Naona history inazidi kujirudia. Hapo kale, NCCR Mageuzi kilikuwa chama kikuu cha upinzani. Kilidhoofishwa na kuporomoshwa na migogoro/mipasuko ya design hii. Baada ya hapo chama cha CUF kikalivaa hilo taji la chama kikuu cha upinzani. Kama vile watu wake hawakujifunza yale yaliyokiporomosha chama cha NCCR Mageuzi, nao hawakuweza kuyaepuka; CUF nayo ikaporomoka na hivi ninavyoandika (na wewe unaposoma) iko na inaendelea kuwa kwenye life support!
Kwa mwenendo huu wa CHADEMA, ACT Wazalendo hawana budi kujiandaa kukipokea kijiti cha chama kikuu cha upinzani. Siamini kama CHADEMA ni clever enough kuweza kuukwepa huu mkenge!