Uchaguzi 2020 Hedaru: Dkt. Magufuli amuagiza katibu mkuu TAMISEMI apeleke milioni 100 kukarabati kituo cha afya

Uchaguzi 2020 Hedaru: Dkt. Magufuli amuagiza katibu mkuu TAMISEMI apeleke milioni 100 kukarabati kituo cha afya

Hii nchi ina tatizo kubwa sana la kiutawala na kifedha.

Kwahiyo huyo magufuli anataka kusema kwamba leo asingefika hapo hiyo hospitali ingeendelea milele kutokuwa na mashine ya X RAY na sehemu ya kuhifadhia maiti?

Huu ujinga hauwezi kuisadia nchi tunajidanganya wenyewe.

Nchi lazima iwe na mifumo ya kifedha na kitaasisi kujiendesha yenyewe bila kutegemea hisani za magufuli.

Na hii haitawezekana kama fedha zote ziko miguuni kwa magufuli.

Rais tunaomba choo, Rais tunaomba kisima, Rais tunaomba sijui nini.

Tunajidanganya wenyewe, hatumdanganyi yeyote.
 
Huyu Rais ni kiaxi kwerikweri! It's already TOO LATE to catch the Airplane!!!!
Huu si wakti wa kutoa maagizo ya kiwendawazimu kupitia simu!! Miaka 5 alikuwa wapi kupeleka hizo Milioni 100 za Ukarabati?
Magufuli aache cheap politics!!!
Kweli kabisaa mkuu anabaka demokrasia nchini ni kwa kuwa yy yuko juu ya sharia ngoja tutamuonyesha kuwa hatumtaki kweny kura tar 28 sio mbali dunia itashangaa mbona watu tunamachungu moyoni tutayaotoa kweny kura [emoji35][emoji35][emoji35]
 
Leo Dkt Magufuli alimtafuta waziri Jaffo kwenye simu lakini hakupatikana na kuamua kumtafuta katibu mkuu na mazungumzo yao yalikuwa hivi.

MAGUFULI: Katibu mkuu hujambo?

NYAMHANGA: Sijambo, shikamoo mheshimiwa Rais

MAGUFULI: Marahaba, habari yako injinia Nyamhanga

NYAMHANGA: Salama mheshimiwa Rais, hongera kwa kampeni

MAGUFULI: Nilikuwa namtafuta waziri wako, waziri Jaffo naona hapatikani kwenye simu.

NYAMHANGA: Atakuwa kwenye kampeni huko Kisarawe.

MAGUFULI: Sasa natoa maagizo hapa, leo niko Hedaru, nimekuta kuna kituo cha afya hapa kina wodi ya kulaza wakinamama na akina baba, hakina wodi ya kufanyia operesheni, hakuna maeneo ya kuhifadhi maiti lakini hakuna X-Ray na vitu vingine.

Nimetoa maagizo mlete Tshs milioni 100(Wananchi shangwe). Na hiyo mjulishe huyo waziri wako, milioni 100 zije hapa Hedaru mfanye ukarabati na kuongeza majengo yote ya wodi ili wana Hedaru operesheni ziwe zinafanyika hapa.

NYAMHANGA: Sawa mheshimiwa Rais

MAGUFULI: Umenielewa katibu mkuu

NYAMHANGA: Nimekuelewa mheshimiwa Rais

MWISHO WA MAONGEZI

============

MAGUFULULI: Ndugu zangu mimi nimemaliza ahadi niliyoitoa, nimeitoa jua linawaka na hii hospitali itakapokamilika nitakuja kushughulikia lakini sera nyingine ya maji na nini nayo tunaendelea kuyashughulikia, nawashukuru sana Mungu awajaalie. Wangapi mtanipa kura lakini?
Tumesema hadi atatambaa kwa tumbo mwaka huu, kupiga magoti haitoshi
 
Leo Dkt Magufuli alimtafuta waziri Jaffo kwenye simu lakini hakupatikana na kuamua kumtafuta katibu mkuu na mazungumzo yao yalikuwa hivi.

MAGUFULI: Katibu mkuu hujambo?

NYAMHANGA: Sijambo, shikamoo mheshimiwa Rais

MAGUFULI: Marahaba, habari yako injinia Nyamhanga

NYAMHANGA: Salama mheshimiwa Rais, hongera kwa kampeni

MAGUFULI: Nilikuwa namtafuta waziri wako, waziri Jaffo naona hapatikani kwenye simu.

NYAMHANGA: Atakuwa kwenye kampeni huko Kisarawe.

MAGUFULI: Sasa natoa maagizo hapa, leo niko Hedaru, nimekuta kuna kituo cha afya hapa kina wodi ya kulaza wakinamama na akina baba, hakina wodi ya kufanyia operesheni, hakuna maeneo ya kuhifadhi maiti lakini hakuna X-Ray na vitu vingine.

Nimetoa maagizo mlete Tshs milioni 100(Wananchi shangwe). Na hiyo mjulishe huyo waziri wako, milioni 100 zije hapa Hedaru mfanye ukarabati na kuongeza majengo yote ya wodi ili wana Hedaru operesheni ziwe zinafanyika hapa.

NYAMHANGA: Sawa mheshimiwa Rais

MAGUFULI: Umenielewa katibu mkuu

NYAMHANGA:
Nimekuelewa mheshimiwa Rais

MWISHO WA MAONGEZI

============

MAGUFULULI: Ndugu zangu mimi nimemaliza ahadi niliyoitoa, nimeitoa jua linawaka na hii hospitali itakapokamilika nitakuja kushughulikia lakini sera nyingine ya maji na nini nayo tunaendelea kuyashughulikia, nawashukuru sana Mungu awajaalie. Wangapi mtanipa kura lakini?
 
Kwa kweli miluzi mingi humpoteza mbwa ,kwa hiyo sekta ya utalii inachochewa na miundo mbinu ipi?

Ndege ni uwekezaji wa kibiashara kama zilivyo biashara zingine ambazo hata wewe ungefanya mfano kuliko kupokea mshahara wa mwezi kununua chakula na malazi ukautumia kuwekeza kununua shamba hivi kweli shamba linaweza kuwa halina faida kwa familia yako iwe sasa au baadae? JPM ilani imemtaka kuboresha shirika la ndege unadhani angeboreshaje na alikuta ndege 1 mbovu.

Hivi unataka kusema viwanda vya Dar vinatunufaisha vipi sisi tuliopo Chongoleani Tanga na Dhahabu iliyo Geita ina manufaa gani kwa watu ,jibu nijepesi miradi yote ya Serikali sio mali ya mtu binafsi bali ni ya Umma hizo pesa zote zinaenda kwenye kapu moja ndilo ambalo linasaidia miradi ya ujenzi Zahati na barabara.

Hivi hujui mradi wa Ziwa victoria kwenda Tabora umefikia wapi,na ule mradi wa Arusha mabilioni unayajua ni mangapi na huku Miradi mingi ya Dar ikiwa ni Trillion of money leo unapiga kelele ndege ambazo ni uhuduma ya kuchochea sekta zingine kukua pia kama Utalii na Usafirishaji.

Nahisi wewe utakuwa umekula age haya sio mawazo ya kijana wa kisasa maana teknolojia inaenda kasi sana sio vibaya na sisi kwenda kama dunia inavyoenda kuwa Bullet train ,Ndege majengo ya kisasa kwenhe miji yetu n.k ,nadhani umeona kwa wenzetu train zao zinavyowakera kwa sababu ya mawazo machache ya washamba kama wewe kwa dunia ya sasa huwezi kuponda ununuaji wa Ndege.

Nchi za wenzetu umeme sio tatizo lakini utakuta mtu yupo village ana mashamba yake kapiga Panel za solar hakuna shida kabisa ila hapa ni malalamiko mnawekewa Bwawa la umeme mnarudisha kelele za tungeanza gesi .

Nimenyoosha mikono Tanzania bila Magufuli tukapata wanaoyumbishwa maendeleo tutayasikia kwingine.
*Magufuli 5 tena*
Hizo ndege zimeenda Nchi zipi prime zinazoleta watalii wengi hapa Nchini?

Sent from my TA-1024 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom