wanajiona kama hii nchi ni mali yao, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
Wanasiasa si Huwa mnatunishiana misuli? Mmja alisema atakinukisha na kuvuruga uchaguzi na akathubutu kuitikisa Nchi akisaidiwa na Mabeberu Sasa ni zamu yake,apambane.

Binafsi sijawahi na haitakuja kutokea nikamuonea huruma mwanasiasa Kwa sababu hao hawana Msaada wowote Kwa mwananchi.
 
Kwako wewe haki ni kumuachia Lissu tu?
 
Kwako wewe haki ni kumuachia Lissu tu?
Sitaki aachiwe nataka kesi iendelee kwa wakati, kama anaachiwa aachiwe kwa haki na sio hisani ya yoyote ama kumkomoa. Maana kama ni kesi ameshawashinda hao vilaza mliowapaga. Hata majaji wanaoendesha hiyo kesi wanaona aibu kuendelea nayo, ni basi tu ni mahakama za simu moja.
 
Dini ni nyenzo mojawapo ya watawala kutawala vizuri kwa wepesi raia wake, haina maana nyingine kubwa sana kwa watawala kama mnavyofikiria mkiwaona kanisani na misikitini.
Sahihi kabisa, na hao viongozi hawaendi kwenye nyumba za ibada kwasababu ya imani zao kwa Mungu, bali ni sababu ya background zao, au kama fashion ili ionekane ni wacha Mungu. Lakini hakuna lolote wanaamini zaidi ya madaraka na utukufu waupatao kupitia madaraka.
 
Sahihi sana haya usemayo.
 
Ni wakati Watanzania wote wanaoitakia mema Tanzania, bila kujali itikadi zao, kujitoa mhanga kwa ajili ya Lissu kama yeye alivyojitoa mhanga kwa Tanzania kwa miaka takribani 30 sasa.

Upepo wa kisiasa upo upande wa CHADEMA sana kwa sasa.

Huu ni wakati wa kuhesabiwa.
 
Hao Majaji ndo wanahudumia Kanda Nzima kuna Mahahabusu Keko, Segerea nao wanahitaji kesi zao kusikilizwa no one is Special majaji wanavyopanga tarehe kuna majukumu wanayatimiza mbona mnataka Lissu Aonekane so special?
 
Tayari wanawake wa CHADEMA wameonyesha mfano juzi walipokataa amri batili ya kuzuia wasikutane wakati wa maadhimisho ya sikuu ya wanawake duniani.

Huu uwe ni mwanzo wa hatua nyingine kwenda mbele.

Kukaa tu na kusubiri, au kulalamika mara moja moja hakusaidii chochote na hawa watu waovu kabisa..

Kazi ya CHADEMA iwe ni kuongoza juhudi za waTanzania wote wasiokubali uovu wa hawa watu.
 
Hao Majaji ndo wanahudumia Kanda Nzima kuna Mahahabusu Keko, Segerea nao wanahitaji kesi zao kusikilizwa no one is Special majaji wanavyopanga tarehe kuna majukumu wanayatimiza mbona mnataka Lissu Aonekane so special?
Asingekuwa special asingekuwa anapewa ulinzi special na mzito kiasi kile. Kesi ya uhaini hauwezi kulinganisha na kesi ya kuiba kuku. Jamii inataka kujua hatma ya huyo mnayesema alitaka kupindua serikali.

Cha kushangaza msivyo na akili, alipoenda kwenye kesi ile nyingine ya mali za CHADEMA, mkampa ulinzi wa kawaida. Hapo inaonyesha huyo mtu siyo hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…