Uchaguzi 2020 Hedaru: Dkt. Magufuli amuagiza katibu mkuu TAMISEMI apeleke milioni 100 kukarabati kituo cha afya

Uchaguzi 2020 Hedaru: Dkt. Magufuli amuagiza katibu mkuu TAMISEMI apeleke milioni 100 kukarabati kituo cha afya

Kashinda tayari - wafanyakazi (ganzi), wakulima (ganzi), wafugaji (ganzi), wafanyabiashara (ganzi) - Tanzanian community ganzi.

28 tunashinda
 
Kashinda tayari - wafanyakazi (ganzi), wakulima (ganzi), wafugaji (ganzi), wafanyabiashara (ganzi) - Tanzanian community ganzi.

28 tunashinda

Kunyamazisha watu ndo kitu pekee naweza kumpongeza, kama ni kitu kizuri.
 
Magufuli asingelazimisha kununua midege isiyokuwa na faida yoyote kwetu malalamiko haya yasingekuwepo.h

Katika miaka mitano ijayo Magufuli amepanga kutumia billion 490 kununua ndege mpya toka kwa mabeberu.

Sasa hebu jiulize billion 490 zinaweza kukamilisha miradi mingapi ya maendeleo hapa nchini? kwanini wanalazimisha kununua ndege kama hakuna upigaji?
Nyumba walizojengewa Rais Kikwete na Mzee Mwinyi zina thamani zaidi ya milioni 100

Hivi kuna sababu ya wananchi kulala wodi moja, halafu serikali ijenge jengo zima kwa mtu mmoja tena mwenye nyumba na mshahara mnono!

Ile nyumba ya Kikwete au Mwinyi ni '' kituo cha afya tosha'' leo kumbe kuna watu wanalala wanaume na wanawake pamoja. Maelfu wanateseka tunajali watu 2 waliotosheka.
 
Milioni 100 ikamalizie majengo, ijenge sehemu ya kuhifadhia maiti, Ikanunue Xray si ndio baadae utakuja kumtumbua mtu useme amejenga chini ya kiwango na kununua mashine mbovu!

Let us be serious guys!

Haya maigizo yataisha lini!

Takukuru!

Hata wewe ukishikwa kende utaahidi chochote ili kujinasua, huyu Mzee kashikwa pabaya.
 
Marefa hawawezi kuamua maana bosi ndio anawalipa mshahara! Na yeye ndio kacheza rafu saa hizi
 
Ikiwa umeongea vitu vingi vya msingi lakini ukaishia kutetea ununuzi wa ndege nakuona usiyekuwa na mantiki na hicho ulichoongea
Lazima ukubali kwamba yamefanyika makosa katika ununuzi wa ndege na bwana mkubwa bado anashupaza shingo wakati yeye mwenyewe naamini anatambua kwamba amekosea katika hili

Huwezi ukatumia mamia ya mabilion kununua ndege bila kuwa na plani ya kutengeneza faidi kutokana na hiyo pesa uliyowekeza hapo
Kupitia pesa hiyo ingefaa kutatua matatizo mengi kabisa ya watanzania maskini ambapo matokeo yangekuwa ni makubwa Sana kiasi cha Tanzania kuonekana tumepiga hatua katika jambo fulani

Ndege zetu zinasemwa kwamba haziendi huko nje wanakotoka watalii sasa zinaongezaje utalii


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Nilifikiri na niliamini yale mapumziko, walikuwa wanamfunda mgombea wao, asivunje kanuni kwa makusudi, very sad!

Alichobakisha sasa, ni kutoa minoti hadharani, na kugawia wananchi, COZ hiki anachofanya ni rushwa tu kama za kubrashia viatu!

Aibuuuuuuu! NEC joka la kibisa! Tungeuona UHURU wa tume, kama japo wangelikemea hili hadharani!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Milioni mia moja (100,000,000/=) ni Rushwa hapo Hedaru.

TAKUKURU, NEC, POLISI, JWTZ, TIS, Magereza, Mahakama,Taasisi za kidini, Jumuia ya Kimataifa, wananchi na Magambo chukueni hatua.

Lissu peleka malalamiko Tume ya Uchaguzi ili kamati ya maadili ya uchaguzi imfungie siku 14.
 
Hii nchi ina tatizo kubwa sana la kiutawala na kifedha.

Kwahiyo huyo magufuli anataka kusema kwamba leo asingefika hapo hiyo hospitali ingeendelea milele kutokuwa na mashine ya X RAY na sehemu ya kuhifadhia maiti?

Huu ujinga hauwezi kuisadia nchi tunajidanganya wenyewe.

Nchi lazima iwe na mifumo ya kifedha na kitaasisi kujiendesha yenyewe bila kutegemea hisani za magufuli.

Na hii haitawezekana kama fedha zote ziko miguuni kwa magufuli.

Rais tunaomba choo, Rais tunaomba kisima, Rais tunaomba sijui nini.

Tunajidanganya wenyewe, hatumdanganyi yeyote.

Rais huyu amegeuka kuwa mungumtu lazima kila mtu aombe pesa toka kwake ndiyo ampe!!!
Yeye ndo hazina,yeye ndo Chief Treasurer, yeye ndo Waziri wa Fedha na yeye ndo Gavana wa BOT......!!!!!
 
It's already TOO LATE to catch the Airplane!

Huu si wakati wa kutoa maagizo ya kiwendawazimu kupitia simu!! Miaka 5 alikuwa wapi kupeleka hizo Milioni 100 za Ukarabati?
Magufuli aache cheap politics!
Amechelewa.
 
NEC mpo? Magufuli amevunja wazi kabisa Sheria ya uchaguzi. Mtamfanya nini? Kamati yenu ya Maadili Ipo wapi?
 
Back
Top Bottom