Hekima imuelekeze Mbowe kujiepusha na midahalo holela, badala yake ajikite kumobilize wajumbe wa mkutano mkuu ili apate ushindi wa kishindo kwa haki

Hekima imuelekeze Mbowe kujiepusha na midahalo holela, badala yake ajikite kumobilize wajumbe wa mkutano mkuu ili apate ushindi wa kishindo kwa haki

Wakati ule wa maandamano ya Chadema ulikuwa upande ule wa barabara, sasa uko upande huu wa barabara, eti?
elezea wadau kwa kina kifupi kidogo gentleman, kuhusu hilo..

hata hivyo,
nimeelezea kwa kifupi sana, kinagaubaga kuhusu mdahalo na sio maandamano gentleman 🐒
 
Uchaguzi ni wa chama, sio wa nchi. Mdahalo ni kwa ajili ya wapiga kura, sio kila mtu maana kuna maadui pia. Kama ni mdahalo, ufanyike ukumbini mbele ya wajumbe wa mkutano, vinginevyo mtanufaisha hata wasiohusika
 
Achana na mambo ya CHADEMA. Kamshauri mwenyekiti wa CCM a true Makamu Mwenyekiti
 
Hakuna haja wala sababu ya maana au ya msingi hata moja kwa Freeman Mbowe kupoteza muda wake na kushiriki midahalo ambayo ni wazi ina ushari ndani yake, na isiyo na tija wala maana yoyote, badala yake aelekeze nguvu na jitihada zake za kisiasa kucosolidate strong holds zake za wajumbe na kumobilize wajumbe wa mkutano mkuu Taifa, na kujipanga nao vizuri ili hatimae kujihakikishia ushindi wa uhakika, wa kishindo kwa uhuru, haki na uwazi.

Zaidi sana,
Ajiandae na maandalizi mengine muhimu mathalani, ya kuweka vipaumbele vya mambo muhimu ambayo atayaweka wazi mkutanoni, siku ya kujieleza wakati wa kuomba kura, mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema Taifa, ambao ndio waamuzi wa mwisho wa nani awe kiongozi wa Chadema Taifa.

My friends ladies and gentlemen, Je,
mdahalo huo unaopendekezwa una faida gani hasa, na ni kwa maslahi ya nani, wakati wagombea wana nafasi na fursa ya kujieleza kikamilifu mbele ya wajumbe zaidi ya 1000, wa mkutano mkuu wa chadema Taifa siku ya uchaguzi?

mbona kama kuna dalili za kishirikina? mnataka kumroga chairman ee, au kufurahisha mabenyenye ya magharibi yanayomfadhili Kibaraka?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Mbowe akifanya hivyo hizo ni dalili za rushwa kuanza ku mobileze wajumbe
 
Si anajiamini na kujiita mwamba? Aende kwenye mdahalo akagagaragazwe na lissu kama jinsi tramp alivyomgaragaza biden mpaka ikabidi ashauriwe asigombee tena urais. Naye mbowe akigaragazwa atashauriwa ajitoe kugombea tena uenyekiti
kwamba kutokushiriki mdahalo kutamfanya asiwe mwamba wa kaskazini, right?🤣

mdahalo compulsory upo, na ni mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu Taifa wa chadema, ambao ndio wapiga kura wa kuamua nani awe mwenyekiti wa Chadema Taifa,

huo mnao upepelea ufanyike ni ili kuwafurahisha mabwenyenye ya magharibi right?

au wanajieleza kwa nani?🤣
 
Kukimbia mdahalo ni udhaifu wa Kiongozi asiyejiamini na anayeng'ang'ana madarakani wakati anaowaongoza wamamchoka.
Kwa hiyo, kitendo chochote cha Mbowe kukimbia mdahalo ni kuitangazia Dunia kuwa hana uwezo tena wa kuongoza chama.

Huko mbeleni tutakuwa na mdahalo kati ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, sasa kama atakimbia hata mdahalo tu wa ndani ya chama, atawezaje kufanya mdahalo na CCM?
Lazima Mbowe aingie kwenye mdahalo, msianze kumkingia kifua sasa. Tena Mbowe asilete visingizio vyovyote ili kukwepa mdahalo.
 
aingie kwenye mdahalo ili iweje?

nini hasa dhima ya huo mdahalo wa jumla?

wagombea uongozi wa chadema wana nafasi na fursa ya kujieleza na kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu Taifa ili hatimae wapigiwe kura na hatimae kupimana nguvu kwenye sanduku la kura.

huo mdahalo unalenga nini au matokeo yake ni nini?

kujifurahisha?
au kufurahisha mabenyenye ya ya Magharibi?🐒
Sina shida na Wana CCM kukwepa midahalo. Inawezekana wana sababu zao za aidha woga au kutojiamini. Lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa watu wengine au vyama vingine visifanye midahalo. Chadema sio chama kikubwa kuliko Republican ya Marekani. Wao walianza midahalo ndani ya chama ili kumpata atakayegombea kupitia chama chao. Tuache uoga ndugu!
 
Kukimbia mdahalo ni udhaifu wa Kiongozi asiyejiamini na anayeng'ang'ana madarakani wakati anaowaongoza wamamchoka.
Kwa hiyo, kitendo chochote cha Mbowe kukimbia mdahalo ni kuitangazia Dunia kuwa hana uwezo tena wa kuongoza chama.

Huko mbeleni tutakuwa na mdahalo kati ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, sasa kama atakimbia hata mdahalo tu wa ndani ya chama, atawezaje kufanya mdahalo na CCM?
Lazima Mbowe aingie kwenye mdahalo, msianze kumkingia kifua sasa. Tena Mbowe asilete visingizio vyovyote ili kukwepa mdahalo.
Gentleman,
anakimbiaje na wakati ni Lazima kwa wakati muafaka, asimame mbele ya wajumbe, ajieleze na kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu Taifa wa chadema kabla ya kupigiwa kura..

huo mdahalo mnaoupigia chapuo anajieleza nini, kwa nani, na ili kitokee nini? kama sio kupoteza wakati?

asie na uwezo wa kuiongoza Chadema atashindwa na atakataliwa kwa kura kwenye uchaguzi utakaofanyika Jan. 22, 2025.

ni muhimu kutuliza mawenge ndrugu zango 🐒
 
Kamuulize marehemu wenu chato aliyeahidi kuiuwa chadema mtaota sana na msipoandaa mafungu ya polisi kuwalipa ili muwatumie kama trash mtalia kilio hata wa kuwanyamazisha hatakuwepo by the way endelea kuota kuwa chadema imekufa huku unaijadili.
Chadema ilishajifia, marehemu hua anajadiliwa tu ndio maana hata wewe umemtaja marehemu Magufuli.

Juzi hapa Mbowe aliitisha maandamano wakaandama yeye na waandishi wa habari, jiji kama la Dar es Salaam lenye watu zaidi ya milioni 6 unaitisha maandamano wanajitokeza waandishi wa habari halafu useme hicho chama bado kipo?

Wewe na mbowe endeleeni kuota ndoto za mchana. Hata Lissu ameshtuka ndio maana ameamua amwage mboga kabisa kwa kutoa siri za ndani kwamba chama kinafadhiliwa na ccm halafu kwa nje Mbowe anadanganya umma kwmaba chama kiko imara, imara chini ya ccm?

Acha ccm mwakani iwafanye hamna na huyo mwenyekiti wenu.
 
Hakuna haja wala sababu ya maana au ya msingi hata moja kwa Freeman Mbowe kupoteza muda wake na kushiriki midahalo ambayo ni wazi ina ushari ndani yake, na isiyo na tija wala maana yoyote, badala yake aelekeze nguvu na jitihada zake za kisiasa kucosolidate strong holds zake za wajumbe na kumobilize wajumbe wa mkutano mkuu Taifa, na kujipanga nao vizuri ili hatimae kujihakikishia ushindi wa uhakika, wa kishindo kwa uhuru, haki na uwazi.

Zaidi sana,
Ajiandae na maandalizi mengine muhimu mathalani, ya kuweka vipaumbele vya mambo muhimu ambayo atayaweka wazi mkutanoni, siku ya kujieleza wakati wa kuomba kura, mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema Taifa, ambao ndio waamuzi wa mwisho wa nani awe kiongozi wa Chadema Taifa.

My friends ladies and gentlemen, Je,
mdahalo huo unaopendekezwa una faida gani hasa, na ni kwa maslahi ya nani, wakati wagombea wana nafasi na fursa ya kujieleza kikamilifu mbele ya wajumbe zaidi ya 1000, wa mkutano mkuu wa chadema Taifa siku ya uchaguzi?

mbona kama kuna dalili za kishirikina? mnataka kumroga chairman ee, au kufurahisha mabenyenye ya magharibi yanayomfadhili Kibaraka?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Pale wapiganiaji mdahalu wanapoona midahalo ni Adui kwa ni kichekesho mbona
 
Sina shida na Wana CCM kukwepa midahalo. Inawezekana wana sababu zao za aidha woga au kutojiamini. Lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa watu wengine au vyama vingine visifanye midahalo. Chadema sio chama kikubwa kuliko Republican ya Marekani. Wao walianza midahalo ndani ya chama ili kumpata atakayegombea kupitia chama chao. Tuache uoga ndugu!
Gentleman,
hao wamarekani walikua wanafanya midahalo ya kugombea uongozi wa nafasi gani kwenye chama cha republican?

hata hivyo,
visionary leaders kama Trump na hata MBOWE wanapima mantiki ya mdahalo ndipo wanashiriki,

lakini,
huu mjadala wa eti kibaraka na mbowe ni completely useless 🐒
 
Nilichojifunza kwenye huu uzi wako;

1:Mbowe hana hoja na hawezi akajenga hoja kumzidi Lissu

2:CCM mnamuogopa sana Lissu na mnaomba usiku na mchana FAM ashinde ili muweze kumuendesha………Mnajua kabisa akiingia Simba TAL yeye ndiye atawaendesha na atawapelekea moto vibaya sana

3:Ni utaratibu wa kiongozi dhaifu kukimbia midahalo,unahisi wapiga kura wa “Mwamba tuvushe” atawapatia wapi ikiwa hataki hoja zake ziwe public!??

4:Nchi inamuhitaji Lissu kuliko Lissu anavyo ihitaji Nchi/CHADEMA

Tulia dawa ikuingie taratibu wewe Chawa na hapo bado,safari hii mtaomba TAL apotee kabisa hapa duniani na yeye anafahamu hilo coz hana cha kupoteza
Sipati picha apa lissu anapeleke mashambulizi pale yupo MWABUKUSI mbna ccm watakoma!? tupate wap watu kama Hawa!?
 
Mbowe akifanya hivyo hizo ni dalili za rushwa kuanza ku mobileze wajumbe
Gentleman,
ndicho kinachofanyika tangu uchaguzi wa ndani ya chadema uanze,

unadhani hasira za kibaraka wa mabwenyenye ya Magharibi zinatoka wapi? kila mjumbe anae mgusa ili amuunge mkono anaambiwa umechelewa 🐒
 
Sipati picha apa lissu anapeleke mashambulizi pale yupo MWABUKUSI mbna ccm watakoma!? tupate wap watu kama Hawa!?
makamanda,
hapo mnapeana matumaini au faraja?🤣
 
Gentleman,
anakimbiaje na wakati ni Lazima kwa wakati muafaka, asimame mbele ya wajumbe, ajieleze na kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu Taifa wa chadema kabla ya kupigiwa kura..

huo mdahalo mnaoupigia chapuo anajieleza nini, kwa nani, na ili kitokee nini? kama sio kupoteza wakati?

asie na uwezo wa kuiongoza Chadema atashindwa na atakataliwa kwa kura kwenye uchaguzi utakaofanyika Jan. 22, 2025.

ni muhimu kutuliza mawenge ndrugu zango 🐒
Yeye ni Mwamba kama mnavyompamba. Kwa nini kwenye issue ya mdahalo mnakuwa wapole na mnaandaa mazingira ya kukimbia?
Narudia tena, kitendo cha kukimbia mdahalo ni kuwathibitishia wajumbe kuwa hana tena uwezo wa kuongoza chama, hivyo wamchague mwingine.
 
Back
Top Bottom