PostGE2025 Heche awatembelea Niffer na Chavala gerezani Segerea kuwatia Moyo. Aishutumu Serikali ya CCM kwa kubambikizia watu kesi

PostGE2025 Heche awatembelea Niffer na Chavala gerezani Segerea kuwatia Moyo. Aishutumu Serikali ya CCM kwa kubambikizia watu kesi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ona zezeta hili hao watoto wana mtandao gani kwa mfano,
Yaani makosa ya Vilaza wa CCM mnaenda kuwabambikia watoto wadogo wasio na chochote katika maamuzu are you dung?
Niffer alijuaje kuna mask za kuzuwia bomu la machozi?.. aliagiza ngapi toka wapi?..hicho kitendo siyo kuunga mkono harakati za kuvuruga uchaguzi na kupindua serikali?
 
Niffer alijuaje kuna mask za kuzuwia bomu la machozi?.. aliagiza ngapi toka wapi?..hicho kitendo siyo kuunga mkono harakati za kuvuruga uchaguzi na kupindua serikali?
Ndio maana nasema huko Lumumba kumejaza matahira kama wewe na inasikitisha sana kudeal na vitu pet pet kama urojo,huyo binti kusema anauza barakoa ilikua kama utani wa huko TikTok kwanza hakuna mtu mwenye akili timamu alijua wabongo wangeandama,sad story hali ikawa kweli kwa ujinga wa MaCCM
Leo mnakamata watoto eti wanachochea maandamano upuuzi wa serikali yako kupuuzia mambo leo unahara pumba hapa!
 
Hii ndio sababu kubwa maridhiano hayawezi kufanyika na serikali ya samia.Wale ambao ni sauti ya wananchi mnawauwa, mnawateka, mnawatishia na kuwabambikizia kesi.Masikio yao hayana uwezo wa kusikiliza ukweli.So insecured and triggered by the truth.Wanasema tuongelee amani, wakati tukiongea ukweli unaondoa amani yao wanaanza kupanic.Nothing will be built without the truth.
 
Tuko na CCM mpaka waharibu amani ya nchi hii kabisa
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Bara, John Heche amewatembelea jana Novemba 29, 2025 kijana Mika Chavala na Niffer gerezani Segerea. Lengo la ziara hiyo, amesema, lilikuwa kuwapa moyo na kuwahakikishia kwamba hawako peke yao katika vita wanavyopitia.

Heche pia aliwatumia ujumbe wa matumaini, akisema Watanzania wapo pamoja nao na wanawaombea katika hali hiyo ngumu. Hata hivyo, alibainisha kuwa serikali, aliyoiita dhalimu, ya CCM, ilikataa kuwaachia wafuate na kuwapokea gerezani.

Aidha, Heche alitoa wito kwa serikali hiyo kuwaachie watu wote waliobambikiziwa kesi za uongo za uhaini na ugaidi Nchi nzima. Alisisitiza kuwa serikali inayobambikizia watu kesi haifai kuheshimiwa wala kubaki madarakani.

“Watu huongozwa kwa ushawishi, sio kwa kuwatia hofu. Hakuna kitisho kitakachoturudisha nyuma,” alisema Heche.


HAKUNA KULIPA KODI KWA SERIKALI HARAMU
 
Aliyesema wakipoteza watu bs polisi wasihangaike kuwatafuta kwan ni wao wamewapoteza yupo ktaa anauza sura, pili aliyesema watakata watu vichwa yupo ktaa kapewa onyo eti aliyecheza wimbo manyonyo ule wa nywi nywi nywi yupo jera eti ni muhaini aahaaaha salamaleko TANGANYIKA.
 
Back
Top Bottom