Hela ya Tanzania haina thamani tena, naanza kuiona Zimbabwe Bongo

Ozon

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2024
Posts
2,910
Reaction score
4,711
Hizi ni ishara tosha kwamba hela ya Tanzania imepoteza thamani yake rasmi.Bwana siku hizi, mtaani na kwenye mitandao ya kijamii kumezuka tabia ya Watanzania kutrendisha mambo yasiyo na manufaa yoyote kama kawaida ya wabongo. Watu wanachezea minoti ya shilingi kumi kumi kama wamevurugwa hivi, kana kwamba ni jambo la kawaida, wakijinadi kwa mabulungutu ya noti hizo kwenye sherehe, shughuli mbalimbali, huku ma-influencer, machawa, content creators, forex traders na wengine wakitembea na mabegi yaliyojaa noti kwenye magari kama kawaida yao.

Hata hivyo, licha ya mbwembwe zote hizo, uhalisia wa maisha mtaani ni mgumu. Watu wana noti nyingi za shilingi elfu kumi, lakini hazifanyi jambo lolote la maana. Hata ukiwa na laki moja au laki tano, ukiingia sokoni haziwezi kukupatia vitu vingi vya maana.

Aisee, tukubali tukatae, hela ya Tanzania haina thamani tena. Watu wanazidi kujaza makaratasi kwenye mabegi, lakini hayana thamani yoyote kwa
sasa.
 
thamani bado ipo japo kwa kidogo sana isipokua imeathiriwa zaidi na udumavu wa ujira wa mtu mmoja mmoja..Malipo ya raia wa Tanzania yalitakiwa yaongezeke katika Kila sekta ili yaendane na mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali muhimu ulioikumba Dunia na Tanzania kwa ujumla.

Sasa wew kama bado unalipwa laki nne na haijapanda wakati huohuo mafuta yamepanda bei na nauli na vyakula vimepanda wht do you expect??

Serikali haramu haitufai

Over
 
From what i know, hali ya maisha mtaani siyo nzuri. Thamani ya pesa nayo kwenye mzunguko na matumizi ya kila siku hauridhishi.

Mfano shilingi 50 na 100 zinaelekea kupotea kwa sababu ya kukosekana vitu vya kununulia. Noti za elfu moja na elfu mbili zinatumika mpaka zinatia huruma. Ukija kwenye noti za elfu tano na elfu kumi na zenyewe hali si hali. Ukishika elfu 10 ukiingia sokoni au dukani unatoka na nidhaa chache na hubakiwi ma kitu.

Hali hii ikiendelea, sitashangaa serikali ya ccm ikija na wazo la kuchapicha noti ya elfu 20 na elfu 50!

CCM wanatupeleka shimoni ndugu zangu. Huu ni ukweli mchungu. Mimi sito mchumi wa kusomea darasani. Nimeongea kutokana na uhalisia wa maisha ya huku mtaani tuliko. Mfumuko wa bei na mzunguko mdogo wa biashara unatisha.
 
Hizi ni ishara tosha kwamba hela ya Tanzania imepoteza thamani yake rasmi.Bwana siku hizi, mtaani na kwenye mitandao ya kijamii kumezuka tabia ya Watanzania kutrendisha mambo yasiyo na manufaa yoyote kama kawaida ya wabongo. Watu wanachezea minoti ya shilingi kumi kumi kama wamevurugwa hivi, kana kwamba ni jambo la kawaida, wakijinadi kwa mabulungutu ya noti hizo kwenye sherehe, shughuli mbalimbali, huku ma-influencer, machawa, content creators, forex traders na wengine wakitembea na mabegi yaliyojaa noti kwenye magari kama kawaida yao.

Hata hivyo, licha ya mbwembwe zote hizo, uhalisia wa maisha mtaani ni mgumu. Watu wana noti nyingi za shilingi elfu kumi, lakini hazifanyi jambo lolote la maana. Hata ukiwa na laki moja au laki tano, ukiingia sokoni haziwezi kukupatia vitu vingi vya maana.

Aisee, tukubali tukatae, hela ya Tanzania haina thamani tena. Watu wanazidi kujaza makaratasi kwenye mabegi, lakini hayana thamani yoyote kwa
sasa.
Naandaa Zimbabwe......Roma Mkatoliki
 
thamani bado ipo japo kwa kidogo sana isipokua imeathiriwa zaidi na udumavu wa ujira wa mtu mmoja mmoja..Malipo ya raia wa Tanzania yalitakiwa yaongezeke katika Kila sekta ili yaendane na mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali muhimu ulioikumba Dunia na Tanzania kwa ujumla.
Sasa wew kama bado unalipwa laki nne na haijapanda wakati huohuo mafuta yamepanda bei na nauli na vyakula vimepanda wht do you expect??..Serikali haramu haitufai

Over
Kwamba ukipandisha mishahara thamani itaongezeka!? Hizo ni issues mbili tofauti, Hela ya Tanzania haina thamani na bado mishahara ya wafanyakazi ipo chini.
 
Kiongozi mkuu chura aka kizimkazi Hana elimu nzr zaidi ya hapa na pale.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom