Mamtolo
Senior Member
- Feb 27, 2018
- 186
- 208
Mukombi wa kiarabu....hahaaaa!Sister alifurahi kupata wifi 'Mwarabu'
"ale munanso muza naibii"
Atula mukombi na tende!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mukombi wa kiarabu....hahaaaa!Sister alifurahi kupata wifi 'Mwarabu'
"ale munanso muza naibii"
Atula mukombi na tende!
Wameshusha bus 7 mpya haoMzee kampuni ya utatu mtakatifu imerudi tena. Leo zimepita Bus mpyaa kadhaa hapa barabarani.View attachment 2546377
Kinyiramba hiki,duhSister alifurahi kupata wifi 'Mwarabu'
"ale munanso muza naibii"
Atula mukombi na tende!
Yes, mimi ni Mtaturu.Kinyiramba hiki,duh
Mkuu wewe wa Singapore!?
We mkuu Mungu anakuona eti Mercii ya nyoko !![emoji1787][emoji1787]Picha ni kwa hisani ya google, hazina uhusiano wa moja kwa moja na simulizi wala majina katika hizo picha si yenyewe.
Umemaliza kila kitu UVUMILIVU NA UTULIVU KWELI NI TUNDA LA KHERI(b) Zari la mentali
Hayo yalikuwa maelezo ya Papa Blaze ambaye alimuona Bosio kwenye moja ya hoteli alizokuwa akienda kujiburudisha akija Dar es Salaam na kumtokea ili aanzishe uhusiano. Bosio alivyolifikisha suala lake kwetu (mimi na Hamida) ndio tukafanya kikao naye ili tupate kumjuwa vizuri ndio akafunguka kama nilivyoeleza hapo juu kwa kifupi, maana alisimulia kwa kirefu sana. Sote tuliridhika kwa maelezo yake, tukafanya uchunguzi kiasi kutaka kujuwa ukweli wa aliyosema kuanzia mpaka wa Tunduma, Ubalozi wa DRC Dar es Salaam na na ubalozi wa Rwanda hapa Dar na tukaridhika kuwa amesema kweli.
Hamida akaongea na Bosio na kumweleza kuwa aliyo ongea Papa Blaze ni ya kweli na kwamba amepata mchumba aliyepitia hali ngumu hivyo wanaweza kujenga uhusiano ulio imara.
Taratibu za kufikisha barua ya posa Kishasa zikaendelea.
Aidha kwa upande wa Janeth alipitia kashkash kadhaa lakini wote baada ya uchunguzi ilionekana hawakidhi vigezo…
Kuna aliyejaribu kuligonga gari lake (gari yangu niliyompa atumie akiwa Dar) ili tu apate nafasi ya kubadilishana namba kisha kuwa karibu wakati wa matengenezo ya gari na hatimaye kutaka kuanzisha uhusiano…
Huyu kijana alikuwa ni mtoto wa mwanasiasa mkubwa nchini lakini baada ya uchunguzi ilionekana anajihusisha na magenge ya kihalifu, akapigwa chini.
Kuna Mchungaji ambaye alifiwa na mke miezi kadhaa iliyopita (wakati huo), akitokea kanisa lingine la dhehebu hilohilo, bila shaka alipata taarifa za uwepo wa Janeth kutoka kanisa analosali, lakini baada ya uchunguzi ilionekana amezalisha waumini wasiopungua wawili wa kanisa lake na afya yake pia ilikuwa ina mashaka, akapigwa chini.
Kuna waumini kadhaa wa kanisa alilokuwa akisali walijitokeza lakini wote hawakuionesha subira ama nia ya dhati ya kutaka kuoa bali kushiriki tendo tu, wengine eti Janeth ashike ujauzito kwanza kisha taratibu zingine zifuate, walipigwa chini.
Bahati ikaangukia kwa kijana Dikolu ambaye walikutana kule gereji ambako Alphard ilipelekwa kwa ajili ya kunyooshwa ilipogongwa na baladhuli yule, huyu kijana alikuwa na fundi makanika wa ile gereji (kapuni), ingawaje hakuhusika katika kulirudisha lile gari katika hali yake ya kawaida, lakini alionekana hapo akiendelea na kazi zake za kila siku. Dikolu alikuwa ni mrefu na aliyejazia misuli na kifua kama wafanya mazoezi ya viungo, nadhani ni kutokana na kazi za ufundi lakini bila shaka alikuwa ni mfanya mazoezi.
Dikolu alikuwa ni kijana mwenye umri usiozidi thelathini na miwili, ni mchaga aliyetokea eneo la Kishimundu na kuja Dar miaka kumi na tano iliypoita akitokea Moshi. Alikuja mara tu baada ya kufeli kidato cha pili na kufukuzwa nyumbani kwao, akaamua kuja Dar kujibanza kwa kaka yake ambaye alikuwa dereva wa daladala. Kwa vile alikuwa anapenda mambo ya ufundi magari, kaka yake aliona asipoteze hela kumsomesha sekondari bali alimpeleka gereji anapofanyia sevisi daladala lake ili aanzie hapo kujifunza mambo ya ufundi.
Baada ya mwaka mmoja kukaa gereji kaka yake aliamua ampeleke Chang’ombe veta ili apate mafunzo rasmi ya darasani. Alifaulu vizuri trade test grade III na kurudi pale gereji kuendeleza ufundi kwa vitendo ambapo akapata umaarufu sana kutokana na bidii ya kazi pamoja na kazi nzuri azifanyazo za kutengeneza magari. Baada ya mwaka mmoja mwingine wa kufanya kazi, yeye mwenyewe aliamua kurudi veta ili kusoma na kufanya trade test grade II ili aweze kuwa na ujuzi wenye uhakika na kutambulika zaidi. Kweli baada ya kurudi mtaani aliendelea na kazi lakini kaka yake akaona sasa mdogo wake amevuka daraja la kufanyia kazi ‘uchochoroni’ hivyo akamtafutia nafasi katika gereji kubwa maarufu ambako ndipo alipoonekana na Janeth.
Nilishangaa sana siku naangalia service card ya gari ya Janeth nikakuta ni ya gereji nyingine na siyo ile niliyozoea, kumbe ilipofika muda wa kufanyia sevisi gari alirudi pale gereji lilipo nyooshwa gari kwa ajili ya kazi ya sevisi ya kawaida ya gari.
===
Kufupisha stori ni kwamba, siku nyingine Janeth alimuomba fundi huyo aliendeshe gari na kuisikiliza maana ilikuwa inatoa mvumo sio wa kawaida. Ni kweli gari ilikuwa inahitajia kubadilishwa ‘wheel bearing’ za mbele, lakini pia Janeth alitumia nafasi hiyo kumtega Dikolu na Jamaa uvumilivu ukamshida wakajikuta wamebusiana.
Siku nyingine wakajitafutia nafasi wakazungumza wee ndipo sisi tukaletewa taarifa kuwa kuna kijana Dikolu ambaye anataka kuleta posa.
Baada ya uchunguzi tuligundua kuwa ni kweli Dikolu ni mzaliwa wa Kishimundu, lakini tayari walikuwa wameshayaweka sawa masuala ya kufukuzana nyumbani na wazazi kusema walikuwa wanampa akili kwa njia ya vitendo, kaka yake alikiri juu ya utulivu wa mdogo wake katika kazi na masuala mazima ya maisha, na Dikolu mwenyewe alisema hakujihusisha na masuala ya mapenzi lakini alikuwa mteja wa ‘ambiance’ siku mojamoja akizidiwa maana kwa mujibu wake alikuwa hapati ‘kichwa kuuma’ wala kuwa mtumwa wa kutoa pesa mara kwa mara kama angeanzisha uhusiano na alikuwa anajilinda vizuri na magonjwa yaambukizayo kwa njia ya kujamiiana.
Vipimo vikafanyika kwa wote inaonekana wapo salama, wakaendeleza uhusiano wao ili wazidi kufahamiana na baada ya miezi mitatu kupita Janeth alirudi tena na vipimo vikafanyika na wote wakawa salama. Taratibu za kupeleka posa Kigali zikabarikiwa.
===
Mzee mzima nikapata hekaheka ya ku-‘host’ kitu kilichoitwa ‘pre wedding ceremony ‘ ambapo Bosio na Janeth wote walikuwa ni ma bibi harusi watarajiwa, tuliwaalika wajomba wa Bosio na Baba zake wakubwa na wadogo, pia familia ya Janeth kutoka Kigali ilihudhuria na ndugu na marafiki wa familia za Dikolu na Papa Blaze walihudhuria na kufanya msisimko wa aina yake jijini sherehe iliyofanyika katika moja ya kumbi maarufu jijini Dar.
Baaya ya wiki chache kupita mimi na Hamida tukashiriki ndoa jijini Kigali, Bosio pia alikuja yeye pamoja na mtarajiwa wake na wiki mbili zilizofuata tukashuhudia sherehe matata jijini Kinshasa kwenye ndoa ya Bosio na Papaa Blaze ambapo pia Janeth na mumewe Dikolu walihudhuria.
===
Janeth na Bosio wote muda huu wana watoto wachanga chini ya mwaka mmoja. Urafiki wa Tanzania, Rwanda na Congo DR ‘ukaimarika’ kwa kuunganisha familia hizo, Bosio alihamishia makazi yake ya kudumu Mbezi Dar es Salaam kwa mumewe, watoto wakewakubwa waliendelea kubaki Kishasa kwa kuwa bado wapo wanasoma lakini huja wakati wa likizo kumsalimia mama yao, Janeth na Dikolu walinunua uwanja maeneo ya Kimara Dar es Salaam na ujenzi unaendelea, biashara ya duka kule Kigali amewachia wadogo zake na yeye amefungua 'boutique’ nyingine kubwa hapa Dar es Salaam na ameanza kuagiza mizigo ya dukani kwake na kwa wadogo zake moja kwa moja kutokea Uturudi na Thailand.
Furaha imetujaa moyoni kwa kufanikisha furaha za mabinti hawa wa Kigali na Congo DR. Hekaheka zitaongezeka nyumbani kwangu maana wajukuu wanazidi kuongezeka na ikifika msimu wa kushambulia mapera hekaheka za mchezo wa maliwato zitamkuta Hamida akiwasaidia wajukuu zake.
===
MWISHO.
Nimelazimika kuifupisha kwa sababu ya mabadiliko ya ghafla ya ratiba zangu.
Shukran sana mkuu ushauri mwanana sana huu ingawa Mimi sijaajiriwaUshauri Kwa watumishi / waajiriwa:-
Anza kustaafu ukiwa bado kazini.
Yaani jizoeshe maisha ya mtaani kana kwamba vile tayari umeshastaafu.
Anzisha mradi hata mdogo Kwa kukuingizia kipato japo kidogo.
Kuza huo mradi hadi uweze kukuendeshea maisha ya kawaida ya kila siku.
Ishi vizuri na mwenza wako sasa ili siku za usoni usijutie.
Kazini ulipoajiriwa fanya kazi Kwa bidii bila kutegea ili ari hiyo ihamie kwenye mradi (miradi yako)
Usimuonee mtu yoyote wala kumdharau yoyote kinyume chake tenda haki.
Furahia maisha muda wote na punguza "makasiriko"
Linda afya yako maana ni mtaji mzuri sana.
Kila la heri.
Benbulugu
Nimeuchukua.Ushauri Kwa watumishi / waajiriwa:-
Anza kustaafu ukiwa bado kazini.
Yaani jizoeshe maisha ya mtaani kana kwamba vile tayari umeshastaafu.
Anzisha mradi hata mdogo Kwa kukuingizia kipato japo kidogo.
Kuza huo mradi hadi uweze kukuendeshea maisha ya kawaida ya kila siku.
Ishi vizuri na mwenza wako sasa ili siku za usoni usijutie.
Kazini ulipoajiriwa fanya kazi Kwa bidii bila kutegea ili ari hiyo ihamie kwenye mradi (miradi yako)
Usimuonee mtu yoyote wala kumdharau yoyote kinyume chake tenda haki.
Furahia maisha muda wote na punguza "makasiriko"
Linda afya yako maana ni mtaji mzuri sana.
Kila la heri.
Benbulugu
Sasa ndio uandike kwa kukoza wino..!Usimuliaji una bore. Unataka kuchangamsha kwa kuweka weka maneno ambayo mwishowe yanaishia kuchosha msomaji. Na nimeshangaa sababu wewe umesema ni mstaafu sasa unaandikaje kama kijana wa miaka 20.utoto utoto mwingi na maneno meeeeeeengi yasiyo na tija. Ungesimulia tu bila kutaka kunogesha ingependeza sana.... Maneno kama kilimo cha umwagiliaji n.k ni useless hayana maana kwa mtu mzima ambaye unataka simulizi yako ionekane ni ya kweli.
Nilimjibu na kuongea naye mawili matatu, mara Hamida akaingia na kukaa jirani huku akisikiliza. Ila nyie wanawake, Mungu anawaona. Muda wote mko na hisia hisia tu. ‘Anyway’ (siyo ‘anyways’), ndivyo jinsi mlivyoumbwaMSIMU WA PILI
Season II
Hekaheka Uzeeni
(i). Ugomvi, Suluhu, Faida.
Ilikuwa siku ya alhamisi mchana Hamida alipokuja kunipokea Ubungo bus terminal. Nikiwa mwenye furaha ya kumuona mke wangu lakini yeye alikuwa amenuna njia nzima tulipokuwa tunaelekea Kariakoo kumsindikiza Bosio hoteli ambayo aliambiwa na wakala wake afikie. Aliendesha Nadia yake kwa kasi ingawaje foleni za hapa na pale zilikuwa zinamzuia asikimbie kwa muda mrefu.
“Atafikia Sleep inn hotel ya Kariakoo…” nilisema wakati mwendo wa gari ulikuwa umekolea baada ya kupita taa za mtaa wa Msimbazi na Morogoro rd.
Ni kwa bahati tu taa nyekundu zilituzuia kuendelea lakini dalili za kulala na speed zote niliziona. Baada ya taa kuruhusu alikunja kuingia barabara ya Lumumba, njia ilikuwa na magari mengi hivyo hakuweza kulipelekesha gari.
“Ingia mtaa wa Mahiwa..” nilimuelekeza Hamida.
Mbele kidogo jirani kabisa na mtaa wa ‘jiwe linaloishi’ akapaki na Bosio akashuka na kushukuru kwa lifti.
“Merci Papaa pulabalade…” Alisema akimaanisha anashukuru kwa lift.
Nikafunga mlango na kurudi kwenye siti yangu na kufunga mlango na mkanda, mara nikasikia..
“Mercii ya nyoko!”
Nikamwangalia wife kisha nikatikisa kichwa na kukaa kimya. Safari iliendelea hadi tulipofika nyumbani tukiwa kama mabubu maana niliamua nijizuie kusema lolote. Nyumbani nikashusha mizigo vizuri na begi langu yeye akiwa bado amenuna na kuelekea jikoni.
Uzuri wa Hamida ni kwamba, hata kama amenuna huduma zingine zote anakupatia vizuri tu, hivyo sikuwa na wasiwasi wa kunyimwa huduma za nyumbani.
Baada ya kuoga kuliko nichukuwa muda mrefu, nikajiandaa na kuelekea sehemu ya maakuli ambako nilikuta ameniandalia chakula changu pendwa kama kawaida. Nikakaa chini ‘mkekani’ na kuanza kula peke yangu.
Baada ya chakula nikapitia mitandao ya kijamii kidogo kisha nikaenda kijilaza chumbani. Saa kumi na mbili kasoro hivi niliamshwa kwa voice call ya whatsapp kutoka kwa Janeth.
“Du hekeheka uzeeni hizi…”, nilijisemea.
“Halo, habari, ulifika salama?” ilikuwa sauti ya Janeth akiongea.
Nilimjibu na kuongea naye mawili matatu, mara Hamida akaingia na kukaa jirani huku akisikiliza. Ila nyie wanawake, Mungu anawaona. Muda wote mko na hisia hisia tu. ‘Anyway’ (siyo ‘anyways’), ndivyo jinsi mlivyoumbwa.
“Hii simu ni kutoka nje ya nchi, ni familia iliyonifadhili kule Kigali wakati wa ‘lockdown’ wanataka kujuwa kama nilifika salama…” nilijitetea baada ya kukata simu.
“Enhe, hebu niambie, yule mwanamke tuliye mshusha kule hotelini ni nani!” aliuliza Hamida kwa hamaki.
Ikanichukuwa muda mrefu kumuelezea kuanzia pale mpakani Gatuna jinsi tulivyokutana na safari yetu hadi tulivyofika na kwamba hakuna kinachoendelea. Baada ya majibizano ya muda mrefu hatimaye alikubali kushuka chini na kuomba afungue mizigo yangu akague. Ila wanawake! Nimewavulia kofia.
Akajifanya anatenganisha nguo chafu na safi na kuziweka sehemu zake, akakung’uta begi kuhakikisha hakuna kitu kilichobaki kisha akahamia kwenye mzigo mwingine ambao ndani kulikuwa na vitenge vyake.
Kwenye ule mzigo, vile vitenge vya dola 50 hamsini niliviweka juu na vile vya dola 80 themanini niliviweka chini. Sasa alivyoanza kufungua ule mzigo akaanza kusasambua na kuvirusha kitandani…
“Hivi si ni sawa tu na vya Kitumbini! Wala hakuna tofauti yoyote..” alikuwa aking’aka kama vile bado ana kitu rohoni.
Mara paap akavifikia vile wax orijino! Nikaona tu anatabasamu na kusema…
“Hivi sasa ndio vitenge…”
Aliendelea kuvichambua vyote na kuishia kusema vizuri sana, ahsante! Akanikumbatia pale kisha akaviweka vizuri.
===
Usiku ule ulikuwa murua kwani nilifanya zoezi la kilimo cha umwagiliaji na kufanikiwa kama wafanyavyo wakulima wa Kinyarwanda lakini nilibandikwa maswali ambapo majibu yake ndiyo yaliyoleta ugomvi na kusameheana baadaye.
Ni kwamba Hamida alikuwa anamfahamu Janeth na familia yao kwakuwa tulikuwa tunawasiliana kwa ‘video call’ na alikuwa ameongea na watu wote ndani ya ile nyumba (Kigali), lakini hakuwa amedhani kwamba nimechepuka na mmoja wao hadi aliponibana kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Ilikuwa ni ulimaji tofauti na aliouzoea, tulio uzoea!, ingawaje hata kabla ‘kilimo kwa kumwagilia’ kilikuwa kunafanyika. Sasa hii ‘pro max’ aliona ni tofauti sana na kunibana nimueleze nilipojifunzia. Nikaamua kusema ukweli kuwa Janeth alinifundisha. Mama yangu! Kilichofuata hakiandikiki.
Lakini mwisho wa yote vile vitenge vilimpooza na kumwambia vile vya ziada yeye aamue nani ampe na nani asimpe lakini kali kuliko yote alitaka tena kumwagilia bustani.
Baada ya kuridhika kuwa bustani imelowana maji vya kutosha akatulia na kusema…
“…lakini tamu…” Nimekusamehe, lakini utanipeleka ‘shopping’ ninapopataka mimi kama fidia.
Kusikia hivyo mzee mzima nikataka sasa nipeleke moto ile kibongobongo lakini mjamaa kichwa wazi ‘akazila’ kabla hata moto haujakolea, nikajikuta tu nasema hii sasa ni hekaheka uzeeni. Ilibidi kuahirisha zoezi na kupisha mwili na akili vikae sawa hadi kulivyokucha asubuhi.
ITAENDELEA...
Macho yangu mabovu
Hata usihangaike nae. Mtu anajiita Chizi, unategemea ataongea cha maana?Kuongeza chumvi kidogo ama maji kiasi kwenye baadhi ya sehemu ni kwa ajili ya kuleta ladha aitakayo msimuliaji...
Msimuliaji hatarajii simulizi au aina ya usimuliaji imfurahishe kila mtu...
Wachache watakao furahia inatosha, anaye inaona 'inamboa' msimuliaji hana namna ya kumsaidia...
Narudia kusema kuwa ninyi vijana msidhani kuwa watu wazima hawajui lugha za vijana, tena watu wazima wenyewe waliohadhiri utandawazi na kitembea kwingi...
Msimuliaji anajuwa hadhira anayoisimulia, hivyo si vibaya akileta katika lugha ambayo hadhira hiyo itaielewa haraka na kufurahia...
JF ni moja ya sehemu ninapoondolea stress, acha tufurahie maisha Chizi Maarifa
Burudika na hiiHata usihangaike nae. Mtu anajiita Chizi, unategemea ataongea cha maana?
Anyway, it's been a while mzee. Dondosha kitu vijana tupate mawili matatu ya kujifunza!
Wanawake wana hisia kali sana. Kuna mambo wanaweza kuona ambayo sisi wanaume tusione kabisa!Nilimjibu na kuongea naye mawili matatu, mara Hamida akaingia na kukaa jirani huku akisikiliza. Ila nyie wanawake, Mungu anawaona. Muda wote mko na hisia hisia tu. ‘Anyway’ (siyo ‘anyways’), ndivyo jinsi mlivyoumbwa
Lakini si ulimchakata janeth mkuu..!!...ndio maana alipokuhisi alipita mle mle
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app