Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo Dkt Magufuli alimtafuta waziri Jaffo kwenye simu lakini hakupatikana na kuamua kumtafuta katibu mkuu na mazungumzo yao yalikuwa hivi.
MAGUFULI: Katibu mkuu hujambo?
NYAMHANGA: Sijambo, shikamoo mheshimiwa Rais
MAGUFULI: Marahaba, habari yako injinia Nyamhanga
NYAMHANGA: Salama mheshimiwa Rais, hongera kwa kampeni
MAGUFULI: Nilikuwa namtafuta waziri wako, waziri Jaffo naona hapatikani kwenye simu.
NYAMHANGA: Atakuwa kwenye kampeni huko Kisarawe.
MAGUFULI: Sasa natoa maagizo hapa, leo niko Hedaru, nimekuta kuna kituo cha afya hapa kina wodi ya kulaza wakinamama na akina baba, hakina wodi ya kufanyia operesheni, hakuna maeneo ya kuhifadhi maiti lakini hakuna X-Ray na vitu vingine.
Nimetoa maagizo mlete Tshs milioni 100(Wananchi shangwe). Na hiyo mjulishe huyo waziri wako, milioni 100 zije hapa Hedaru mfanye ukarabati na kuongeza majengo yote ya wodi ili wana Hedaru operesheni ziwe zinafanyika hapa.
NYAMHANGA: Sawa mheshimiwa Rais
MAGUFULI: Umenielewa katibu mkuu
NYAMHANGA: Nimekuelewa mheshimiwa Rais
============
MAGUFULULI: Ndugu zangu mimi nimemaliza ahadi niliyoitoa, nimeitoa jua linawaka na hii hospitali itakapokamilika nitakuja kushughulikia lakini sera nyingine ya maji na nini nayo tunaendelea kuyashughulikia, nawashukuru sana Mungu awajaalie. Wangapi mtanipa kura lakini?

MWISHO WA MAONGEZI