- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Madai
Kumekuwapo na gafiki inayosambazwa mtandaoni ikitumia tambulisho wa Jambo TV ikiwa na kichwa cha habari kinachosomeka "Tupo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na serikali"
Je, ni upi uhalisia wa grafiki hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha taarifa inayomnukuu John Heche kuhusu kauli hiyo.
Aidha kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Jambo TV haijachapisha taarifa hiyo bali wapotoshaji wametumia utambulisho huo kusambaza taarifa isiyo ya kweli.