Parata
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 3,090
- 680
nimeona ni vema kuwaeleza ndugu zangu walioko chuo na wanaotarajia kuingia chuo mwaka huu kuwa pesa tunayopewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu(heslb)Kama mtu umebahatika kupata utailipa kama wanavosema ingawa kuna maneno ya kufarijiana tukiwa chuo kuwa ooh sitalipa ila kiukweli kila mtu atalipa na kuna kupingwa faini kama umechelewa kuanza kulipa nadhani mmesoma haya sasa cha kufanya ni kuhakikisha kuwa unatumia pesa hiyo vizuri lasivyo kuna kujuta.kuna wapenda kuiga na starehe za ajabu ajabu,kuna wanaozani kuwa hela hizo ni nyingi na si kweli...kwaiyo kama mwanajamii nimeona ni vema kuwashauri haya tusije baadae tukapata malalamiko hatukuwaambia na tahadhari ni kuwa usije ukatoka huko kwenu kama first year na ukaja na ela ya nauli ukizani kuwa eti kuna mkopo tu ukiripoti,serikali na bodi yake na vyuo vingi sana havieleweki kwenye kutoa hiyo pesa na first year kwa uelewa wangu ni mpaka wafanyiwe registration wakae kidogo ndio wapewe kwaiyo jiandae vema.......
NAWASILISHA
NAWASILISHA