Hela ya mwekezaji Simba itarudi kwa kuuza mechi Yanga, Azam

Hasara utakayoipata wewe shabiki wa kawaida uliyekuwa umezoea kuingia uwanjani kiujanjaujanja, kununua jezi zilizotandazwa chini kwa 2000, uliyezoea kuaona Ndanda lazima ifungwe na Simba, uliyezoea kusikiliza mechi za Simba kwenye redio, uliyekuwa umezoea kupata ticket kwa njia za ajabuajabu, uliyekuwa unaendesha maisha yako kwenye mgongo wa Simba (majengo ya klabu, mabaunza, wauza vifaa feki vya Simba) sasa hivi ndiyo mwisho wenu. Viongozi walikuwa wanaongelea yale mazuri tu ya mfumo huu lakini hawakuwaambia mashabiki nini wategemee kutoka kwenye mfumo huu mpya wa uendeshaji mpira ambao wacheza kamali na watafuta faida ni kikwazo kikubwa kwa furaha za mashabiki.
 
sorry
 
Umeongea vizuri
 
Shabiki yeyote duniani unachotakiwa kuhoji ni performance mbaya ya team peke yake.Vitu vingine huna haki ya kuhoji.Period.
 
Ni sensa ipi ilifanyika kuonyesha simba inawashabiki wachache halaf yanga ni wengi.Au ni mambo yako ya kichoko
 
Ndiyo maana kuna tofauti kati yako, na MO, usipopaona wewe yeye hupaona, ndiyo maana yupo pale. Lazima tukubali mabadiliko ingawa ni magumu mwanzoni.
 
Umeongea kweli ila jambo kubwa ninalo kiulizA ni jinsi gani MO atapata Faida au kurudisha Pesa yake aliyo wekeza.....

Kama atafanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika..Mazingira Ya nchi yetu kwa sasa sio rafiki katika uwekezaji kwenye soka...

Kwa mimi ilikuwa kama sisi wadau wa mpira tungepiga kelele kwanza miondo mbinu iwe mizuri hata mwekezaji akiwekeza kwenye timu ajue anakuja kupata Faida...!
Sasa Leo Mishahara ya wachezaji ya miezi miwili ni sawa na zawadi ya mshindi VPL + FA.....

Bidhaa za Simba walizo nazo sidhani kama zinafika mauzo ya 200milioni...

N:B Pia kwenye hili clubs zingine zinatakiwa zijifu ze kupitia Simba
 
Mkuu una uwakika Simba anaweza kuuza Jezi Milion 5 kwa msimu mmoja[emoji52][emoji52]?
 
Kaka hata purchasing power ya watanzania ni ndogo sana kuweza kununua huduma za mpira. Watanzania wengi bado wanahangaika kupata chakula, maji, matibabu, malazi, na Usafiri. Wanamudu kununua bidhaa kuukuu zilizokwishatumika mahala pengine na vile bandia kutoka Asia. Ukosefu wa ajira, ujira mdogo, na kilimo, ufugaji na uvuvi duni ni chanzo cha tatizo. Kuuza mechi kunaweza kuwa chanzo muhimu cha mapato kwa muwekezaji wa mpira Tanzania hasa katika kipindi hiki ambacho kodi ni lazima ulipwe na madawa ya kulenya hakuna.
 
Nimeumia sana roho .
 
Usilolijua acha kuchangia, watu watang'amua uwezo wako na kukuacha kama ulivyo - Mo ni mfanyabiashara kupitia Simba atatangaza biashara zake na zitamlipa maradufu jinsi club inavyopata umaarufu ndani na nje ya nchi we unadhani Heineken wanavyoidhamini UCL wanalipwa? Wao ndio wanalipa kwani umaarufu wa Uefa Champion ni Duniani kote kupitia ilo Heineken imetambulisha na kufahamika kweli kweli ulimwenguni na imefungua branch nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania na wanafanya biashara kweli kweli hii ndio siri ya wafanyabiashara wengi kununua bilabu mkuu
 
Ninapenda Heineken na Windhock lakini sio kutokana na UCL bali kutokana ubora wao na promotion wanazofanya kwenye mabaa mbalimbali, sidhani kama wewe unakunywa Heineken kwakuwa umeiona UCL. Watanzania wengi hawana choice bali wanaongozwa na uwezo wao wa kununua. Man U inadhaminiwa na kampuni la magari la Kimarekani la Chevrolet, wako Watanzania wanaipenda Man U lakini hawana magari ya Chevrolet.
 
Jibu: Ni wengi wenye uwezo wa kufanya hivyo
 
Biashara matangazo, leo hii mtu aliyeko kijiji angeweza kuelewa kama man u wadhamini wake wakuu ni watengeneza magari kama sio kujitangaza?
 
Hivi Nyinyi [HASHTAG]#Ndala[/HASHTAG] Kwanini Munawashwa na Mambo Ya Simba?
Wacheni Wivu Huo Kwa Kuona Simba imepiga Hatua....
Muekezaji Ni Mfanya Biashara! Kwahiyo Pakuzipata Pesa anapajua Yeye... Wewe Hayakuhusu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…