GE2025 Heche: Magari waliyopewa wagombea wengine wa Urais kufanyia Kampeni ni dalili ya Rushwa

GE2025 Heche: Magari waliyopewa wagombea wengine wa Urais kufanyia Kampeni ni dalili ya Rushwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Ameandika Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche kupitia ukurasa wake wa Instagram "Magari waliyopewa vyama vya mfukoni kufanyia kampeini ni rushwa.. Lengo ni kujaribu kuhalalisha uchafu huu unaoitwa uchaguzi. Bajeti ya serikali inapitishwa na bunge, Tume waseme wametoa hizo fedha wapi? Ni fungu gani la bajeti lilitengwa kununulia vyama vya mfukoni magari, kulipia madereva na gharama nyingine zote. Ni wajibu wa kila chama kugharamia kampeini zake, sio wajibu wa tume kugharamia kampeini za mtu fulani kwa pesa ya umma. Huu ni uchafu mwingine mkubwa na wakati muafaka watu watatakiwa kujibu.

Watu hawana maji, madawa wala barabara kwa haraka haraka magari 17 kwa kwa sh milioni 500 ni zaidi ya bilioni 8.5 hivi ni vituo 17 kwa kata 17 katika nchi. Miradi ya maji inayosumbua na wilaya ikapata maji ya uhakika mingi ni chini ya bilioni 1.5. Mwanza ziwani hakuna maji unaambiwa matenki madogo, mradi huo unahitaji pesa kidogo zaidi ya hizo watu wapate uhakika wa maji.

Barabara za lami za kawaida ni milioni 500, ina maana ni KM 17 za barabara za mitaa ukiweka pale Mwanza karibia kila mtaa utapata lami.. Kwenye barabara kubwa ina maana ni bilioni 1 kwa km moja hizo ni km 8.5 za lami kwenye barabara kuu."

1757667758545.png
 
Write your reply...
Heche nyoko..mura wewe na huyu mtani wetu mmekipasua chama halafu unaleta unyoko hapa..
Hv baada ya tarehe 29, hayo manoo noo yataendelea kuimbwa?
 
Ndio maana anatakiwa kusimamia NRNE kwa vitendo wakati huu mwenyekiti yupo ndani akipambania uhuru wake.

Vinginevyo itakuwa sawa na kilio cha samaki baharini au ziwani.
 
Nasisi wananchi tupewe hayo mavi8 jamaniiii mboba yanatolewa kwa kubaguana??
 
Hiyo ni rushwa kamili, na hakuna upinzani hapo, subirini muone kura watakazopata vikaragosi hao mtacheka mpaka basi
 
Naunga mkono hoja
Chadema hawashiriki uchaguzi ila mambo ya wanaoshiriki yanawawasha.

Ni kama Samia mwanzoni alivyokuwa anawaongela Chadema wakati Cdm hawapo kwenye hizo mbanga zao.
 
TAKUKURU wangekuwa wanajielewa wangeanzia hapa
 
Back
Top Bottom