DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, amesema kuwa chama hicho kinaungana na msimamo wa Askofu Josephat Gwajima, juu ya kupinga masuala ya utekaji ambayo ymekuwa yakiripotiwa nchini.
Heche ameongeza kuwa kutokana na msimamo huo wanapinga pia kitendo cha Serikali kulifungia kanisa la Askofu huyo mara baada ya kuzungumzia masuala ya utekaji.
================================
Hatua hii ya kulifungia kanisa lote nchi nzima ni batili maana inawakosesha fursa waumini wa kanisa hilo kumuabudu Mungu wao. Alichokisema Askofu Gwajima na kupelekea serikali kuchukua hatua za kulifuta kanisa, ni ukweli mtupu kuwa suala la utekaji na uwepo wa magenge ya uhalifu ndani ya mfumo wa vyombo vya ulinzi na usalama linahatarisha amani ya Taifa letu na lazima likomeshwe.
Serikali na vyombo vya dola lazima viwajibike na sio kuzima kelele na vilio vya watanzania ambao ndugu na rafiki zao wanapotezwa na kuuwawa.
Hivyo tunaiambia serikali, ilifungulie kanisa la Glory of Christ haraka ili kuwapa fursa ya waumini wa kanisa hili kufanya ibada kwa uhuru.
Tunawasihi pia viongozi wote wa dini watoke hadharani kukemea vitendo hivi vya utekaji kwa sababu wanao tekwa ni waumini wa dini mbalimbali.
Video: The Chanzo