Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche ameeleza kuwa chama hicho kinaandaa barua ambazo zimepangwa kupelekwa kwa mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwamo Amnesty International, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya (EU), pamoja na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu, lengo ni kuijulisha dunia kuwa kuna wanachama wao 51 ambao wameshtakiwa kwa kesi za ugaidi, na kama kuna msaada wowote wa kisheria.