Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amekemea vikali wimbi la utekaji na kupotea kwa watu nchini wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa mpakani wa Sirari, wilayani Tarime mkoani Mara.
Akihutubia mamia ya wananchi waliofika katika mkutano wa hadhara Sirari, Agosti 6, Heche alihoji mantiki ya serikali kujinasibu kwa miradi ya maendeleo kama ujenzi wa barabara, hospitali, na miradi ya maji wakati raia wanaotegemewa kutumia huduma hizo wanapotea au kutekwa.
Alisisitiza kuwa kila kitu duniani kipo kwa ajili ya binadamu, hivyo ni vigumu kuelewa ununuzi wa ‘Ambulance’ au ujenzi wa hospitali ikiwa binadamu hawapo, akisema kuwa hospitali haziwezi kujengwa kwa ajili ya mbwa bali kwa watu.
Soma pia: Heche: CHADEMA haitafanya maridhiano na CCM bila mpatanishi wa kimataifa
Pia alieleza hitaji la chama hicho la kuwa na msuluhishi wa kimataifa atakayekuja nchini kusimamia utatuzi wa matatizo ya kisiasa. Amesema msuluhishi huyo atasaidia kupitia nyaraka mbalimbali ili kuhakikisha watu wote waliohusika na matendo ya kuua na kuteka watu wanawajibishwa kwa mujibu wa sharia.