John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Kupitia makamu mwenyekiti wake
John Heche, CHADEMA Novemba 19, 2025 ilitoa
msimamo wake kuhusu tume iliyoandaliwa kuchunguza “matukio ya uvunjifu wa amani” baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.
Ikumbukwe kuwa Novemba 18, 2025 Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka alitoa
taarifa kwa umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliunda Tume ya kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.
Madai
Kutokana na mkutano wa Heche na waandishi wa habari kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikitumia utambulisho wa Jambo TV kuwa Heche amesema 'serikali imetuhakikishia mchakato wa katiba mpya, utaanza muda wowote kuanzia sasa'
Uhalisia
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia marejeo ya video umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli, ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani Kauli hiyo haikutolewa kabisa na kiongozi huyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Novemba 19, 2025.
Vilevile grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachapishwa katika kurasa rasmi za
Jambo TV.