PostGE2025 Heche awatembelea Niffer na Chavala gerezani Segerea kuwatia Moyo. Aishutumu Serikali ya CCM kwa kubambikizia watu kesi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Bara, John Heche amewatembelea jana Novemba 29, 2025 kijana Mika Chavala na Niffer gerezani Segerea. Lengo la ziara hiyo, amesema, lilikuwa kuwapa moyo na kuwahakikishia kwamba hawako peke yao katika vita wanavyopitia.

Heche pia aliwatumia ujumbe wa matumaini, akisema Watanzania wapo pamoja nao na wanawaombea katika hali hiyo ngumu. Hata hivyo, alibainisha kuwa serikali, aliyoiita dhalimu, ya CCM, ilikataa kuwaachia wafuate na kuwapokea gerezani.

Aidha, Heche alitoa wito kwa serikali hiyo kuwaachie watu wote waliobambikiziwa kesi za uongo za uhaini na ugaidi Nchi nzima. Alisisitiza kuwa serikali inayobambikizia watu kesi haifai kuheshimiwa wala kubaki madarakani.

“Watu huongozwa kwa ushawishi, sio kwa kuwatia hofu. Hakuna kitisho kitakachoturudisha nyuma,” alisema Heche.


​
 
Sas hawa vijana wana kosa gani jamani?
 
Ukishitakiwa kwa uhaini wanakuwa wameshakupa tiketi ya kuwa mtu unayeheshimika katika jamii. Muhimu ni kukaza ukiwa ndani huko. Usibreak wala usikubali wakuingize uwe kibaraka wao.

Siku ukitoka utakuwa na heshima kuliko viongozi wengi wa serikali. Tulia, jipange ili ujue utatumiaje hizo nguvu zako mpya.
 
Kwahy hao wawili wanafanya kazi na wana-usalama wakiwa gerezani?
Eeh,wanausalama wanakamua info toka kwao,wanaenda field kuhakiki,huyo niffer alijuaje kuna mask za kuzuwia bomu la machozi?..aliambiwa na nani?..alileta ngapi toka wapi?
 
Ndiyo,wanahojiwa kufukua kamtandao ka uhaini,kazi wanayo hao madogo
Ona zezeta hili hao watoto wana mtandao gani kwa mfano,
Yaani makosa ya Vilaza wa CCM mnaenda kuwabambikia watoto wadogo wasio na chochote katika maamuzu are you dung?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…