Hili jambo la msingi sana uliloandika mleta mada, kila siku tumekuwa tunalalamika mahakama zetu hasa mahakama kuu imeoza, majaji wake wameiondolea credibility imepoteza uaminifu kwa watanzania wote wapenda haki.
Kinachofuata kifanyike nini ili kututoa hapa tulipo? hili linahitaji suluhisho la muda mfupi ambalo litasaidia kurudisha imani ya watu kwa mahakama zetu, hapa ndio hoja yako mleta mada inapata nafasi.
Jaji mkuu anatakiwa ajiuzulu, tusiendelee kulea huu uozo matokeo yake wengi watazidi kuumizwa na maamuzi ya hovyo yanayolenga kuwaumiza wapinzani wa serikali ya CCM yasiyofuata misingi ya sheria na haki za binadamu.
Napendekeza pawepo na movement isiyo na mwisho kumtaka jaji mkuu ajiuzulu mara moja kwa kushindwa kuwaweka majaji walio chini yake wafuate misingi ya haki wakiongozwa na sheria, naamini kwa nafasi yake ana mamlaka ya kuwashughulikia wote wanaokiuka viapo vyao, lakini kwa kukaa kwale kimya anaoneaha nae hafai kuendelea kushikilia hiyo nafasi.
Tusihangaike kila siku na hawa majaji wa chini wasiojali miiko ya taaluma yao, sasa tumuangalie yule kiongozi wao anayeonekana kukaa kimya na kufurahia huu uozo unaoidhalilisha tasnia ya sheria nchini kwetu Tanzania.