Heko kwa Kufuzu, ila kwa Mpira 'mbovu' tuliocheza na kwa Timu tunayoenda Kukutana nayo, tukifuzu Nusu Fainali mnizamishe Baharini na Jiwe

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Tusheherekee zetu tu kwa Kushinda jana na Kufuzu huko Robo Fainali ya CAFCC na kupata hicho Kitita cha Shilingi Milioni Mia Nane ( 800,000,000/= Tsh)

Ila kwa Mpira mbovu niliouona Jana huku Beki Onyango, Beki Tshabalala, Viungo Mkude na Kanoute na Washambuliaji Morrison na Sakho wakionyesha Utoto mwingi na Kunyimana Pasi na kutaka Sifa Binafsi za Kufunga GENTAMYCINE nakuwa wa Kwanza kusema kuwa Safari yetu ndiyo imeishia hapa.

Simba SC inaenda Kukutana na Moja ya Vigogo hivi viifuatavyo Barani Afrika hivyo ninaposema kuwa tunaishia hapa Robo Fainali kutokana na kuwa na Timu mbovu kwa sasa na yenye Kiwango kibovu hasa kwa Mechi za Kimataifa ninamaanisha.....

1. TP Mazembe ( Congo DR )
2. Orlando Pirates ( South Africa )
3. Al Ahly Tripoli ( Libya )

Najua kwa huu Uzi wangu msiotaka Ukweli, wapenda Unafiki na msio na Jicho la Kiufundi la Kimpira hapa mtanitukana na Kunidhihaki kwa kila namna na mpo pia ambao mtasema Mimi ni Yanga SC ila nasisitiza tena kuwa Mafanikio yetu yameishia Jana tu kwa kufika hapa Robo Fainali ya CAFCC lakini nina uhakika wa 100% kwa Simba SC hii ya sasa 'hatutoboi' kamwe hatua ya Nusu Fainali.

Na nakumbusha tu kuwa hizi Mechi za hatua Robo Fainali kati ya moja ya hizo Timu nilizozitaja hapo juu zitachezwa / tutacheza kati ya tarehe 15 hadi 17 Mwezi huu wa April na kurudiana tena kati ya tarehe 22 hadi 24 Mwezi April, 2022.

Timu inashinda kwa Morali tu ya Pesa kwa Ahadi za Mwekezaji na Rais wa Heshima Mohammed Dewji na Mambo yetu ya 'Kienyeji' hasa ya Nje ya Uwanja ila siyo kwa Kiwango cha Mpira kinachotakiwa na hata Kocha wa Simba SC hana Ubora na Uzuri huo na hatuna Wachezaji wa Kiushindani isipokuwa tunao tu hawa wa Kubahatisha ambao leo Moja wanatufurahisha lakini Mechi zaidi ya Tano ( 5 ) za Ligi au za ASFC au za Kimataifa Wanaharibu na Kurukaruka tu Viwanjani

Ushauri wangu wa mwisho kwakuwa nina uhakika kuwa Simba SC tunaenda kuishia tu hapa Robo Fainali nashauri tujikite tu zaidi huku katika NBC Premier League na kule ASFC ili tubebe Ubingwa ( japo katika Ligi Kuu ya NBC nina wasiwasi kama tutabeba ) na tukifanikiwa basi Uongozi wa Simba SC ufanye Maamuzi Magumu ya Kuachana ( Kuwatema ) Wachezaji wengi Wazawa na hata Wageni ( wasio na Hadhi ya Kuchezea Simba SC kwa sasa ) kisha Tusajili Wachezaji mahiri na wa uhakika kweli kama ambao baadhi yao wapo kwa Watani zetu Yanga SC mfano wa akina Beki Kiraka Yanick Bangala, Kiungo Fundi Khalid Aucho na Mshambuliaji hatari Fiston Mayele ( wa Nje ) na akina Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Feisal Salum Fei Toto ( wa Ndani )

Kila Ia Kheri Mechi yetu na Coast Union FC katika Ligi Kuu ya NBC tarehe 7 April, 2022 na Mechi ya Police Tanzania Wikiendi hii ijayo na tugangamale kweli katika Mechi zetu zote za Ligi Kuu na hata Kombe la ASFC kwani kwa hatua za sasa hakuna Kulala wala Mzaha tena kwani kwa Upinzani mkubwa uliopo na jinsi Yanga SC ilivyo na Kiwango kikubwa na cha Hatari ( huku wakiwa wamejipanga vyema ndani na nje ya Uwanja ) kuna uwezekano pia ambao GENTAMYCINE nauona wa Wao ( Yanga SC ) kubeba Ubingwa ( Makombe ) yote haya na Simba SC yetu ( yangu ) kwa Msimu huu tukabaki na Mafanikio ya Kubeba Kombe la kuishia tu Robo Fainali ya CAFCC.

'Ukweli' huuma, ila ni 'Dawa' inayotibu!!!

Cc: Mzizi wa Mbuyu
 
Mbona unakata tamaa mapema mkuu wayafanyie mapema tu mapungufu ..hao vigogo tutawakalisha tu .Mungu wetu sote.
 
With all my respect kwako mkuu, mada hii hujaifanyia nchi na club ya Simba sc haki yake, vilabu vyote ulivyoviorodhesha hapo msimu huu ni vya kawaida kabisa, labda TP Mazembe lakini sio hao Mabakabaka ni wa kawaida mno msimu huu(masandawana wameshapeperuka na ubingwa wa nchi)hao kutoka Tripoli ndio weupe kabisa, this time Simba sc anaingia semi, tunaweza bet kwa faida ya charity hapa mimi na wewe mkuu, kitakachopatikana kwa mshindi tusaidie wanaohitaji msaada zaidi.
 
Kweli isemwe mpira wa Hovyo sana Sana...Simba inabidi ijiangalie sana kwenye game plan unashindwa kuelewa wanacheza formation gani...
 
Ukweli mchungu, wakubali wakatae msimu huu simba ni weupe kwa mambo ya kiufundi tunayoyaona sisi tunaoujua mpira mnayo kazi ya ziada Sana vinginevyo endeleeni kutegemea ushindi wa nje ya uwanja lakini ndani ya uwanja mtakuwa mnapata tabu sana kwa timu zinazofahamu janja zenu mnazofanya nje ya uwanja.

aina ya wachezaji mnaotegemea wawape matokeo asilimia kubwa wamechoka awana mbinu mpya wala kasi uwanjani, wachezaji wa aina hii wataonekana ni wazuri wamapokuwa wamepata msaada wa makafara na figisu nyingine za nje ya uwanja kinyume chake mnalia na kusaga meno.

kufuzu robo fainali wala sio hoja kwa kuwa mlikuwa na advantage ya home ground na mkiitaji ushindi wowote wakati mimosas walikuwa ugenini wakicheza na timu nyingine iliyokuwa inahitaji ushindi ili ifuzu.

kwa mazingira ayo mngeshindwa kuingia robo na uyo kocha wenu alitakiwa afukuzwe maana ingekuwa ameonyesha udhaifu wa hali ya juu wa kimbinu.
 
Kwa ubinafsi wa jana kipindi cha kwanza kama utaendelea mechi ya robo fainali ambayo tutaanzia nyumbani, uhakika wa kuishia robo fainali ni mkubwa mno.
 
Ukweli mchungu, wakubali wakatae msimu huu simba ni weupe kwa mambo ya kiufundi tunayoyaona sisi tunaoujua mpira mnayo kazi ya ziada Sana vinginevyo endeleeni kutegemea ushindi wa nje ya uwanja lakini ndani ya uwanja mtakuwa mnapata tabu sana kwa timu zinazofahamu janja zenu mnazofanya nje ya uwanja, aina ya wachezaji mnaotegemea wawape matokeo asilimia kubwa wamechoka awana mbinu mpya wala kasi uwanjani, wachezaji wa aina hii wataonekana ni wazuri wamapokuwa wamepata msaada wa makafara na figisu nyingine za nje ya uwanja kinyume chake mnalia na kusaga meno, kufuzu robo fainali wala sio hoja kwa kuwa mlikuwa na advantage ya home ground na mkiitaji ushindi wowote wakati mimosas walikuwa ugenini wakicheza na timu nyingine iliyokuwa inahitaji ushindi ili ifuzu, kwa mazingira ayo mngeshindwa kuingia robo na uyo kocha wenu alitakiwa afukuzwe maana ingekuwa ameonyesha udhaifu wa hali ya juu wa kimbinu
Tunashukuru kwa pumba zako.
 
Tusheherekee zetu tu kwa Kushinda jana na Kufuzu huko Robo Fainali ya CAFCC na kupata hicho Kitita cha Shilingi Milioni Mia Nane ( 800,000,000/= Tsh)

Ila kwa Mpira mbovu niliouona Jana huku Beki Onyango, Beki Tshabalala, Viungo Mkude na Kanoute na Washambuliaji Morrison na Sakho wakionyesha Utoto mwingi na Kunyimana Pasi na kutaka Sifa Binafsi za Kufunga GENTAMYCINE nakuwa wa Kwanza kusema kuwa Safari yetu ndiyo imeishia hapa.

Simba SC inaenda Kukutana na Moja ya Vigogo hivi viifuatavyo Barani Afrika hivyo ninaposema kuwa tunaishia hapa Robo Fainali kutokana na kuwa na Timu mbovu kwa sasa na yenye Kiwango kibovu hasa kwa Mechi za Kimataifa ninamaanisha.....

1. TP Mazembe ( Congo DR )
2. Orlando Pirates ( South Africa )
3. Al Ahly Tripoli ( Libya )

Najua kwa huu Uzi wangu msiotaka Ukweli, wapenda Unafiki na msio na Jicho la Kiufundi la Kimpira hapa mtanitukana na Kunidhihaki kwa kila namna na mpo pia ambao mtasema Mimi ni Yanga SC ila nasisitiza tena kuwa Mafanikio yetu yameishia Jana tu kwa kufika hapa Robo Fainali ya CAFCC lakini nina uhakika wa 100% kwa Simba SC hii ya sasa 'hatutoboi' kamwe hatua ya Nusu Fainali.

Na nakumbusha tu kuwa hizi Mechi za hatua Robo Fainali kati ya moja ya hizo Timu nilizozitaja hapo juu zitachezwa / tutacheza kati ya tarehe 15 hadi 17 Mwezi huu wa April na kurudiana tena kati ya tarehe 22 hadi 24 Mwezi April, 2022.

Timu inashinda kwa Morali tu ya Pesa kwa Ahadi za Mwekezaji na Rais wa Heshima Mohammed Dewji na Mambo yetu ya 'Kienyeji' hasa ya Nje ya Uwanja ila siyo kwa Kiwango cha Mpira kinachotakiwa na hata Kocha wa Simba SC hana Ubora na Uzuri huo na hatuna Wachezaji wa Kiushindani isipokuwa tunao tu hawa wa Kubahatisha ambao leo Moja wanatufurahisha lakini Mechi zaidi ya Tano ( 5 ) za Ligi au za ASFC au za Kimataifa Wanaharibu na Kurukaruka tu Viwanjani

Ushauri wangu wa mwisho kwakuwa nina uhakika kuwa Simba SC tunaenda kuishia tu hapa Robo Fainali nashauri tujikite tu zaidi huku katika NBC Premier League na kule ASFC ili tubebe Ubingwa ( japo katika Ligi Kuu ya NBC nina wasiwasi kama tutabeba ) na tukifanikiwa basi Uongozi wa Simba SC ufanye Maamuzi Magumu ya Kuachana ( Kuwatema ) Wachezaji wengi Wazawa na hata Wageni ( wasio na Hadhi ya Kuchezea Simba SC kwa sasa ) kisha Tusajili Wachezaji mahiri na wa uhakika kweli kama ambao baadhi yao wapo kwa Watani zetu Yanga SC mfano wa akina Beki Kiraka Yanick Bangala, Kiungo Fundi Khalid Aucho na Mshambuliaji hatari Fiston Mayele ( wa Nje ) na akina Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Feisal Salum Fei Toto ( wa Ndani )

Kila Ia Kheri Mechi yetu na Coast Union FC katika Ligi Kuu ya NBC tarehe 7 April, 2022 na Mechi ya Police Tanzania Wikiendi hii ijayo na tugangamale kweli katika Mechi zetu zote za Ligi Kuu na hata Kombe la ASFC kwani kwa hatua za sasa hakuna Kulala wala Mzaha tena kwani kwa Upinzani mkubwa uliopo na jinsi Yanga SC ilivyo na Kiwango kikubwa na cha Hatari ( huku wakiwa wamejipanga vyema ndani na nje ya Uwanja ) kuna uwezekano pia ambao GENTAMYCINE nauona wa Wao ( Yanga SC ) kubeba Ubingwa ( Makombe ) yote haya na Simba SC yetu ( yangu ) kwa Msimu huu tukabaki na Mafanikio ya Kubeba Kombe la kuishia tu Robo Fainali ya CAFCC.

'Ukweli' huuma, ila ni 'Dawa' inayotibu!!!

Cc: Mzizi wa Mbuyu
Uliuona wapi wakati ulikuwa uchochoroni kwenye vibanda vya wauza 'shake shake beer' (pombe ya matapu tapu).
 
Naheshimu mawazo yako na mtazamo wako, lakin nina imani tutafanya vizuri japo sitamani tukutane na timu kutoka Afrika kusini
 
Back
Top Bottom