TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Something must be extremely wrong with CCM.Why all these deaths.CCM take care.
(UPDATED 13:30 - October 16, 2015)

Kwa mujibu wa Jerry Silaa (aliyekuwa Meya wa Ilala):


Heshima kwenu Wakuu,

Kuna habari zinasambaa kwamba kuna Chopa ilikua imebeba Makada wa CCM imepotea ikiwa inaelekea Njombe.

Taarifa zinasema, wakati inaondoka ilishindwa kupaa lakini mwisho wa siku ikawa imepaa.

Hadi sasa sijajua kipi ni kipi. Hivo nimeileta hii habari kama tetesi ili mwenye taarifa za mwanzo atujuze.

Asanteni sana.

========
UPDATES:

- JamiiForums imejaribu kumtafuta Filikunjombe kupitia simu yake ya mkononi bila ufanisi
- Taarifa zinabainisha kuwa kweli kuna ajali ya helikopta imetokea lakini mpaka sasa hali za waliokuwa kwenye chombo hicho hazijajulikana
- Baadhi ya abiria wanaodaiwa kuwa ndani ya chombo hicho ambacho kinasemekana kilikuwa kikirushwa na Kapteni Silaa ambaye ni baba Mzazi wa Jerry Slaa, ni Haule (ndugu yake Filikunjombe), Deo Filikunjombe, Mtumishi mmoja wa Halmashauri mojawapo ya Mkoa wa Njombe...
- Jitihada za kufika eneo la ajali zimekuwa ngumu kwakuwa ni eneo ambalo si rahisi kufikika nyakati za usiku; juhudi zinaendelea
- Helikopta iliruka saa tisa ilitakiwa itue saa 11 Iringa. Status ni MISSING. Casualties sio CONFIRMED kwa kuwa ni porini mpaka kesho gari likifika eneo la tukio sababu kuna mto na watu wa camp na rangers hawawezi kuvuka usiku huu.

=> Katika Kituo cha Luninga cha ITV taarifa ya habari saa tano usiku wamethibitisha kutokea kwa ajali ya helkopta ambayo Deo Filikunjombe alikuwa anasafiria lakini wanadai yuko salama

================

- Ndege inayodaiwa kuanguka leo katika Hifadhi za Selou...

View attachment 299341View attachment 299342View attachment 299343View attachment 299344
 
R>I>P wote waliopatwa na janga. Mungu awape nguvu ndugu ,marafiki na wanachama wote wa Lumumba kwa wakati huu mgumu kwao wa majonzi.
Mapenzi yake Bwana binadamu hawezi kutia mkono.
 
sasa naanza kuamini kwamba mungu amekitupa mkono ccm,hakina upako wowote ndio maana ajali NA vifo vimezidi,watubu NA kuomba wakiwa wamevaa magunia
Subiri ndani ya siku hizi tisa zilizobaki,pigo linakuja kwa Chadema pigo la fainali
 
January Makamba ana kesi ya kujibu kazitoa wapi hizo helikopta mara tunasikia Mwigulu alishindwa kuruka ooh Kibajaji aliicha helkopta sijui kijiji gani hiyo ya akina Deo yenyewe ilikataa kuruka bado wakalazimisha kuna akili hapo kweli yaani maisha yao waliona yawekwe rehani kwa ajili ya CCM, chain ya Hashim Rungwe January Makmba na Captain Silaa uone wanavyojineemesha akina Deo ni victims tuu

inawezekana ni helkopta za jeshi LA somalia,hazina rekodi ya kukarabatiwa/service NA pengine marubani hawajasomea hiyo kazi,labda in mafundi gereji tu
 
Milele na daima , Taifa litakukumbuka....

Mungu ailaze mahala pema peponi Deo mpambanaji
 
January kwa kweli nina hofu na uwezo wake wa akili,ni bora angekaa kimya kuliko kutweet habari za uongo,yaani ujinga sana tena sana

Mm nashindwa kuelewa huyu January mbona mropokaji tuu bila kufikiri eti alikuwa tano bora
 
, chain ya Hashim Rungwe January Makmba na Captain Silaa uone wanavyojineemesha akina Deo ni victims tuu[/QUOTE]


Weka vuzuri haijaeleweka
 
Hata kama angesikia CNN au BBC bado ilimlazimu ajiridhishe kwanza kabla ya kukurupuka na kuleta propaganda za kijinga.

Acha uongo kama bosi wako. January Makamba na ITV nani kaanza kutangaza habari ya chopa kuanguka ?
 
R.I.P Deo na ndugu zangu mliokuwa kwenye hii ajali .

Poleni sana ndugu zangu wote mlioguswa kwa njia moja ama nyingine na msiba huu mkubwa

Respect !!!
 
Deo jamani, eeh Mungu why umeliruhusu hili litokee jamani? Nashindwa kuyazuia macho yangu yasitoe machozi, Mungu mpumzishe kwa amani
 
Back
Top Bottom