Hekaheka Uzeeni

Hekaheka Uzeeni

Mkuu, usisubiri hadi ustaafu.

Kama hujaoa bado tembelea sasa. Lakini angalizo usiwe na papara maana kule ni kama restaurant, unaweza kuagiza chakula lakini kila ukigeuza shingo kuagalia walivyo agiza wenzako naona ndo vizuri.

Hivyo chukua muda kusoma 'menu'.
JBourne59 Ushauri mjarabu sana huu. Much respect bro. Kazi nzuri
Heka heka yako ni ya kipekee, walikufundisha kilimo cha umwagiliaji kwa njia za kisasa. Ukawaozesha baada ya kufanikiwa.
 
MSIMU WA PILI
Season II

Hekaheka
Uzeeni

(i). Ugomvi, Suluhu, Faida.

Ilikuwa siku ya alhamisi mchana Hamida alipokuja kunipokea Ubungo bus terminal. Nikiwa mwenye furaha ya kumuona mke wangu lakini yeye alikuwa amenuna njia nzima tulipokuwa tunaelekea Kariakoo kumsindikiza Bosio hoteli ambayo aliambiwa na wakala wake afikie. Aliendesha Nadia yake kwa kasi ingawaje foleni za hapa na pale zilikuwa zinamzuia asikimbie kwa muda mrefu.

“Atafikia Sleep inn hotel ya Kariakoo…” nilisema wakati mwendo wa gari ulikuwa umekolea baada ya kupita taa za mtaa wa Msimbazi na Morogoro rd.

Ni kwa bahati tu taa nyekundu zilituzuia kuendelea lakini dalili za kulala na speed zote niliziona. Baada ya taa kuruhusu alikunja kuingia barabara ya Lumumba, njia ilikuwa na magari mengi hivyo hakuweza kulipelekesha gari.

“Ingia mtaa wa Mahiwa..” nilimuelekeza Hamida.

Mbele kidogo jirani kabisa na mtaa wa ‘jiwe linaloishi’ akapaki na Bosio akashuka na kushukuru kwa lifti.

“Merci Papaa pulabalade…” Alisema akimaanisha anashukuru kwa lift.

Nikafunga mlango na kurudi kwenye siti yangu na kufunga mlango na mkanda, mara nikasikia..

“Mercii ya nyoko!”

Nikamwangalia wife kisha nikatikisa kichwa na kukaa kimya. Safari iliendelea hadi tulipofika nyumbani tukiwa kama mabubu maana niliamua nijizuie kusema lolote. Nyumbani nikashusha mizigo vizuri na begi langu yeye akiwa bado amenuna na kuelekea jikoni.

Uzuri wa Hamida ni kwamba, hata kama amenuna huduma zingine zote anakupatia vizuri tu, hivyo sikuwa na wasiwasi wa kunyimwa huduma za nyumbani.

Baada ya kuoga kuliko nichukuwa muda mrefu, nikajiandaa na kuelekea sehemu ya maakuli ambako nilikuta ameniandalia chakula changu pendwa kama kawaida. Nikakaa chini ‘mkekani’ na kuanza kula peke yangu.

Baada ya chakula nikapitia mitandao ya kijamii kidogo kisha nikaenda kijilaza chumbani. Saa kumi na mbili kasoro hivi niliamshwa kwa voice call ya whatsapp kutoka kwa Janeth.

“Du hekeheka uzeeni hizi…”, nilijisemea.

“Halo, habari, ulifika salama?” ilikuwa sauti ya Janeth akiongea.

Nilimjibu na kuongea naye mawili matatu, mara Hamida akaingia na kukaa jirani huku akisikiliza. Ila nyie wanawake, Mungu anawaona. Muda wote mko na hisia hisia tu. ‘Anyway’ (siyo ‘anyways’), ndivyo jinsi mlivyoumbwa.

“Hii simu ni kutoka nje ya nchi, ni familia iliyonifadhili kule Kigali wakati wa ‘lockdown’ wanataka kujuwa kama nilifika salama…” nilijitetea baada ya kukata simu.

“Enhe, hebu niambie, yule mwanamke tuliye mshusha kule hotelini ni nani!” aliuliza Hamida kwa hamaki.

Ikanichukuwa muda mrefu kumuelezea kuanzia pale mpakani Gatuna jinsi tulivyokutana na safari yetu hadi tulivyofika na kwamba hakuna kinachoendelea. Baada ya majibizano ya muda mrefu hatimaye alikubali kushuka chini na kuomba afungue mizigo yangu akague. Ila wanawake! Nimewavulia kofia.

Akajifanya anatenganisha nguo chafu na safi na kuziweka sehemu zake, akakung’uta begi kuhakikisha hakuna kitu kilichobaki kisha akahamia kwenye mzigo mwingine ambao ndani kulikuwa na vitenge vyake.

Kwenye ule mzigo, vile vitenge vya dola 50 hamsini niliviweka juu na vile vya dola 80 themanini niliviweka chini. Sasa alivyoanza kufungua ule mzigo akaanza kusasambua na kuvirusha kitandani…

“Hivi si ni sawa tu na vya Kitumbini! Wala hakuna tofauti yoyote..” alikuwa aking’aka kama vile bado ana kitu rohoni.

Mara paap akavifikia vile wax orijino! Nikaona tu anatabasamu na kusema…

“Hivi sasa ndio vitenge…”

Aliendelea kuvichambua vyote na kuishia kusema vizuri sana, ahsante! Akanikumbatia pale kisha akaviweka vizuri.
===

Usiku ule ulikuwa murua kwani nilifanya zoezi la kilimo cha umwagiliaji na kufanikiwa kama wafanyavyo wakulima wa Kinyarwanda lakini nilibandikwa maswali ambapo majibu yake ndiyo yaliyoleta ugomvi na kusameheana baadaye.

Ni kwamba Hamida alikuwa anamfahamu Janeth na familia yao kwakuwa tulikuwa tunawasiliana kwa ‘video call’ na alikuwa ameongea na watu wote ndani ya ile nyumba (Kigali), lakini hakuwa amedhani kwamba nimechepuka na mmoja wao hadi aliponibana kwenye kilimo cha umwagiliaji.

Ilikuwa ni ulimaji tofauti na aliouzoea, tulio uzoea!, ingawaje hata kabla ‘kilimo kwa kumwagilia’ kilikuwa kunafanyika. Sasa hii ‘pro max’ aliona ni tofauti sana na kunibana nimueleze nilipojifunzia. Nikaamua kusema ukweli kuwa Janeth alinifundisha. Mama yangu! Kilichofuata hakiandikiki.

Lakini mwisho wa yote vile vitenge vilimpooza na kumwambia vile vya ziada yeye aamue nani ampe na nani asimpe lakini kali kuliko yote alitaka tena kumwagilia bustani.

Baada ya kuridhika kuwa bustani imelowana maji vya kutosha akatulia na kusema…

“…lakini tamu…” Nimekusamehe, lakini utanipeleka ‘shopping’ ninapopataka mimi kama fidia.

Kusikia hivyo mzee mzima nikataka sasa nipeleke moto ile kibongobongo lakini mjamaa kichwa wazi ‘akazila’ kabla hata moto haujakolea, nikajikuta tu nasema hii sasa ni hekaheka uzeeni. Ilibidi kuahirisha zoezi na kupisha mwili na akili vikae sawa hadi kulivyokucha asubuhi.

ITAENDELEA...
,Nakadori my
 
Mkuu JBourne59 kilichobaki tunaomba darasa la kilimo cha umwagiliaji maana Ni muhimu sana ,ni changamoto sana kutegemea mvua
Pitieni uzi huu

Japo wengi wanasema zitafutwe fedha, maji yatapatikana tu...

Lakini someni utangulizi wake vizuri.

Muhimu: Hakikisha juhudi za kumwagilia shamba liwe lako kihalali.

Sintohusika na matumizi mabaya katika elimu niliyotoa.

 
Pitieni uzi huu

Japo wengi wanasema zitafutwe fedha, maji yatapatikana tu...

Lakini someni utangulizi wake vizuri.

Muhimu: Hakikisha juhudi za kumwagilia shamba liwe lako kihalali.

Sintohusika na matumizi mabaya katika elimu niliyotoa.

Barikiwa sana mkuu
 
Analyse Half american IamBrianLeeSnr KatKit Johnnie Walker Antonnia baby zu Dejane Numbisa Watching

Hii imeisha pitieni story za huyu mzee ziko bomba sana na nimwandishi mzuri sana. .

Mngeanzia huku kwanza hamtijutia
 
Yeah mwamba yuko poa sana!
Kuna ile yake ya Hamida niliianza sijaimaliza!
Ile story alishamaliza. Fanya uimalize uandishi yuko vizuri sana havlboi kabisa
 
Ile story alishamaliza. Fanya uimalize uandishi yuko vizuri sana havlboi kabisa
Shukrani sana mkuu ngoja niipitie
 
Analyse Half american IamBrianLeeSnr KatKit Johnnie Walker Antonnia baby zu Dejane Numbisa Watching

Hii imeisha pitieni story za huyu mzee ziko bomba sana na nimwandishi mzuri sana. .

Mngeanzia huku kwanza hamtijutia
Pamoja sana.. Gily ingawa hii nilisha pita nayo...Barikiwa sana.
 
Analyse Half american IamBrianLeeSnr KatKit Johnnie Walker Antonnia baby zu Dejane Numbisa Watching

Hii imeisha pitieni story za huyu mzee ziko bomba sana na nimwandishi mzuri sana. .

Mngeanzia huku kwanza hamtijutia
Nitarud baadae mkuu shukrani
 
Analyse Half american IamBrianLeeSnr KatKit Johnnie Walker Antonnia baby zu Dejane Numbisa Watching

Hii imeisha pitieni story za huyu mzee ziko bomba sana na nimwandishi mzuri sana. .

Mngeanzia huku kwanza hamtijutia
Duh sawa nikiwa na mda nitapitia zote kwa amri yako
 
Nilikuwa nataka nijifunze nini wasomaji wa JF wanapenda

Nimegundua kuwa hawapendi stori ndefu

Pia nimegunduwa huwa wana enjoy eposode 1 kila wiki labda

Pia nadhani huwa wanapenda sogozi baina ya episode na episode

Season II tutaenda sawa.
Yaani ungefanya episodes ndio ungeambulia matusi zaidi. Simulizi yako kali na inafunza,na ulivyoamua kutususia yote mpk imeisha imekuwa vzr sana. Sehemu nyingi ulizozitaja nimekaa/nazijua hivyo kunipaa ladha ya kipekee sana,imenikumbusha kukumbukumbu njema. Hongera
 
Yaani ungefanya episodes ndio ungeambulia matusi zaidi. Simulizi yako kali na inafunza,na ulivyoamua kutususia yote mpk imeisha imekuwa vzr sana. Sehemu nyingi ulizozitaja nimekaa/nazijua hivyo kunipaa ladha ya kipekee sana,imenikumbusha kukumbukumbu njema. Hongera
Huwa nafurahi sana nikipata mirejesho kama hii.
 
Huwa nafurahi sana nikipata mirejesho kama hii.
Pale kinampanda mission ulipofikia wakati unaenda middle school tabora...ndo nyumbani. Nimepata kipaimara pale usharika wa kkkt kinampanda...nimesoma Tumaini secondari...Nduguti...nkalakala.....gumanga.....msingi...kote nimepita..napafahamu. sikufika ibaga,chemchem na mkalama tu...japo babu yangu na bibi waliwahi kuwa walimu pale Mkalama primary. Pia babu yangu upande mwingine...ambaye kwa kabila alikua Mtaturu pure kama ww, Mr. Haama...aliwahi kuwa mwl pale Chemchem primary. Maeneo mengi ktk story yako ya Hamida..hasa kule singida nayajua...na hata ruti ya treni itigi tabora...nimeruka nayo mara kadhaa...nimeisoma story yote ya hamida kwa siku 2 tu...iliniteka...nilijihisi niko ndani ya stori. Vionjo vya lugha yangu...kinyiramba...ni moja ya vitu nimefurahia..." UYU MWELU PEE"....( sista ako akimwelezea mchumbako Hamida) Hahaaaaa...salute mkuu
 
Back
Top Bottom