Uchaguzi 2020 Hedaru: Dkt. Magufuli amuagiza katibu mkuu TAMISEMI apeleke milioni 100 kukarabati kituo cha afya

Uchaguzi 2020 Hedaru: Dkt. Magufuli amuagiza katibu mkuu TAMISEMI apeleke milioni 100 kukarabati kituo cha afya

Utakuta watu kama nyie kodi hamlipi ila mnataka kodi ziwanufaishe nyie.
Kama hupandi ndege ni wewe
Mlumumba darasa la nne failure, mwalimu wako hajakufundisha kuwa kila mtanzania analipa kodi? Hata yule mtoto mwenye sh.mia anayeenda kununua peremende dukani?
 
Ndio maana matokeo ya urais hawataki yahojiwe mahakamani. Hii ni rushwa ya wazi kabisa. Alifanya hivi akiwa waziri wa ujenzi kwenye uchaguzi mdogo Igunga, aliahidi daraja la mto Mbutu kwenye kampeni; mwisho wake uchaguzi ulifutwa ule baada ya kupelekwa mahakamani.
 
Ndio muwaeleweshe wananchi wa Hedaru sasa kuwa wakifanya makosa miaka 5 mingine ya mseto inakuja. Hiyo mil 100 kwa maboresho aliyoyasema ni ndogo sana na hayatafanyika kabla ya uchaguzi, akishinda tena mjue hali itaendelea ile ile na mkiuliza mtajibiwa kwa kebehi.
 
Hiyo million 100 ipo kwenye bajeti? Anapoitoa kwenye kampeni ni RUSHWA. Katika jamii iliyostaarabika mamlaka husika ingemuondoa ktk uchaguzi kwa kosa la kutoa rushwa
 
Wananchi wa Hedaru msidanganywe na pipi kama watoto.Kwa vile anaomba kura ndio anaamuru hiyo pesa iletwe. Hamjawahi kumuona kabla ya hapo na hamtamuona (ikiwa atashinda) kwa miaka mitano ijayo. Tunataka UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU. Chagua CHADEMA tupate UHURU HAKI NA MAENDELEO YA WATU. Rais wetu ni Lissu.
 
Hiyo milioni 100 ni rushwa. TAKUKURU ng'ataaa
Na NEC hawata kemea hili. Watakaa kimya. Subiri Lissu ampe mama mjane elfu kumi ya kumnunulia mtoto daftari.. Mhhh hata mashetani watasikia.
 
Kwa kweli miluzi mingi humpoteza mbwa ,kwa hiyo sekta ya utalii inachochewa na miundo mbinu ipi?

Ndege ni uwekezaji wa kibiashara kama zilivyo biashara zingine ambazo hata wewe ungefanya mfano kuliko kupokea mshahara wa mwezi kununua chakula na malazi ukautumia kuwekeza kununua shamba hivi kweli shamba linaweza kuwa halina faida kwa familia yako iwe sasa au baadae? JPM ilani imemtaka kuboresha shirika la ndege unadhani angeboreshaje na alikuta ndege 1 mbovu.

Hivi unataka kusema viwanda vya Dar vinatunufaisha vipi sisi tuliopo Chongoleani Tanga na Dhahabu iliyo Geita ina manufaa gani kwa watu ,jibu nijepesi miradi yote ya Serikali sio mali ya mtu binafsi bali ni ya Umma hizo pesa zote zinaenda kwenye kapu moja ndilo ambalo linasaidia miradi ya ujenzi Zahati na barabara.

Hivi hujui mradi wa Ziwa victoria kwenda Tabora umefikia wapi,na ule mradi wa Arusha mabilioni unayajua ni mangapi na huku Miradi mingi ya Dar ikiwa ni Trillion of money leo unapiga kelele ndege ambazo ni uhuduma ya kuchochea sekta zingine kukua pia kama Utalii na Usafirishaji.

Nahisi wewe utakuwa umekula age haya sio mawazo ya kijana wa kisasa maana teknolojia inaenda kasi sana sio vibaya na sisi kwenda kama dunia inavyoenda kuwa Bullet train ,Ndege majengo ya kisasa kwenhe miji yetu n.k ,nadhani umeona kwa wenzetu train zao zinavyowakera kwa sababu ya mawazo machache ya washamba kama wewe kwa dunia ya sasa huwezi kuponda ununuaji wa Ndege.

Nchi za wenzetu umeme sio tatizo lakini utakuta mtu yupo village ana mashamba yake kapiga Panel za solar hakuna shida kabisa ila hapa ni malalamiko mnawekewa Bwawa la umeme mnarudisha kelele za tungeanza gesi .

Nimenyoosha mikono Tanzania bila Magufuli tukapata wanaoyumbishwa maendeleo tutayasikia kwingine.
*Magufuli 5 tena*

Matunda_kuniga
Umejitahidi sana kumfagilia Jiwe ili apate 5 tena. Uko sahihi kwa upande huo wa nzi wa KIJANI lakini kwa uhalisia tu ni kwamba WATANZANIA WANATAKA MAENDELEO YAO NA SIYO YA VITU!!!
Kama wewe Ni mfuatiliaji wa speech za Baba wa Taifa utakubaliana naye kuwa MAENDELEO YA VITU LAZIMA YA AKISI(REFLECT) MAENDELEO YA WATU.
Huwezi kukomaa na kujenga FLYOVERS, interchange, SGR, STIEGLERS GORGE, etc wakti WANANCHI WANAZIDI KUWA NA HALI NGUMU YA KUMAISHA!

Lakini pia iwe Ni maendeleo ya Watu au Vitu LAZIMA MAENDELEO HAYO YAWE katika MAZINGIRA YA UHURU NA AMANI.
Magufuli hwezi kujisifu kuwaletea maendeleo Watz huku akiminya UHURU na DEMOKRASIA ya Watz haohao!!

Tatizo la Magufuli ni kunyanyasa, kutesa na hata kupoteza maisha ya wale wanao onekana KUPINGANA AU KUTOFAUTIANA NAYE KIMAWAZO NA KIMTAZAMO.
Huo Kama sio Udikteta Ni kitu gani?
Watanzania siyo wajinga Kama MAGUFULI na CCM yake wanavofikiri....!
Mitano(5) inayofuata sasa apewe Mhe. LISSU ambaye ameonesha kubadilisha upepo wa Kisiasa Tanzania katika Uchaguzi huu wa 2020.
 
Unadhani wengine hawakuwa na kofia mbili, au kofia mbili zimeanza 2015. Busara katika uongozi ni kitu cha msingi sana, jambo ambalo huyu limbukeni wa chato hana.
Hata Jakaya na wengine walifanya hivi,sema ulikuwa hufuatilii siasa.
 
Kwa kweli miluzi mingi humpoteza mbwa ,kwa hiyo sekta ya utalii inachochewa na miundo mbinu ipi?

Ndege ni uwekezaji wa kibiashara kama zilivyo biashara zingine ambazo hata wewe ungefanya mfano kuliko kupokea mshahara wa mwezi kununua chakula na malazi ukautumia kuwekeza kununua shamba hivi kweli shamba linaweza kuwa halina faida kwa familia yako iwe sasa au baadae? JPM ilani imemtaka kuboresha shirika la ndege unadhani angeboreshaje na alikuta ndege 1 mbovu.

Hivi unataka kusema viwanda vya Dar vinatunufaisha vipi sisi tuliopo Chongoleani Tanga na Dhahabu iliyo Geita ina manufaa gani kwa watu ,jibu nijepesi miradi yote ya Serikali sio mali ya mtu binafsi bali ni ya Umma hizo pesa zote zinaenda kwenye kapu moja ndilo ambalo linasaidia miradi ya ujenzi Zahati na barabara.

Hivi hujui mradi wa Ziwa victoria kwenda Tabora umefikia wapi,na ule mradi wa Arusha mabilioni unayajua ni mangapi na huku Miradi mingi ya Dar ikiwa ni Trillion of money leo unapiga kelele ndege ambazo ni uhuduma ya kuchochea sekta zingine kukua pia kama Utalii na Usafirishaji.

Nahisi wewe utakuwa umekula age haya sio mawazo ya kijana wa kisasa maana teknolojia inaenda kasi sana sio vibaya na sisi kwenda kama dunia inavyoenda kuwa Bullet train ,Ndege majengo ya kisasa kwenhe miji yetu n.k ,nadhani umeona kwa wenzetu train zao zinavyowakera kwa sababu ya mawazo machache ya washamba kama wewe kwa dunia ya sasa huwezi kuponda ununuaji wa Ndege.

Nchi za wenzetu umeme sio tatizo lakini utakuta mtu yupo village ana mashamba yake kapiga Panel za solar hakuna shida kabisa ila hapa ni malalamiko mnawekewa Bwawa la umeme mnarudisha kelele za tungeanza gesi .

Nimenyoosha mikono Tanzania bila Magufuli tukapata wanaoyumbishwa maendeleo tutayasikia kwingine.
*Magufuli 5 tena*
Ndugu umeongea sana nmekuelewa hivi kosa la nchi kukosa ndege ni la nani maana tangu mm nazaliwa cjawahiona chama kingine kinakuwa madarakank tofauti na ccm?
Hivi Kama sekta ya ndege ilikuwa na upungufu wa kuwa na ndege moja na hatimae shirika la ndege kudhoofika kwa maana hiyo ni lazma utawala wako wote ujikite kwenye ununuzi wa ndege tu hakuna vitu vingine vya kusimamia Kama mkuu wa nchi na vikaendelea kuinufaisha nchi zaidi na ikabakia kwa awamu ya rais mwingine kuangalia hiyo sekta kwa jicho la pekee?
Hivi ni sahihi rais kuongea mbele za watu kuwa mlikosea kuchagua mngechagua ccm ndo maana cjaleta maendeleo? Hii ni sera ya madiwani na wabunge c kwa rais kusema mbele za watu ebu tujiulize ni chama gani kpo madarakani ni cmm hafu unaongea habari zile kweli? Hivi hakuna sehemu ambako Kuna ccm lkn hamna maendeleo mifano ni mingi mno

Hii nchi ni ya watanzania c ya rais peke yake yy tumempatia kuwa mcmamizi tu kama unavyojua kuwa hakuna muunganiko wa pamoja bila kuwepo kiongozi.

Hizo pesa unazosema nchi imeingiza Kuna wananchi wanafaidikaje nazo likiwa Kama pato la mwananchi kwa nchi yake?

Hivi kipimo cha uchumi wa kati kimetumikaje mpaka kugudua nchi ipo ktk uchumi wa kati? Nmeuliza hivyo huku mm naona deni la nchi limeongezeka hafu vile vile wananchi hawajafaidi na nchi yenye uchumi wa kati kuliko awamu zote zilizowahi pita ktk utawala wa nchi na uchumi ulikuwa chini lkn hali ya maisha ilikuwa vzr, ajira zinapatikana huduma za jamii znapatikana kulingana na uhitaji

Kwenye afya hamna madawa takwimu hazitolewi kwa usahihi hii ni nchi gani na ukitoa takwimu kosa hivi hii nchi ni ya nani Kama hina haki ya kuhoji na kuuliza?

Elimu hazina walimu, hamna madawati hamna vitabu baadhi ya shule tena zilizo nyingi hamna maji walimu wanaishi mazingira mabovu hatari nk
Kilimo: baadhi ya bidhaa na vitendea kazi kwenye kilimo viko ghari muda huo saiv watu wanategemea kilimo hawana hela majembe bei juu mbegu bei juu hivi tunaenda wapi hafu tunaanza kudanganyana watu wanahama wànapewa hela na mada ya kuzungumza ili tu tuendelee kuwa watumwa hapana viongozi ifikie wakati tuangalie na tabaka la chini linakatishwa tamaa na maisha cjaona nini maana ya rais wa wanyonge ktk kioindi chote cha miaka mitano
 
Chadema wasichoke kupeleka malalamiko Yao NEC Ili kuweka Kumbukumbu Vizuri. Mana NEC watasema hawafanyii kazi malalamiko ambayo hayajawasilishwa kwao.
 
Lpp
Leo Dkt Magufuli alimtafuta waziri Jaffo kwenye simu lakini hakupatikana na kuamua kumtafuta katibu mkuu na mazungumzo yao yalikuwa hivi.

MAGUFULI: Katibu mkuu hujambo?

NYAMHANGA: Sijambo, shikamoo mheshimiwa Rais

MAGUFULI: Marahaba, habari yako injinia Nyamhanga

NYAMHANGA: Salama mheshimiwa Rais, hongera kwa kampeni

MAGUFULI: Nilikuwa namtafuta waziri wako, waziri Jaffo naona hapatikani kwenye simu.

NYAMHANGA: Atakuwa kwenye kampeni huko Kisarawe.

MAGUFULI: Sasa natoa maagizo hapa, leo niko Hedaru, nimekuta kuna kituo cha afya hapa kina wodi ya kulaza wakinamama na akina baba, hakina wodi ya kufanyia operesheni, hakuna maeneo ya kuhifadhi maiti lakini hakuna X-Ray na vitu vingine.

Nimetoa maagizo mlete Tshs milioni 100(Wananchi shangwe). Na hiyo mjulishe huyo waziri wako, milioni 100 zije hapa Hedaru mfanye ukarabati na kuongeza majengo yote ya wodi ili wana Hedaru operesheni ziwe zinafanyika hapa.

NYAMHANGA: Sawa mheshimiwa Rais

MAGUFULI: Umenielewa katibu mkuu

NYAMHANGA:
Nimekuelewa mheshimiwa Rais

MWISHO WA MAONGEZI

============

MAGUFULULI: Ndugu zangu mimi nimemaliza ahadi niliyoitoa, nimeitoa jua linawaka na hii hospitali itakapokamilika nitakuja kushughulikia lakini sera nyingine ya maji na nini nayo tunaendelea kuyashughulikia, nawashukuru sana Mungu awajaalie. Wangapi mtanipa kura lakini?
Jamaa keshapoteana, yupo sooo desperate now. Wakati anatoa rushwa Tanga kule alikopita mwanzo wameshamkataa na Lissu Bado anashindilia mispana. Tutaona mengi Siku hizi 6 zilizobaki.
 
Back
Top Bottom