TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Rest In Peace Deo Filikunjombe. Poleni sana wanafamilia na wana Ludewa!
 
Kama ni kosa kupotosha kuwa mtu amefariki wakati yuko hai, je si kosa kupotosha kuwa mtu yuko hai wakati amefariki?
 
Poleni Familia ya wafiwa. Tumempoteza kiongozi muwajibikaji.


Je, mtu anapotoa taarifa za uongo yampasa afanyweje na TCRA? Makama katudanganya kuwa helikopta zote za chama ziko salama, taarifa hii awali ilipunguza majonzi kwetu na kurudisha tumaini juu ya wapendwa wetu.Ila ilipokuja taarifa ya uhakika imekuwa ni pigo kubwa sana kwetu lililotea mpasuko mkubwa ktk miyo yetu.

Nashindwa kuelewa tumwamini nani, ikiwa hata hao viongozi wanaosimamia wizara nyeti za mawasiliano wanatuhadaa, na kutupa tumaini bila kufanya uhakiki wa taarifa inayokwenda kwa walaji.

R.I.P Deo, R.I.P woote waliofikwa na ajali hii mbaya.

Tuweke tofauti zetu za kisiasa kando, tuwajibike na kushiriki pamoja na familia ya marehemu ktk kuwafariji kwenye kipindi hiki kigumu cha majonzi.
 
Mwanadamu hawezi kuingia mipango ya MUNGU, katika uchaguzi huu muumba wetu alipanga yatokee hayo, ingawa sisi hatukujua lakini ilikuwa mipango yake ya sirini. Kuna siku nilipata maono kuwa watakufa wanasiasa wanaogombea ubunge wapatao sita (6). Naamini Filikunjombe ametimiza idadi hiyo. TUENDELEE KUMUOMBA MUNGU ALIEPUSHE TAIFA LETU NA MACHAFUKO TUNAPOELEKEA KATIKA UCHAGUZI, maana naliona giza nene likiwa limeifunika nchi yetu kwa muda wa miezi sita.
 
Hiyo Tweet ya January sijaisoma, ila kwa jinsi watu wanavyoonyesha kukasirika lazima itakuwa ya hovyo sana. Jambo ambalo wengi ndani ya CCM hawajui ni kuwa pamoja na kuwa Baba yake January Mzee Makamba alikuwa Bogus sana kiasi cha kuitwa Pwagu, huyu mwanae ni zaidi ya baba. Lakini ndani ya CCM mtu akiwa bogus lakini mjanja mjanja basi huwa anachukuliwa ni Think tank. Hasa kama ataonyesha mbinu chafu za kukabiliana na Wapinzani.
Unaweza kushangaa mwenyewe kuwa katika timu ya watu Mashuhuri 32 walioteuliwa na chama kumkampenia mgombea wa chama Tawala (maana lazima uwe mashuhuri na makini) wapo Lusinde na Asumpta Mshama. Hiyo ni kuonyesha hata mtu wa hovyo hovyo kabisa anaweza kuonekana Mahiri kama tuu anaweza kuutukana upinzani bila aibu na kuandaa mbinu chafu.
Ndivyo ilivyo kwa Makamba.
Watu kama Profesa Mwandosya kinachowauma siyo kukatwa majina bali wao ni Usomi wao wote na uzoefu wa miaka mingi kukatwa majina na tano bora kuigizwa muhuni kama January Makamba, hii ni zaidi ya dharau na kwa wale ambao hawaijui vizuri ccm wakawaulize Balozi Mahiga na Jaji Augustino Ramadhani wamefundishwa kwa vitendo kwamba ccm ni chama cha aina gani.
 
Huyu Makamba katoa kauli gani?

makamba mnamuonea bure enyi watu,,,yeye alikua anafuata ripoti ya ITV waliotangaza kuwa filikunjombe yuko salama...makamba nadhani kwa kuaimini itv,alidhani itv wamestablish contact na deo....sasa hapa anaepaswa kulaumiwa ni itv
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na ambayo hatujawahi kushuudi tanzania imepoteza wanasiasa nguli kwa kipindi kisichozidi mwenzi mmoja.
Bado nikiwa kama mzalendo na kuweka itikadi pembeni najiuliza nini tatizo?Wapi tumemkosea mungu?

1. Mtoi

2. Mtikila

3. Kombani

4. Makaidi

5. Kigoda

6. Filikunjombe

Dats nonsense....kwan wao ndo waliandikiwa watakufa kipind kisicho cha uchaguzi......when ur day n hour reaches...nowhere to run to...yo soul wil b taken out of your body.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na ambayo hatujawahi kushuudi tanzania imepoteza wanasiasa nguli kwa kipindi kisichozidi mwenzi mmoja.
Bado nikiwa kama mzalendo na kuweka itikadi pembeni najiuliza nini tatizo?Wapi tumemkosea mungu?

1. Mtoi

2. Mtikila

3. Kombani

4. Makaidi

5. Kigoda

6. Filikunjombe

Bado mgombea wa ACT Arusha mjini na kampen meneja wa chadema kanda za juu kusini waliopataga ajali akiwa na mgombea ubunge kama sijakosea ni wa songea huko.Mungu awape pumziko na mwanga wamilele awangazie
 
Jamani hivi vifo kuna nini lakini?!Na Deo kaondoka?!dah!maskini!kwaheri jembe,so painful.mie naanza kuuogopa huu uchaguzi jamani.
 
hata kama walinusurika,inawezekana wameliwa na simba au fisi,wamekaa muda mrefu bila kuokolewa
 
makamba mnamuonea bure enyi watu,,,yeye alikua anafuata ripoti ya ITV waliotangaza kuwa filikunjombe yuko salama...makamba nadhani kwa kuaimini itv,alidhani itv wamestablish contact na deo....sasa hapa anaepaswa kulaumiwa ni itv
Unajiaibisha bure, unajuwa Makamba yupo wizara gani? yani leo sifa ya kuwa mwanaccm ni sharti uwe na mtindio wa Ubongo?
 
Back
Top Bottom