Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
- Thread starter
- #41
MTEGO WA PANYA HUINGIA WALIOKUWAMO NA WASIOKUWAMO
Palikuwa mtu na mkewe, Ndani ya nyumba yao walikuwamo panya wengi sana wakiharibu vitu, na kutoboa makanda ya
Mtama. Hata yule bwana wa nyumba akatafuta mtego akaenda ghalani akatega. Hatimye akapita panya akauona ale mtego akatambua kuwa mtego huu ametegewa yeye. Akapita jogoo panya akamwambia jogoo, "Wewe mwenzangu mkubwa kuliko, mimi hufanyi jamala ukaupiga teke huu mtego ufyatuke?"
jogoo akamwambia, "Mtego huu umetegewa wewe, mimi haunihusu kitu."
Panya akanena, "Kweli, lakini nauona umekaa vibaya wasije wakaingia waliomo na wasiokuwamo."
Jogoo akanena, "Najuaje?" akaenda zake.
Mara akapita mbuzi. Panya akamwambia mbuzi, "Bwana mdogo, hufanyi taratibu akaufyatua huu mtego na mimi nikapata riziki?"
Mbuzi akamwambia, "Mimi na mtego tu wapi? Mtego huu umetegewa wewe unayeharibu vitu vya watu, mimi chakula changu majani."
Panya akanena, "Kweli huu ni mtego wa panya, lakini tena ni mtego wa kuingia waliomo na ‘wasiokuwamo."
Mbizi akanena, "Mimi sijui hayo, akaondoka akaenda zake.
Hatimaye akapita ng’ombe. Panya akamwambia, "Ee Bwana mkubwa, tafadhali ufyatue huu mtego, na mimi nikapata riziki, tena nauona umekaa vibaya, wasije wakaingia waliomo na wasiokuwamo."
Ng’ombe akanena, "Hayo ni mambo yako wewe unayetoboa vya watu: mimi nakula majani, na mtama wapendapo kunipa. Sina haja kujishughalisha na mambo yasiyonihusu." Akaondoka akaenda zake. Na panya naye akaenda zake. Akawahubiria wenziwe kuwa ghalani kuna mtego wa kuwanasa.
Mara akapita nyoka naye anawinda panya, akapita njia ya mtego akanaswa. Yule mwenye nyumba aliposikia ukifyatuka akachukua fimbo akaenda ghalani. Mkewe akamwambia, "Bwana, huchukui taa?"
Akanena, "Kuna kuua panya kukahitaji taa?" Alipoufikia mtego kwa ile fimbo yake yule nyoka akamwuma. Yule bwana akasema, "Ah kaniuma ati!" Mkewe akaleta taa kumulika akasema, "si panya, bwana, ni nyoka."
Yule bwana akawa hoi, hoi tena maumivu yamemshika.
Huku na huku wakaitwa jamaa zake, wasidiriki kuja wote, akafa. Basi wakaja watu wachache usiku, ili kuwaliwaza wafiwa. Akachukuliwa jogoo akachinjwa kitoweo cha wale watu waliolala. Siku ya pili wakaja watu wengi kulala matangani. Akachukuliwa mbuzi akachinjwa kitoweo cha watu wa matangani. Hata siku ya kusoma hitma akachukuliwa ng'ombe akachinjwa, maneno ya panya yakatimia, ni mtego wa panya lakini wakaingia waliokuwamo na wasiokuwamo.