PreGE2025 POTOSHI Heche akiri CHADEMA imepangaranyika na kupasuka, Wanachama 3000 wakimbia Chama

PreGE2025 POTOSHI Heche akiri CHADEMA imepangaranyika na kupasuka, Wanachama 3000 wakimbia Chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Screenshot 2025-05-26 091616.png
 
Tunachokijua
John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho aliyeko mahabusu akituhumiwa kwa kesi ya uhaini na uchochezi ambapo kesi yake inatarajiwa kuendelea tarehe 02 Juni, 2025.

Mwezi Mei 23, 2025 Heche aliongoza kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kujadili mambo mbalimbali, ambapo moja ya ajenda zilizoainishwa kujadiliwa na kikao hicho ni pamoja na hali ya Kisiasa Nchini, oparesheni ya 'No Reform No Election' (Bila Mabadiliko Hakutakuwa na Uchaguzi) pamoja na uvunjani wa Haki za Binadamu na Ukandamizaji wa demokrasia nchini.

Katika mtandao wa TikTok, Mtumiaji mmoja kwa jina la 'Mapinduzi 64' alichapisha kipande cha video kinachomuonesha Heche akikiri kuwa CHADEMA imeparaganyika, imepasuka na kwamba wameondoka watu elfu tatu (3,000).


Je, ni upi uhalisia wa kipande hicho cha video?

Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) pamoja na marejeo ya video ya mkutano huo, JamiiCheck imejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwa kukata vipande na kuviunganisha, kitendo kilichoharibu ujumbe halisi.

Katika kikao Hicho, Heche hakutoa kauli yoyote iliyoonesha kukiri kwamba CHADEMA imeparaganyika ama kupasuka bali alikanusha madai hayo na kwamba chamba hicho bado kipo imara na kinaendelea kufanya kazi.

Sehemu ya hotuba ya Heche, Iliyohusisha sehemu ya video hiyo iliyopotoshwa Heche alisema,

"Kumekuwepo na kelele kutaka kuonesha dunia kwamba CHADEMA imeparaganyika, imepasuka, CHADEMA haipo, na waandishi wanachukua, wanaandika kwenye magazeti, mimi nimekuwa kwenye uongozi kwa muda mrefu kidogo, najua habari ambazo ziko pushed na serikali na zinapelekwa na zinaandikwa vilevile.

Haiwezekani unakuta gazeti moja limeandika taarifa inayofanana na nyingine na nyingine. Kwa mfano Watu wanasema CHADEMA inaparaganyika, Nataka nitumie nafasi hii na mfanye utafiti kabla hamjaandika.

Cha kwanza CHADEMA ni kina nani? ni kamati kuu hii hapa, kati ya wajumbe wote wa kamati kuu ameondoka mjumbe mmoja ambaye ni asilimia mbili kati ya wajumbe wote, baraza kuu lina wajumbe 456 kati ya walioondoka kwa sababu zinazoeleweka wameondoka wajumbe 20, mkutano mkuu wetu una wajumbe 1,400 kati ya hao walioondoka ni 34.

Chama kipo imara, kimetulia na kinachapa kazi walioondoka tunawatakia safari njema. Na waandishi muwape watanzania ukweli uliopo.

Ni maajabu kusema kwamba wameondoka watu 3000, hao watu wenyewe walipoenda ukumbi hauchukui hata watu 400, mnawalisha watanzania hivi vitu kwa sababu gani. Chombo cha habari kinaandika kwamba wameondoka watu 3000, sasa hawa watu wamekaa wapi? ni jambo la ajabu na la kusikitisha."


Rejea kiunganishi cha video nzima hapa

View: https://www.youtube.com/live/1-31t9-HSUM?si=X7XBlYx10tZL7B8A&t=1531​
Back
Top Bottom