Uchaguzi 2020 Hedaru: Dkt. Magufuli amuagiza katibu mkuu TAMISEMI apeleke milioni 100 kukarabati kituo cha afya

Uchaguzi 2020 Hedaru: Dkt. Magufuli amuagiza katibu mkuu TAMISEMI apeleke milioni 100 kukarabati kituo cha afya

Magufuli asingelazimisha kununua midege isiyokuwa na faida yoyote kwetu malalamiko haya yasingekuwepo.h

Katika miaka mitano ijayo Magufuli amepanga kutumia billion 490 kununua ndege mpya toka kwa mabeberu.

Sasa hebu jiulize billion 490 zinaweza kukamilisha miradi mingapi ya maendeleo hapa nchini? kwanini wanalazimisha kununua ndege kama hakuna upigaji?
Utakuta watu kama nyie kodi hamlipi ila mnataka kodi ziwanufaishe nyie.
Kama hupandi ndege ni wewe
 
Ahadi kama hizi zinapotolewa kwenye kampeni ni rushwa,tume ya uchaguzi ya ccm ndiyo hivyo tena.

Mbwa hamng'ati mmiliki wake.

Fedha zinatoka bila utaratibu,Makofuli ndiye rais,bunge na mahakama...uongozi wa hivyo kwelikweli
 
Hizo ndege zimeenda Nchi zipi prime zinazoleta watalii wengi hapa Nchini?

Sent from my TA-1024 using JamiiForums mobile app
Dah asee kweli upinzani upo ,yani ununue ndege leo then kesho zianze safari unadhani hizo ni sawa na Hice ,usafiri wa anga unataratibu zake nadhani utakuwa shahidi kuna mikoa hata hizo ndege za ATCL zilikuwa hazifiki ila sasa zinafika na usiseme tu kuwa zinaenda wapi utakuwa ni muongo.
Hizo ndege zinaenda India na baadae China,kwa sasa zinaenda soko la bara hili la Afrika kama South Africa ,Entebe,Comoro ,Kenya kwani hizo nchi zipo bongo .
Unadhani ndege hizo zinatosha kwenda ulaya na Marekani ndio mana zinatakiwa walau kubwa kubwa ziwe hata Sita unataka twende bila Stategic Planning kama vile mlevi kaona Barmed hii ni biashara ya kimataifa mzee haihitaji kukurupuka utaharibu soko lako unatikwa ukianza hakuna kufaulisha ni mwendo wa hii inapaa hii inatua Wazungu hawapendi Kucancell route kisa ndege imechelewa.
Tulia mambo yanakuja mazuri Bullet Train kutoka Korea zinafanana na kichwa cha ndege mbona mwaka huu mtakonda.
 
Pamoja na umuhimu wa mradi lakini timing ya kutoa hela inaashiria rushwa ya dhahiri kabisa. Ila Vibogoyo TAKUKURU hawatafanya lolote
 
Leo Dkt Magufuli alimtafuta waziri Jaffo kwenye simu lakini hakupatikana na kuamua kumtafuta katibu mkuu na mazungumzo yao yalikuwa hivi.

MAGUFULI: Katibu mkuu hujambo?

NYAMHANGA: Sijambo, shikamoo mheshimiwa Rais

MAGUFULI: Marahaba, habari yako injinia Nyamhanga

NYAMHANGA: Salama mheshimiwa Rais, hongera kwa kampeni

MAGUFULI: Nilikuwa namtafuta waziri wako, waziri Jaffo naona hapatikani kwenye simu.

NYAMHANGA: Atakuwa kwenye kampeni huko Kisarawe.

MAGUFULI: Sasa natoa maagizo hapa, leo niko Hedaru, nimekuta kuna kituo cha afya hapa kina wodi ya kulaza wakinamama na akina baba, hakina wodi ya kufanyia operesheni, hakuna maeneo ya kuhifadhi maiti lakini hakuna X-Ray na vitu vingine.

Nimetoa maagizo mlete Tshs milioni 100(Wananchi shangwe). Na hiyo mjulishe huyo waziri wako, milioni 100 zije hapa Hedaru mfanye ukarabati na kuongeza majengo yote ya wodi ili wana Hedaru operesheni ziwe zinafanyika hapa.

NYAMHANGA: Sawa mheshimiwa Rais

MAGUFULI: Umenielewa katibu mkuu

NYAMHANGA:
Nimekuelewa mheshimiwa Rais

MWISHO WA MAONGEZI

============

MAGUFULULI: Ndugu zangu mimi nimemaliza ahadi niliyoitoa, nimeitoa jua linawaka na hii hospitali itakapokamilika nitakuja kushughulikia lakini sera nyingine ya maji na nini nayo tunaendelea kuyashughulikia, nawashukuru sana Mungu awajaalie. Wangapi mtanipa kura lakini?
Hii ni rushwa ktk uchaguzi, na si mara moja katoa. Hajakemewa hata mara moja. Ingekuwa ni hoja ya kwa nini hazijaletwa wakati zilipangwa, si kosa. Kitabu kinacho andikwa rafu za Magufuli kwenye kampeni, cha kwanza kimejaa na kufungwa.
 
Magufuli asingelazimisha kununua midege isiyokuwa na faida yoyote kwetu malalamiko haya yasingekuwepo.h

Katika miaka mitano ijayo Magufuli amepanga kutumia billion 490 kununua ndege mpya toka kwa mabeberu.

Sasa hebu jiulize billion 490 zinaweza kukamilisha miradi mingapi ya maendeleo hapa nchini? kwanini wanalazimisha kununua ndege kama hakuna upigaji?
Akili fupi unashindwa kuelewa kwamba hizo 490 B ndani ya miaka miwili zinaweza kusababisha 1Trilioni? Kupitia ndege tunaweza kupata watalii ambao watalipa tozo za utalii, watalipa nauli ya ndege, hoteli zitafanya biashara na kutoa kodi. Achilia mbali ajira kwa tour guide, ajira kwa wafanyakazi wa ndege ajira kwenye hoteli.
Akili za nyumba zinaangalia leo haziangalii kesho na kesho kutwa.
Magufuli tumemwelewa sana mitano mingine inamhusu.


Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli asingelazimisha kununua midege isiyokuwa na faida yoyote kwetu malalamiko haya yasingekuwepo.h

Katika miaka mitano ijayo Magufuli amepanga kutumia billion 490 kununua ndege mpya toka kwa mabeberu.

Sasa hebu jiulize billion 490 zinaweza kukamilisha miradi mingapi ya maendeleo hapa nchini? kwanini wanalazimisha kununua ndege kama hakuna upigaji?
Huku mikoani kwa mpango wa 'force account's darasa moja linajengwa kwa sh 7m. Hiyo 490b ni madarasa 70e! Itapunguza sana uhaba wa madarasa.
 
Hovyo kabisa....
IMG_20201020_161500_327.jpg

IMG_20201020_161535_520.jpg
IMG_20201020_161600_472.jpg

IMG_20201020_161634_543.jpg

Huyu ndio hovyo mara 1000.Hamna hata aibu kuhadaa watanzania.
 
Bunge limeidhinisha lini na wapi
Mkulu unachanganya mambo
Hizi ni dakika za kuzungumza haya kweli mbona hujifunzi?!
Toeni hiyo millioni 100 mzitafune
Kwani in five yrs hukujua hakuna kituo cha Afya
Hizi ahadi zipo tangu 1949 bado tu
 
Sheria,kanuni na taratibu wazitunge na kuzipitisha kibabe wenyewe lakini hawawezi kuzifuata. Hii ni rushwa par se.
 
Hivi ukiacha Mahera, huyu mwenyekiti wa hiyo tume mbona hasikiki hata kukohoa?
 
Hii ni rushwa ya wazi wazi lakini NEC hawalioni hili, ukiangalia suala la Kituo cha Afya Hedaru ni la muda mrefu idadi ya watu iliyopo na uwezo kituo haviendani, inatakiwa pajengwe kituo kingine cha afya viwe viwili kuhusu mochwari ni lazima watu wanapeleka maiti Same bonde lote la Hedaru na viunga vyake.

Pamoja na changamoto zilizopo Hedaru haihalalishi dhambi ya kutoa hii rushwa ili apewe kura tena, Changamoto za Hedaru ni za miaka yote alikuwa wapi huyu mzee.

Alikuwepo mwenyekiti wa kijiji kupitia CHADEMA alifanya makubwa sana mkuu wa wilaya na viongozi wa CCM wakafanya figisu wakamtoa kwa nguvu.

Anachodhihirisha Magufuli kwa watu ni mzembe wa kuona matatizo ya jamii, mtoa rushwa mkubwa na mwenye uchu wa madaraka hafai tena
28/10 pigachini mtu
 
Milioni 100 ikamalizie majengo, ijenge sehemu ya kuhifadhia maiti, Ikanunue Xray si ndio baadae utakuja kumtumbua mtu useme amejenga chini ya kiwango na kununua mashine mbovu!

Let us be serious guys!

Haya maigizo yataisha lini!

Takukuru!
 
Back
Top Bottom