The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Wakuu
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA John Heche ameeleza kwanini wanaona ajenda ya No refoms No election ni muhimu kwa sasa. Anaanza kwa kuhoji,
1. Je, tunachokipigania ni cha kweli kwenye ajenda ya No Reforms No election? Ni kweli, Uchaguzi wa nchi hii unaibiwa? Ni kweli unaibiwa,
2. Je, watu wanauawa kwenye uchaguzi? Ni kweli watu wanauawa, kwenye uchaguzi wa nchi hii watu wanauawa ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa ambako watu wawili wameuawa Tunduma wameuawa na Manyoni? Nyumbani kwake mgombea wa CHADEMA amepigwa risasi na polisi na mpaka sasa hakuna aliyewajibishwa
3. Je, mawakala wetu wanakuwa mistreated, wanatolewa kwenye vituo, hawapewi nafasi za kusimamia matokeo, wakurugenzi ndo wanaamua nani awe wakala nani asiwe na wakala? Ni kweli
4. Je, wagombea wetu wanakatwa majina kwa kuondolewa? Ni kweli, na uthibitisho mwingine ni kwamba Waziri wa Tamisemi alisema wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwamba wameondoa wagombea wa upinzani elfu 26 na hakuna mgombea wa CCM hata mmoja aliyeondolewa kwa kutokujua kusoma na kuandika.
Na miongoni mwa mambo ya kijinga yaliyowahi kutokea katika nchi hii ni kwamba wakili Deogratius Mahinyila, wakili wa mahakama kuu ameondolewa akigombea kijiji cha Berege kwamba hajui kusoma na kuandika, lakini mgombea wa CCM darasa la nne anajua kusoma na kuandika kuliko wakili?
Mambo yote haya tunayopigania, ni ya kweli, tufanyeje?, tukubaliane na siasa za ulaghai za kuambwia tugawiwe majimbo kwa hiyo tuingie kwenye uchaguzi kwa kugawiwa majimbo na sio kupiga kura? au tusimamie msimamo wa wananchi kwa kuhakikisha hii nchi inaondolewa kwenye mikono ya mafisadi kwa kura za wananchi?,
Msimamo wa chama chetu ni kusimama na msimamo wa wananchi na kukataa siasa za ulaghai, tumekataa siasa za ulaghai