TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Kifo cha deo ni pigo kwa Tanzania nzima

what a visionary young talent
 
Uchaguzi wa mwaka huu????

1 - Mohamed Mtoi
2 - Selina Kombani
3- Mgombea ubunge Arusha
4- Mzee Makaidi
5- Abdalla Kigoda
6- Deo Filikunjombe

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la bwana lihimidiwe
 
Hiyo Tweet ya January sijaisoma, ila kwa jinsi watu wanavyoonyesha kukasirika lazima itakuwa ya hovyo sana. Jambo ambalo wengi ndani ya CCM hawajui ni kuwa pamoja na kuwa Baba yake January Mzee Makamba alikuwa Bogus sana kiasi cha kuitwa Pwagu, huyu mwanae ni zaidi ya baba. Lakini ndani ya CCM mtu akiwa bogus lakini mjanja mjanja basi huwa anachukuliwa ni Think tank. Hasa kama ataonyesha mbinu chafu za kukabiliana na Wapinzani.
Unaweza kushangaa mwenyewe kuwa katika timu ya watu Mashuhuri 32 walioteuliwa na chama kumkampenia mgombea wa chama Tawala (maana lazima uwe mashuhuri na makini) wapo Lusinde na Asumpta Mshama. Hiyo ni kuonyesha hata mtu wa hovyo hovyo kabisa anaweza kuonekana Mahiri kama tuu anaweza kuutukana upinzani bila aibu na kuandaa mbinu chafu.
Ndivyo ilivyo kwa Makamba.

January makamba
 

Attachments

  • 1445003006706.jpg
    1445003006706.jpg
    35.7 KB · Views: 172
Kama ni kweli ni huzuni kupita maelezo. Filikumjombe anakubalika na wengi hata wapinzani au wanamabadiliko.
 
CCM mjifunze sasa, acheni siasa za kuita wenzenu marehemu, maiti etc..
Kila nafsi itaonja mauti, lala salama filikunjombe.
 
Uchaguzi wa mwaka huu????

1 - Mohamed Mtoi
2 - Selina Kombani
3- Mgombea ubunge Arusha
4- Mzee Makaidi
5- Abdalla Kigoda
6- Deo Filikunjombe

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la bwana lihimidiwe
Mkuu umemsahau mchungaji Chris Mtikila.
 
RIP Deo . Ulikuwa kijana mzuri lakini Chama unachokiunga mkono sicho!

sasa naanza kuamini kwamba mungu amekitupa mkono ccm,hakina upako wowote ndio maana ajali NA vifo vimezidi,watubu NA kuomba wakiwa wamevaa magunia
 
Pumzika kwa amani Comrade Deo. Hakika utakumbukwa kwa mchango wako sio tuu kwa wana Ludewa bali pia kwa Taifa kiujumla. Amen.
 
Guys hivi ni kweli Deo kapata ajali na katutoka?
Roho inaniuma sana, tena sana yani kuhusu huyu jamaa. Ni jembe kuliko maelezo.
 
Dah!Sasa Deo alikuwa anafabya kampeni za niniii?

Mbona hiyo hela angeendelea tu kusomesha wake watoto!
Ungeacha wahangaike wa kutafuta kura Deo sio wewe Jembe!
 
TE=babukijana;14354453]Helikopter ilikataa kuruka,badala ya kucheck tecnic failure ikalazimishwa kuruka.only in Bongo


January Makamba ana kesi ya kujibu kazitoa wapi hizo helikopta mara tunasikia Mwigulu alishindwa kuruka ooh Kibajaji aliicha helkopta sijui kijiji gani hiyo ya akina Deo yenyewe ilikataa kuruka bado wakalazimisha kuna akili hapo kweli yaani maisha yao waliona yawekwe rehani kwa ajili ya CCM, chain ya Hashim Rungwe January Makmba na Captain Silaa uone wanavyojineemesha akina Deo ni victims tuu
 
Mwanadamu hawezi kuingia mipango ya MUNGU, katika uchaguzi huu muumba wetu alipanga yatokee hayo, ingawa sisi hatukujua lakini ilikuwa mipango yake ya sirini. Kuna siku nilipata maono kuwa watakufa wanasiasa wanaogombea ubunge wapatao sita (6). Naamini Filikunjombe ametimiza idadi hiyo. TUENDELEE KUMUOMBA MUNGU ALIEPUSHE TAIFA LETU NA MACHAFUKO TUNAPOELEKEA KATIKA UCHAGUZI, maana naliona giza nene likiwa limeifunika nchi yetu kwa muda wa miezi sita.

Thanx 4 notification.
Inatisha Sana, yatupasa kuomba rehema kwa Muumba, yamkini atuepushe na hayo bcz yeye ni mwingi wa rehema na anatuwazia mawazo ya amani.

Sisi sote ni ndugu, poleni sana kwa tukio hili.
 
CCM mjifunze sasa, acheni siasa za kuita wenzenu marehemu, maiti etc..
Kila nafsi itaonja mauti, lala salama filikunjombe.

mkuu umetoa hoja nzito,kauli zao no chukizo mbele za mungu,ninahisi mwenyezi mungu kawategea mgongo ccm
 
Back
Top Bottom