Kujenga viwanja viwili vya kisasa, kufanya usajili wa wachezaji wa kisasa kabisa wanaoweza kuifunga Yanga wakati wowote, kulipa mishahara ya wachezaji hao kila mwezi, kujenga gym, kujenga hostels za kisasa, kulisha wachezaji, kutibu wachezaji na kusafirsha timu wewe unadhani inaweza kuwa hela ngapi? Purchasing power ya mashabiki wa simba unaijua? wenye uwezo wa kununua zitakazokuwa bidhaa bora original za club wanaweza kuwa wangapi?. Watakaoacha kutumia/kununua bidhaa nyingine na kuvutika kutumia bidhaa za MO (juice, sabuni, na bidhaa nyingine za MO Limited) kwasababu tu MO ndiye mdhamini wa club yao na kuacha biadhaa nyingine zinazofanana au kuzidi kwa ubora bidhaa za MO ni wangapi?